Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huo ni mtizamo wako. Mimi siamini kama Chadema ingemsimamisha Slaa ingepata mafanikio waliyopata walipomsimamisha Lowassa. Nakubali kuwa nae Lowassa alisaidiwa kwa kupata platform ya kugombea. Wote walifaidika ingawa Lowassa aliumia zaidi kwa sababu alitaka sana awe rais.

Inawezekana uko sahihi. Lakini kama nilivyosema, Lowassa alikuwa na extensive network nchini ya watu waliomkubali toka alipokuwa Waziri Mkuu. Kulikuwa na watu wengi tuu CCM ambao waliamini kuwa alionewa kwa kunyimwa nafasi ya kugombea urais. Watu hawa hata siku moja wasingeweza kumpigia debe na hatimae kumpigia kura Slaa lakini kwa Lowassa waliweza.

Hoja ya ufisadi kweli ilikuwa hoja kuu lakini sidhani kama wananchi wengi wa kawaida waliijali sana. Ni kama vile humu ndani watu wamepiga kelele sana kuhusu kuuzwa kwa Bandari lakini mwananchi wa kawaida anachotaka kujua ni kuhusu kula yake ya kesho. Bread and butter issues kwa maneno mengine.

Kwani ataachana na hizo harakati akishindwa kwenye uchaguzi? Yaani hawezi kuchangia asipokuwa Mwenyekiti? Hata kama Heche atamrithi nafasi ya Makamu Mwenyekiti? Hapa si atakuwa ameweka mbele ego yake?

Tundu Lissu atajitoa mwenyewe. Kwa hulka ya Mbowe ya pragmatism, kama atashinda atajaribu kumtumia kikamilifu. Lissu ni tofauti. Akishindwa anaweza kususa. Akishinda anaweza kuwa mtu wa visasi. Si umemsikia leo anahoji utajiri wa Mbowe! Leo anaweza kudai kuwa biashara za Mbowe hazina TIN number? Sitashangaa kama kesho atadai kuwa Mbowe hakuwemo hata katika ndege iliyompeleka Nairobi! Aliisha anza kwa kudai kuwa ni Msigwa ndie aliyeshika chupa ya drip sio Mbowe. Kinachofuata ni kumshushia mzigo wa kuhusika kwa watu wa Chadema kuuawa, kupotea na yeye kupigwa risasi. Amaisha muingiza kinamna Marehemu Kibao. Lissu sio huyo mnaemdhania kuwa atawafikisha katika nchi ya ahadi.

Nasikitika kuwa Lissu amechangia sana kwenye hili. Historia itamhukumu vibaya.

Amandla...

..hapo kwenye jinsi safari ya kumpeleka Nairobi Lissu hajawahi kukana kwamba Mbowe na Msigwa walikuwa naye kwenye ndege.

..hiyo ya kusema Mbowe alishika drip, na Msigwa alishika mtungi wa gesi, or vice versa ni suala ambalo yeyote anaweza kulichanganya, siamini kama Lissu alikuwa na nia ya kumkana au kudogosha mchango wa Mbowe.

..kuhusu masuala ya biashara za Mbowe, Lissu alikuwa akizungumzia kwa muktadha wa biashara kuchangia chama. Je, ni kweli Chadema imekuwa ikiendeshwa kwa kutumia biashara za Mbowe? Bila kujali kama ni kweli au sio kweli nadhani Chadema inapaswa kutafuta namna yenye uwazi zaidi katika kuendesha chama.

..kuhusu Lissu na harakati za Katiba naamini mchango wake utakuwa mkubwa zaidi ikiwa atatumia jukwaa la Chadema kuliko akiwa nje. Pia naamini faida za Lissu kuwa ndani ya Chadema ni kubwa kuliko akiwa nje.

..Kuna jambo limetokea kati ya Mbowe na Lissu. Naamini jambo hilo halina afya kwa Chadema. Ushahidi ni hayo madai kwamba walikwenda kusuluhishwa kwa viongozi wa Dini.

NB:

..Mbowe ametoa mchango mkubwa kuijenga Chadema. Lakini kwa sasa hivi haonekani kuwa na nguvu za kiakili na kimwili kuendelea kuwa Mwenyekiti. Kwa mtizamo wangu amechoka.
 
Mzee wa Posta Club anakabwa kila kona

Umri umeenda akubali tu Asitake kumuiga JK 😄😄

JK mavumba yamo hana Njaa 😂
Hahaha ya kushindana na JK ni sawa sawa na kumuiga tembo kunya mkuu 😀😀😀

JK anamuacha mbali Mbowe kwa sababu ya sifa kuu tatu.

