Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu mbona unanipa Chama kabisa...

Kwa record ipi?
Kwa nini sasa hivi ufiche chama chako wakati ulikua unakiweka wazi?
Screenshot_20250106-160549_1.jpg
 
kwa tunaojua kusoma lugha ya usoni, unaona kabisa DJ anayoyaongea yanatoka usoni hayatoki moyoni, binafsi huwa siwezi kuidanganya nafsi kama anavyofanya yule jamaa. you can fool people for sometime but will never full them forever, watanzania waliokunja ngumi kwa miaka mingi, sio wajinga, wana akili na kisomo kuliko yeye aliyeishia uDJ bilicanas. watu wamepoteza maisha, wamepoteza kazi, wamekuwa vilema, wamedhalilishwa, wamefilisika afu unakuja kuleta utoto kwenye mambo ya msingi? kweli?
 
Kama ni hivyo, kwa nini Mbowe hataki kugombea?

Amandla...

..labda ni biashara kwa maana wenye pesa zao wanafika dau?

..kwamba wanachadema wanateseka kupigania na kujenga chama halafu analetwa mtu mwenye dau kubwa ananunua nafasi ya kugombea Uraisi?
 
Kilichomfanya abadili mawazo ni kutimiza matakwa ya maridhiano yake bonafsi na Samia....
1; Ahakikishe upinzani unakuwa dormant na wasidai katiba mpya
2:;Samia asiwekewe mpinzani toka katika chama pinzani chenye nguvu.
Ina maana katika kuhakikisha hayo ni lazima yeye abaki kuwa mwenyekiti kwa miaka hii 5 mingine

lkn raisi Samia hatogombea 2025 …
 
Nafasi ya mgombea uRais pale Chadema ni biashara

Kwa Sasa wanawavizia February na Dr Naniliu PhD 😂😂😂
Naam Jamaa ana mkataza lissu asigombee ili Aje apige hela kama alivyo Fanya Kwa Lowasa , Yule macho kumchuzi mjanja mjanja sana
 
Wakuu

Kimeumana CHADEMA, Tundu Lissu amvaa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe baada ya kurejea Tanzania kutoka nchini Ubeligiji.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuulizwa kuhusu alichokisema Mbowe kuwa walishauriana asigombee Uenyekiti CHADEMA, pengine baadae angegombea Urais

Soma, Pia: Mbowe: Ilikuwa ghafla sana Lissu kutangaza kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa

"Kwanza hili niliseme kwa masikitiko, kwasababu si jambo nzuri kusema Mwenyekiti (Freeman Mbowe) amesema uongo, kwenye hili amesema uongo. Tulikutana kwa siku tatu hapa Msimbazi, Kanisani tukipatanishwa, tukizungumza juu ya hiki kinyang’anyiro na kwa siku tatu zote Mwenyekiti alisema yeye hajaamua kugombea nafasi yoyote [kwa siku tatu], Katibu Mkuu John Mnyika ni shahidi…."
View attachment 3194110
 

Attachments

  • VID-20250106-WA0032.mp4
    6.3 MB
Hamna kitu kibaya hapa duniani kama kuwa upande wa pili wa Lissu( Na uzuri wa Lissu huwa hana konakona, hata ukimwambia hii ni siri kuna siku utaikuta gazetini)

..somo hapa ni kwamba usijaribu kumshirikisha dili chafu. Lissu atakulipua.

..usiingie mapatano naye halafu ukatoka nje ukajaribu kupotosha ukitegemea " atamezea. "
 
Back
Top Bottom