Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hadi naona shida nianzie wapi kukuelemisha, tafuta taarifa kwanini Lissu aliamua kubadili mawazo na kugombea nafasi ya Uwenyekiti.

Mbowe alijipanga kumfanyia uhuni makamu wake. Alipanga kuanza na kumpoka nafasi ya umakamu kisha kumnyima nafasi ya kugombea Urais.

Lissu akashtuka mapema naye akabadili mawazo, ndio hii imekuwa vita sasa.
Mbowe anajifanya mtoto wa mjini huku akijinufaisha binafsi kwa mgongo wa chama.
Amekutana ni kisiki cha mpingu toka Singida na sio Mtwara.🤣
 
Anasema ana mdomo mpana,

Wanaomshabikia kuna siku atawarudia..

Kama hata vikao vya sir anaropoka mpaka eneo walilofanyia.. imagine ni top boss wa CDM.....

Siasa za upinzani kuendesha chama sio kazi rahisi .

Kuendesha chama kwa kusema tu?

Tupo
Tofauti ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu (ingalau kwenye hili) ni ipi...?

Tatizo kubwa ninaliliona la Freeman Mbowe ni kutokuwa mkweli..

Alishindwa nini siku ile ya interview yake kuweka mambo wazi walijadili nini kwenye vikao na wakakubaliana nini na mwenzake? Kwani kuna siri gani hapo? Huyu ndiye mtu mnayesema ana busara...?

Hakuna busara kwa kiongozi wa njia mbilimbili. Kiongozi wa sitaki-nataka...!!

Mtu unajiuliza ikawaje akajenga utetezi wake ktk namna ya kumtweza na kumjengea mwenzake picha ya kuonekana ni mtu asiyeheshimu makubaliano..?

Katika hili kwanini tuone ajabu Tundu Lissu kuijibu hoja shambulizi hilo kwa namna hii alivyojibu? Huwezi kumstahi mtu mdanganyifu asiyesema kweli...!

Ni kweli Tundu Lissu ana mdomo mpana usioweza kuhimili kukaa na vitu au mambo ya hovyo...

Kama unafanya naye kazi, usiwe mtu wa konakona, kuwa straight na hapo mtaenda pamoja...

Otherwise, ukiwa na longolongo nyingi, atakulipua tu hata kama wewe ni baba yake...

Kwa maoni yangu, huyu mtu ni mzuri sana. Mkiwa naye kwenye utendaji, mta - achieve malengo yetu haraka bila stress...
 
Hadi naona shida nianzie wapi kukuelemisha, tafuta taarifa kwanini Lissu aliamua kubadili mawazo na kugombea nafasi ya Uwenyekiti.

Mbowe alijipanga kumfanyia uhuni makamu wake. Alipanga kuanza na kumpoka nafasi ya umakamu kisha kumnyima nafasi ya kugombea Urais.

Lissu akashtuka mapema naye akabadili mawazo, ndio hii imekuwa vita sasa.
Hili linaweza kuwa na ukweli mkubwa sana, kwani endapo asingegombea nafasi ya M/kiti kwenye nafasi ya makamu m/kiti tayari alikuwa ameandaliwa Wenje, nafasi ya raisi angeingia mwamba mwenyewe, kwa hiyo automatically TAL angekuwa NO BODY ndani ya chama na hilo pengine lingekuwa anguko lake la kisiasa, this might be a planned game. Jamaa kaamua kupindua meza mbwayi na iwe mbwayi. The guy is so smart and led by smart syndicate.
 
Sidhani kama Mbowe anataka kugombea urais. Na inawezekana kuwa ni kweli alikuwa hajaamua kugombea uenyekiti. Mimi nahisi alifanya uamuzi wa kugombea baada ya lugha za kebehi dhidi yake kusheheni mitandaoni. Naamini alikuwa chini ya presha kubwa kutoka kwa ndugu na jamaa za kumtaka asigombee. Ni zile alizoita character assassinations ndio zilimsukuma afanye huo uamuzi.

Kazi sasa ni kwa wapiga kura. Ukweli haya mambo ya vijembe yanasikitisha na yanachosha.

Amandla...
Huu ndio utetezi dhidi yake..?

Akubali tu kuwa hata baada ya kuwa kwenye kiti cha uongozi wa chama kwa miaka zaidi 20, hakuweza kuandaa mtu wa kuja kuchukua nafasi yake...

Huu ni udhaifu mkubwa na mbaya sana wa Freeman Mbowe...

Hii Inaweza kuthibitisha ukweli wa tuhuma ya yeye na genge lake kukitumia chama kama kitega uchumi wake cha kumpatia fedha...

Hoja kuwa aliona kuwa anasemwa na kushambuliwa sana ndio maana akaamua kugombea ni hoja dhaifu isiyo na mantiki yoyote hata kwa kichaa tu...

Kuna mengine yako nyuma ya uamuzi wake. Na yatabumbululuka tu na tayari kidogodogo yanaanza ku - unfold...
 
Back
Top Bottom