1. Mtoto wa mjini
2. Mswahili original
3. Elimu yake ya chuo na zile siasa za toka enzi za Nyerere vinamfanya awe mjanja zaidi ya Mbowe.
 
..hapo kwenye jinsi safari ya kumpeleka Nairobi Lissu hajawahi kukana kwamba Mbowe na Msigwa walikuwa naye kwenye ndege.
Safari ya kukana inaanza taratibu.
..hiyo ya kusema Mbowe alishika drip, na Msigwa alishika mtungi wa gesi, or vice versa ni suala ambalo yeyote anaweza kulichanganya, siamini kama Lissu alikuwa na nia ya kumkana au kudogosha mchango wa Mbowe.
Alikuwa na sababu gani kuizungumzia kama sio kuonyesha mchango wa Mbowe haukuwa mkubwa kama watu wanavyoamini. Sio kila kitu lazima akizungumzie hasa akijua kuna uwezekano mkubwa wa kutafsiri. Alitakiwa kujua kuwa kuna juhudi kubwa za kumgombanisha na Mbowe. Sasa amefanikisha hizo juhudi.
..kuhusu masuala ya biashara za Mbowe, Lissu alikuwa akizungumzia kwa muktadha wa biashara kuchangia chama. Je, ni kweli Chadema imekuwa ikiendeshwa kwa kutumia biashara za Mbowe? Bila kujali kama ni kweli au sio kweli nadhani Chadema inapaswa kutafuta namna yenye uwazi zaidi katika kuendesha chama.
Hili kalizungumzia leo alipoulizwa kuhusu kuchangia milioni 30 kwa ajili ya kufanikisha mkutano mkuu. Akapiga chenga sana halafu akachomekea hilo la watu wanaochangia pesa nyingi lakini hamna anaejua TIN za biashara zao, ofisi zao n.k. Hapa tena amekuwa unnecessarily petty. Vyama vya siasa kwa muondo wake haviwezi kufanya biashara. Vyama karibu vyote vya siasa duniani (isipokuwa vilivyokuwa sehemu ya dola) ni omba omba. Hata Marekani vinategemea ufadhili wa watu ili kuweza kujiendesha. Sifa kubwa ya kiongozi kule ni uwezo wake wa kuchangisha fedha. Katika mfumo wetu, ni watu wachache (pamoja na makampuni yao) wenye uwezo wa kifedha ambao wako tayari kuchangia vyama vya upinzani kwa uwazi. Kuna mtu aliwahi kuwaambia wafanya biashara kuwa wasitegemee kupata leseni kirahisi kama watawachangia wapinzani. Ndio maana ninasubiri kwa hamu ufafanuzi wa hizo njia mbadala alizozungumzia Lissu.
..kuhusu Lissu na harakati za Katiba naamini mchango wake utakuwa mkubwa zaidi ikiwa atatumia jukwaa la Chadema kuliko akiwa nje. Pia naamini faida za Lissu kuwa ndani ya Chadema ni kubwa kuliko akiwa nje.
Mbona amesema hatatoka Chadema? Na sidhani hata akishindwa kama kuna mtu atamzuia kutumia jukwaa la Chadema katika harakati za kudai Katiba Mpya. Labda kama atasusa mwenyewe.
..Kuna jambo limetokea kati ya Mbowe na Lissu. Naamini jambo hilo halina afya kwa Chadema. Ushahidi ni hayo madai kwamba walikwenda kusuluhishwa kwa viongozi wa Dini.
Kabisa. Na siku zinavyoenda ndio kunazidi kuchimbika. Kwa mtazamo wangu Mbowe anajaribu kupunguza joto lakini Lissu anaona hii ndio nafasi ya kumkata koromeo! Anatakiwa ajue vitu gani ni vya ku share na jamii na vipi vya kumezea. Inasikitisha sana.
NB:

