Masoud Kipanya katika kipindi cha Cloud Plus wakati wa kura za maoni za CCM nilimnukuu akisema Wajumbe wa CCM huenda hawakupewa rushwa kabisa lakini walikuwa wanajua Mgombea yupi ana hela kwamba wakimpitisha anaweza kujawashukuru kwa namna yoyote siku za baadae kwa hiyo yeye Masoud aliwapa nafasi kubwa Wagombea Matajiri kuwa watashinda. Na kweli 90% ya walioshinda ni Matajiri na wenye nafasi kubwa serikalini.
Pia walijua Matajiri hawatakuwa na kampeni za kufunga mkanda bali kampeni za kula bata tofauti na maskini ambaye anawaahidi akipata mtakula wote matokeo yake wanawaacha solemba!
Sasa wajumbe wa CHADEMA nao wana mtihani siku chache zijazo! Je wamchague Lissu kupeperusha bendera yao au wamchague Nyalandu?
Lissu ni maarufu sana na mzalendo wa nchi yake. Pamoja na marisasi bado hajakimbilia uhamishoni amerudi nyumbani kama ni kufa afie Tanzania ila hana hela ya kampeni kabisa! Kampeni yake ni wananchi wamchangie. Lakini Chama na viongozi wake hawaaminiki tena kwenye michango. Lissu aunde timu yake ya kampeni haraka yenye watu wanaoaminika kwenye masuala ya fedha sio Mbowe, Mrema na Reggy hawa hawaaminiki na wakiwepo nitaongoza kampeni ya kuzuia michango maana tunawajua.
Changamoto nyingine ya Lissu inaweza kuwa afya. Je ana nguvu na uimara wa kukimbia na magari kwa siku hizi 90+ za kampeni na kutafuta wadhamini? Au atahitaji chopa ambayo ni very expensive na hela hana na Chama pia hakina hela?
Afadhali nyingine ya Lissu ni kuwa Wabunge wanataka kumtumia jina lake kurudi kwenye nafasi zao kwa maslahi yao japo hawamwamini na huenda hata hawampendi ila Baniani mbaya sasa watafanyaje?maana Mbowe na Chama wameshapoteza moral authority kwenye jamii yetu kwa ufisadi na udikteta wao.
Nyalandu nae ni mwana mageuzi aliyeamua kuacha ubunge kwa ajili ya ndoto ya Urais ili awatumikie watanzania. Nyalandu ina aminika ana hela nyingi, za kwake na za wazungu wake huko Marekani na Ulaya. Nyalandu ana mtaji wa kampeni ndivyo wajumbe wanavyoaminishwa.
Sasa je Wajumbe watakwenda na Lissu waendelee na kampeni za kujitoa Mali zao na muda wao? Lissu mwenyewe ana sifa ya Uchoyo na Ubahili kama Mnyika. Apate asipate hakumbuki wenzie.
Au wampe Nyalandu anayeonekana Mlokole Fulani na aliyekulia CCM kwenye siasa za Ukarimu na Takrima? Pia kwa Nyalandu matumaini ya kampeni zenye afueni ni makubwa sana maana inaaminika ana hela na mtandao mkubwa.
Tunawasubiri wajumbe kesho kutwa.
[/QUOTE HUWA mnawapakazia chadema tu ,but nimekifuatilia hichi chama mfumo wake si wa kawaida thats niliwai sikia kwamba chama hichi
kina roho saba japo sijawai jua maana yake , chadema kama chama kwanza kwa kugombea hawaangalii una pesa au la wao la msingi huangalia jinsi unavyo kitumikia chama aijalishi we ni mshona viatu ,ili naliongea maana nimeshuhudia chaguzi nyingi za marudio wa madiwani n.k ,pili umaarufu wa mtu unamata pia .
mfano wakati slaa anagombea urais 2010 alikua Tajiri?
tatu nyarandu na lissu hawa ni ndugu hata lissu akipita usitegemee kama nyarandu hawezi mpigania kamwe ayo ni maneno tu kwa sisi tusiyo yajua ya ndani kwa chama husika.
tatu chadema hakuna alie juu ya chama kisa pesa zako that's angalia hata mfumo wao wa kuwapata viongozi kuanzia kule kwenye uongozi wa kanda si mchezo that's binafsi naamini chadema kwa sasa ni chama bora afrika na hakuna wa kubadilisha mawazo yangu hayo