Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Anasema ana mdomo mpana,

Wanaomshabikia kuna siku atawarudia..

Kama hata vikao vya sir anaropoka mpaka eneo walilofanyia.. imagine ni top boss wa CDM.....

Siasa za upinzani kuendesha chama sio kazi rahisi .

Kuendesha chama kwa kusema tu?

Tupo
umeongea pointless aisee..

yes ni vzuri pia hata akiwarudia wanaomshabikia ikiwa wataenda nje ya mstari!Tunataka mtu wa namna hyo
Being top wa chama ndio uruhusu uongo utawale for the sake of kuwa top!!?
Kwamba kuendesha chama ni kazi kubwa sana ambayo anayeiweza ni Mbowe tu!?Eti huwez endesha chama kwa kusema tu..Watu mnaujinga sana
 
Labda nikujibu kwa kirefu ili upate shule kidogo,
Tofauti kati ya mtu muwazi na mropokaji ni kama ifuatavyo:

Mtu Muwazi

  1. Maana: Huyu ni mtu anayesema ukweli kwa uwazi, lakini kwa hekima na kwa kufuata mipaka ya kile kinachostahili kusemwa.
  2. Tabia:
    • Anaelezea mawazo au hisia zake kwa uwazi na kwa njia inayoheshimu wengine.
    • Hutoa maelezo pale inapohitajika bila kuzidisha.
    • Huzingatia faragha ya watu wengine na mazingira yanayomzunguka.
    • Anakuwa mkweli na wa moja kwa moja, lakini bila kuumiza hisia za watu.
  3. Madhara:
    • Mara nyingi anapendwa kwa sababu ya uaminifu wake.
    • Anaaminika na watu kwa sababu ya uwazi wake wa kufikiria na kusema.

Mropokaji

  1. Maana: Huyu ni mtu anayesema mambo bila kufikiria mara mbili, mara nyingine bila kuzingatia athari za maneno yake.
  2. Tabia:
    • Hutoa habari nyingi, hata zile zisizo na umuhimu au zinazoweza kusababisha madhara.
    • Hajali mipaka ya faragha ya wengine au athari za maneno yake.
    • Anaweza kusema vitu vya siri, visivyotakiwa au vya kufedhehesha.
    • Husema bila kufikiria, mara nyingine akiongea kwa haraka.
  3. Madhara:
    • Mara nyingi huonekana kama mtu asiyeaminika au asiyejali hisia za wengine.
    • Huwa chanzo cha migogoro, fitina, au kutokuaminiana.
    • Anaweza kupoteza heshima kwa sababu ya tabia yake ya kuropoka bila busara.
Kwa ufupi, muwazi ni mwenye busara katika kusema, wakati mropokaji hana mipaka wala umakini. Tofauti kubwa ni hekima na uangalifu katika mawasiliano.
Mifano ya waropokaji;
1. Kibajaji
2. Msukuma
3. Ntobi
4.
5.
 
Sidhani kama Mbowe anataka kugombea urais. Na inawezekana kuwa ni kweli alikuwa hajaamua kugombea uenyekiti. Mimi nahisi alifanya uamuzi wa kugombea baada ya lugha za kebehi dhidi yake kusheheni mitandaoni. Naamini alikuwa chini ya presha kubwa kutoka kwa ndugu na jamaa za kumtaka asigombee. Ni zile alizoita character assassinations ndio zilimsukuma afanye huo uamuzi.

Kazi sasa ni kwa wapiga kura. Ukweli haya mambo ya vijembe yanasikitisha na yanachosha.

Amandla...
Sasa kama ni hivyo kwanini amzuie Lissu asigombee chochote kati ya uenyekiti au urais?
 
Mbowe anaamini kabisa kuwa CHADEMA ni chama CHAKE BINAFSI.
Mkuu, unani kumbusha enzi hizo huko Malawi. "Aliekuwa Rais wa Malawi Mh H.K. Banda - RIP, alifunguliwa mashitaka; wakati anasomewa mashitaka yake na Mheshimiwa Jaji kwamba " Unashitakiwa na Rais wa Malawi kwa makosa ya .........." Rais Banda alishutuka sana na aka wauliza mawakili wake kwamba, huyo ni Rais gani tena! wakati mimi sijui jambo hilo" Kwa heshima mawakili walimtuliza na kumtaka atulie ....; Mkuu, haya ndio madhara ya kukaa madarakani bila kufuata taratibu na sheria muda mrefu na hivyo kujiona wewe ni wewe tu hamna mwingine zaidi yako. Haya ndio leo tuna yaona sasa, ndani CHADEMA hii.
 
Sasa kama ni hivyo kwanini amzuie Lissu asigombee chochote kati ya uenyekiti au urais?
Hivyo ndivyo ulivyomuelewa Lissu. Lissu alitangaza nia ya kugombea urais kitambo tu na sijamsikia kiongozi yeye akimkemea kwenye hilo. Mbowe hana tatizo na Lissu kugombea urais. Alichosema kuwa unahitajika muda ni yeye kuamua kama anataka kugombea urais kama ambavyo Lissu alipendekeza. Hivyo hivyo kwenye kugombea Uenyekiti. Hapa shida ilikuwa ni Lissu kutaka kugombea nafasi hiyo tu. Kwa maneno yake mwenyewe, yeye ndiye alimtaka Mbowe agombee urais na Uenyekiti amuachie yeye. Hapo nani kazuiwa? Lissu haaminiki.