..Mbowe ametoa mchango mkubwa kuijenga Chadema. Lakini kwa sasa hivi haonekani kuwa na nguvu za kiakili na kimwili kuendelea kuwa Mwenyekiti. Kwa mtizamo wangu amechoka.
Inawezekana amechoka lakini sio kiakili. Toka mwanzo Mbowe anataka kuwa Kobe anayemaliza safari wakati kuna wale wanataka wawe kama sungura. Mimi nilianza kumshtukia Lissu alipokaa kimya wakati machawa wake wanabeza mchango wa Mbowe katika kuijenga Chadema. Machawa wa Lissu wamemuita Mbowe king'ang'anizi, mlamba asali, msaliti n.k. lakini amekaa kimyaaaa. Leo mwenyewe kamuongezea sifa ya uongo. Hili nadhani ndio linalo muumiza Mbowe. Na ndio litaleta mpasuko ndani ya chama ambao Lissu hana skills za kuutibu. Kwake yeye compromise ni udhaifu. Kwa sababu hiyo naamini uongozi wake utakuwa wa ki authoritarian. Ukimpinga anakukumbusha ushindi wa kishindo alioupata. Atawakwaza wengi sana. Labda Heche ataweza kumtuliza. Lakini nae kwa hotuba yake ya jana nadhani atakuwa na msimamo huo huo.

Amandla...
 
Lisu sio wa kumuamini..aliwahi kusingizia eti jiwe alimkwida akampiga mitama wakiwa chuo kikuu
 
Kasema Mbowe ni muongo na shahidi yake ni Mnyika. Hivyo kama Lisu ni muongo basi tutamsikia Mbowe mwenyewe au Mnyika akikanusha alichoongea Lisu.
 
Hizi ni aibu gani Mbowe? Ona sasa unadhalilika mchana kweupe.

Hapa ndipo ninapomkubali Lissu, hajui kutafuna maneno.
Kwani Mbowe angesema tu kuwa kwasasa hagombei anapumzika na kumwachia mwingine yote haya yangetoka wapi?
 
Makengeza huwa namwangalia sana anapopambana kwa kurusha maneno ya kishenzi na mtu aliyetangulia mbele ya haki hayati Magufuli ambaye hawezi kujitetea.Kumekucha, mbowe pambana na walio hai wanaoweza kuongea chochote akina Lissu
 
Safari ya kukana inaanza taratibu.

Alikuwa na sababu gani kuizungumzia kama sio kuonyesha mchango wa Mbowe haukuwa mkubwa kama watu wanavyoamini. Sio kila kitu lazima akizungumzie hasa akijua kuna uwezekano mkubwa wa kutafsiri. Alitakiwa kujua kuwa kuna juhudi kubwa za kumgombanisha na Mbowe. Sasa amefanikisha hizo juhudi.

Hili kalizungumzia leo alipoulizwa kuhusu kuchangia milioni 30 kwa ajili ya kufanikisha mkutano mkuu. Akapiga chenga sana halafu akachomekea hilo la watu wanaochangia pesa nyingi lakini hamna anaejua TIN za biashara zao, ofisi zao n.k. Hapa tena amekuwa unnecessarily petty. Vyama vya siasa kwa muondo wake haviwezi kufanya biashara. Vyama karibu vyote vya siasa duniani (isipokuwa vilivyokuwa sehemu ya dola) ni omba omba. Hata Marekani vinategemea ufadhili wa watu ili kuweza kujiendesha. Sifa kubwa ya kiongozi kule ni uwezo wake wa kuchangisha fedha. Katika mfumo wetu, ni watu wachache (pamoja na makampuni yao) wenye uwezo wa kifedha ambao wako tayari kuchangia vyama vya upinzani kwa uwazi. Kuna mtu aliwahi kuwaambia wafanya biashara kuwa wasitegemee kupata leseni kirahisi kama watawachangia wapinzani. Ndio maana ninasubiri kwa hamu ufafanuzi wa hizo njia mbadala alizozungumzia Lissu.

Mbona amesema hatatoka Chadema? Na sidhani hata akishindwa kama kuna mtu atamzuia kutumia jukwaa la Chadema katika harakati za kudai Katiba Mpya. Labda kama atasusa mwenyewe.

Kabisa. Na siku zinavyoenda ndio kunazidi kuchimbika. Kwa mtazamo wangu Mbowe anajaribu kupunguza joto lakini Lissu anaona hii ndio nafasi ya kumkata koromeo! Anatakiwa ajue vitu gani ni vya ku share na jamii na vipi vya kumezea. Inasikitisha sana.

