Uchaguzi 2020 Lissu Maarufu, Nyalandu ana hela, kazi kwa wajumbe

Uchaguzi 2020 Lissu Maarufu, Nyalandu ana hela, kazi kwa wajumbe

Benson Mramba

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2013
Posts
648
Reaction score
1,485
Masoud Kipanya katika kipindi cha Cloud Plus wakati wa kura za maoni za CCM nilimnukuu akisema Wajumbe wa CCM huenda hawakupewa rushwa kabisa lakini walikuwa wanajua Mgombea yupi ana hela kwamba wakimpitisha anaweza kujawashukuru kwa namna yoyote siku za baadae kwa hiyo yeye Masoud aliwapa nafasi kubwa Wagombea Matajiri kuwa watashinda. Na kweli 90% ya walioshinda ni Matajiri na wenye nafasi kubwa serikalini.

Pia walijua Matajiri hawatakuwa na kampeni za kufunga mkanda bali kampeni za kula bata tofauti na maskini ambaye anawaahidi akipata mtakula wote matokeo yake wanawaacha solemba!

Sasa wajumbe wa CHADEMA nao wana mtihani siku chache zijazo! Je wamchague Lissu kupeperusha bendera yao au wamchague Nyalandu?

Lissu ni maarufu sana na mzalendo wa nchi yake. Pamoja na marisasi bado hajakimbilia uhamishoni amerudi nyumbani kama ni kufa afie Tanzania ila hana hela ya kampeni kabisa! Kampeni yake ni wananchi wamchangie. Lakini Chama na viongozi wake hawaaminiki tena kwenye michango. Lissu aunde timu yake ya kampeni haraka yenye watu wanaoaminika kwenye masuala ya fedha sio Mbowe, Mrema na Reggy hawa hawaaminiki na wakiwepo nitaongoza kampeni ya kuzuia michango maana tunawajua.

Changamoto nyingine ya Lissu inaweza kuwa afya. Je ana nguvu na uimara wa kukimbia na magari kwa siku hizi 90+ za kampeni na kutafuta wadhamini? Au atahitaji chopa ambayo ni very expensive na hela hana na Chama pia hakina hela?

Afadhali nyingine ya Lissu ni kuwa Wabunge wanataka kumtumia jina lake kurudi kwenye nafasi zao kwa maslahi yao japo hawamwamini na huenda hata hawampendi ila Baniani mbaya sasa watafanyaje?maana Mbowe na Chama wameshapoteza moral authority kwenye jamii yetu kwa ufisadi na udikteta wao.

Nyalandu nae ni mwana mageuzi aliyeamua kuacha ubunge kwa ajili ya ndoto ya Urais ili awatumikie watanzania. Nyalandu ina aminika ana hela nyingi, za kwake na za wazungu wake huko Marekani na Ulaya. Nyalandu ana mtaji wa kampeni ndivyo wajumbe wanavyoaminishwa.

Sasa je Wajumbe watakwenda na Lissu waendelee na kampeni za kujitoa Mali zao na muda wao? Lissu mwenyewe ana sifa ya Uchoyo na Ubahili kama Mnyika. Apate asipate hakumbuki wenzie.

Au wampe Nyalandu anayeonekana Mlokole Fulani na aliyekulia CCM kwenye siasa za Ukarimu na Takrima? Pia kwa Nyalandu matumaini ya kampeni zenye afueni ni makubwa sana maana inaaminika ana hela na mtandao mkubwa.

Tunawasubiri wajumbe kesho kutwa.
 
Wewe unajuaje maswala ya mtu kwamba ana hela au hana wakati wewe sio cashier wake wala sio mke wake.

Acheni uongo kwani Magufuli ni tajiri mbona yeye hujamwambia aache kugombea kwa sababu sio tajiri.

Kugombea urais mpaka uwe tajiri, mbona Obama alishinda awamu mbili na hakuwa tajiri. Huna hoja wewe, subirini tume yenu iwabebe.
 
tutampitisha mwenye 'mpunga' huyo masikini akae pembeni. Mkono mtupu haulambwi historia inatukumbusha ya 2015
 
Ukisoma mada bila mihemko unaokota kitu hata kama hutaki. Tatizo kuna watu washaset akili zao hawasikii kinyume na wanavyotaka. Kazi zenu hizo za kisiasa mimi sihusiki.
 
Nyalandu apite lissu anaumwa. He is not fit mindcally
 
Wewe unajuaje maswala ya mtu kwamba ana hela au hana wakati wewe sio cashier wake wala sio mke wake.

Acheni uongo kwani Magufuli ni tajiri mbona yeye hujamwambia aache kugombea kwa sababu sio tajiri.

Kugombea urais mpaka uwe tajiri, mbona Obama alishinda awamu mbili na hakuwa tajiri. Huna hoja wewe, subirini tume yenu iwabebe.
Jiandae kisaikolojia. Mbowe kampeni kwake ni mradi. Sasa dili isiyolipa hawezi kuipenda sana
 
Hakuna nchi ambayo mlemavu amewahi kugombea kuwa rais
Kumbuka tunamchagua Amiri Jeshi mkuu

Hakuna nchi ambayo mlemavu amewahi kugombea kuwa rais
Kumbuka tunamchagua Amiri Jeshi mkuu
President Franklin D Roosevelt 32nd Pres of USA. President Mwai Kibaki was on stretchers when he was campaigning after an accident.

Kwani amiri jeshi mkuu anageuka kuwa askari wa miguu? Wacha kunyanyapaa wewe! Mwisho utasema hakuna nchi iliyomsimamisha Zeruzeru kugombea uraisi!
 
Back
Top Bottom