Amandla...
 
Dah! Jabali la siasa za upinzani anapelekewa moto sio poa na huyu mnyampaa.... tusubiri kauli ya Mbowe kupitia Yericko Nyerere na wenzae Ntobi.
Huyo Yericko Nyerere kuna kitu Cha maana anachofahamu? Lile ni bumunda, yuko pale kwa mbowe akisubiri atupiwe chochote kitu ili maisha yaende, huwa naona aibu mie kwa nwanaune mtu mzima kujidhalilisha nanna hiyo, kama yeye (Yericko) anakuwa na njaa namna hiyo, vipi wa Tanzania wengi wanaoishi maisha magumu! Huyo akiambiwa kuolewa si atakubali ili maisha yaende.
 
Nani ataamini?
Kwa nini usiamini maneno ya Lissu wakati keshasema wakati wa viako hivyo vyote 3, John Mnyika ni shahidi?
Utaonekana wa ajabu umuamimi Mbowe aliyetaka hivyo viako viwe siri ili rahisi kwake kudanganya umma.
Waingereza wana msemo ...writings are on the wall.....,wakimaanisha hata kwa mtiririko kadhaa wa vitendo vya Mbowe kama mwenyekiti siku hizo za karibuni zimetosha kutilia mashaka.
Kuanzia kuiingiza Chadema katika uchaguzi na kuondoka katika msimamo wa awali wa hadi katiba mpya ipatikane kwanza kisha akasingizia kamati kuu...na kumsifia sana Samia na muafaka wao hauna tija kabisa uhai wa vyama vya upinzani kiasi cha chadema kuonekana kama CUF.
 
Hivi kwanini Mbowe anang'ang'ania pale? Kwani kuna nini hasa?
Mlishaambiwa mapema ila watu hamkuwa attentive tu.
Koufupi,Mbowe amekuwa sold out...
.amelambishwa asali nzito ambayo kwa hulka yake asingeweza kuikataa kwa kufanya kazi 2..
1: Kuhakikisha Chadema inakuwa dhaifu kadiri.
2: Kuhakikisha samia hapati hawekewi mgombea mwenye nguvu.
 
Hapana, Lissu anatambua vyema kipi ni siri ila hauwezi ukayatumia ya sirini kutaka kumpiga halafu yeye akae kimya.
Mbowe hakupaswa kumshambulia Lissu kuwa anataka vyote na kwamba uamuzi wake wa kugombea ulikuwa ni wa 'ghafla sana' wakati akijua walikutana faragha na kulikuwa na makubaliano.

Kwanini aongee uongo? Kama Lissu angekuwa ni mtoa siri basi hili angeliongea tangu wakati ule anachukua form.
LIssu ameongea na kuhojiwa mara nyingi sana lakini hakuwahi kuonyesha dalili yoyote kwamba kulikuwa na maongezi yoyote baina yao, ni Mbowe ambaye katekenywa kidogo tu, anatoa kauli zinzopelekea yaliyo sirini kuvuja sababu alitaka kuutumia usiri ule kujiweka salama akijifanya 'Mr. Smart'.

Lissu hakuwahi kumshambulia Mbowe, ila inaonekana Mbowe hawezi kujieleza akaeleweka bila ya kumshambulia Lissu
Hii uliyoandika ndio ukweli na hali halisi ilivyo.
Ni kipofu wa akili pekee ambaye hajaelewa hili.
 
Hivi kwanini Mbowe anang'ang'ania pale? Kwani kuna nini hasa?
Lazima ang'ang'anie ili kutimiza matakwa ya asali nzito aliyopewa.
Ukweli ni kwamba Mbowe alidhapanga kutogombea kipindi hiki ns alishadokeza hilo kabla wakati fulani.
Kilichomfanya abadili mawazo ni kutimiza matakwa ya maridhiano yake bonafsi na Samia....
1; Ahakikishe upinzani unakuwa dormant na wasidai katiba mpya
2:;Samia asiwekewe mpinzani toka katika chama pinzani chenye nguvu.
Ina maana katika kuhakikisha hayo ni lazima yeye abaki kuwa mwenyekiti kwa miaka hii 5 mingine
 
Anasema ana mdomo mpana,

Wanaomshabikia kuna siku atawarudia..

Kama hata vikao vya sir anaropoka mpaka eneo walilofanyia.. imagine ni top boss wa CDM.....

Siasa za upinzani kuendesha chama sio kazi rahisi .

Kuendesha chama kwa kusema tu?

Tupo
Fortilo wewe ni ccm kwa nini unapinga lissu kuwa mwenyekiti chadema? Unawaonea huruma chadema?
 
Back
Top Bottom