Inawezekana amechoka lakini sio kiakili. Toka mwanzo Mbowe anataka kuwa Kobe anayemaliza safari wakati kuna wale wanataka wawe kama sungura. Mimi nilianza kumshtukia Mbowe alipokaa kimya wakati machawa wake wanabeza mchango wa Mbowe katika kuijenga Chadema. Machawa wa Lissu wamemuita Mbowe king'ang'anizi, mlamba asali, msaliti n.k. lakini amekaa kimyaaaa. Leo mwenyewe kamuongezea sifa ya uongo. Hili nadhani ndio linalo muumiza Mbowe. Na ndio litaleta mpasuko ndani ya chama ambao Lissu hana skills za kuutibu. Kwake yeye compromise ni udhaifu. Kwa sababu hiyo naamini uongozi wake utakuwa wa ki authoritarian. Ukimpinga anakukumbusha ushindi wa kishindo alioupata. Atawakwaza wengi sana. Labda Heche ataweza kumtuliza. Lakini nae kwa hotuba yake ya jana nadhani atakuwa na msimamo huo huo.

Amandla...

..Mbowe naye anaamini anapaswa kuabudiwa na wote aliowasaidia kifedha huko nyuma.

..muda mwingi anautumia kuelezea fadhila zake kwa viongozi wenzake, na chama, badala ya kutoa muongozo wa wapi anataka kukipeleka chama ikiwa atapewa miaka mitano mingine.

..kwa kweli hapa tulipofikia Mbowe hana jambo jipya la kuwaambia wanachadema, na Watanzania. Mwamba amechoka kifikra na kimwili. Ni vizuri akapumzika abaki kuwa mshauri.
 
Ameanza kusema hivyo watu walivyoanza kudai kuwa hana mchango wowote kwa chama. Mimi sijamsikia akizungumzia kukaa kwake jela wakati mgombea wako kila wakati anatukumbusha kuwa anatembea na risasi mwilini.

Sidhani kama ana haja ya kusema chochote kama anaamini kuwa chama chake kiko katika njia sahihi.

Mimi nisingemshauri abakie kama mshauri wa CDM kama atashindwa kwenye uchaguzi. Akifanya hivyo hawachelea kumshutumu kuwa anataka kuwahujumu. Wanaweza hata kumpelekea watu watakaojifanya wanataka ushauri halafu wakamgeuka na kudai kuwa anaufanyia hujuma uongozi mpya. Akishindwa, achukue family yake na aende nao kutalii duniani. Ajichimbie mahali, ajisomee na aandike historia ya maisha yake. Arudi DSM kupiga kura tu. Baada ya uchaguzi Mkuu ndio aanze kuhudhuria vikao vya Kamati Kuu ya CDM.

..mchango wake ni fedha, fedha, fedha. Kwanini hazungumzii mambo mengine?

..Mbowe anapaswa kueleza vision yake kwa miaka 5 ijayo, badala ya kutumia muda mwingi kuzodoa aliowasaidia kifedha.

..ndio maana nakwambia Mbowe amechoka kifikra na kimwili.
 
Hivi kuna mchango mkubwa katika vyama vya siasa kama fedha? Unadhani CDM ingeweza kuwa na kiburi cha kukataa ruzuku bila fedha? Ila kama unadhani mchango wa Mbowe ni fedha tu basi tatizo ni kubwa.

Amuelezee nani? Kuna mahali pa kuelezea vision yake. Sio kwenye public. Ataielezea wakati anaomba kura kuwa Mwenyekiti wa chama chake kwa muhula mwengine. Wagombea si mpaka wapitishwe na Kamati Kuu? Basi huko ndiko atawaelezea vision zake na kwa nini anadhani kuwa Lissu hafai. Sisi wengine tungojee tu matokeo ya uchaguzi.

..kama fedha ndio kila kitu basi Mbowe angetumia hiyo mihela yake tuona atafika wapi ktk siasa za nchi hii.

..Mbowe na wagombea wote wanapaswa kueleza vision yao ya miaka 5 ijayo kwa wanachama, mashabiki, na wapenzi, wa Chadema.
 
Ukweli wa hilo utajulikana baada ya Lissu kushinda. Tutaona CDM itakavyojiendesha kwa hizo njia mbadala. I fervently hope Mbowe ataenda likizo pamoja na mihela yake.

Wataeleza lakini kwa watu wanaowapigia kura. Atakaeshinda ndie atakuwa na wajibu wa kuwaeleza wanachama, mashabiki, na wapenzi wa Chadema. Pamoja hata na wale ambao kwa sasa sio wapenzi wa CDM. Sasa hivi sio wakati wake.

Amandla...
 
Mbowe na team yako, hata kama Lissu hatapita, ila amewavua nguo. Usanii wenu umeshajulikana. Aibu zenu, ila hasa aibu yako wewe Mbowe.
 
Back
Top Bottom