Huo ni mtizamo wako. Mimi siamini kama Chadema ingemsimamisha Slaa ingepata mafanikio waliyopata walipomsimamisha Lowassa. Nakubali kuwa nae Lowassa alisaidiwa kwa kupata platform ya kugombea. Wote walifaidika ingawa Lowassa aliumia zaidi kwa sababu alitaka sana awe rais.
Inawezekana uko sahihi. Lakini kama nilivyosema, Lowassa alikuwa na extensive network nchini ya watu waliomkubali toka alipokuwa Waziri Mkuu. Kulikuwa na watu wengi tuu CCM ambao waliamini kuwa alionewa kwa kunyimwa nafasi ya kugombea urais. Watu hawa hata siku moja wasingeweza kumpigia debe na hatimae kumpigia kura Slaa lakini kwa Lowassa waliweza.
Hoja ya ufisadi kweli ilikuwa hoja kuu lakini sidhani kama wananchi wengi wa kawaida waliijali sana. Ni kama vile humu ndani watu wamepiga kelele sana kuhusu kuuzwa kwa Bandari lakini mwananchi wa kawaida anachotaka kujua ni kuhusu kula yake ya kesho. Bread and butter issues kwa maneno mengine.
Kwani ataachana na hizo harakati akishindwa kwenye uchaguzi? Yaani hawezi kuchangia asipokuwa Mwenyekiti? Hata kama Heche atamrithi nafasi ya Makamu Mwenyekiti? Hapa si atakuwa ameweka mbele ego yake?
Tundu Lissu atajitoa mwenyewe. Kwa hulka ya Mbowe ya pragmatism, kama atashinda atajaribu kumtumia kikamilifu. Lissu ni tofauti. Akishindwa anaweza kususa. Akishinda anaweza kuwa mtu wa visasi. Si umemsikia leo anahoji utajiri wa Mbowe! Leo anaweza kudai kuwa biashara za Mbowe hazina TIN number? Sitashangaa kama kesho atadai kuwa Mbowe hakuwemo hata katika ndege iliyompeleka Nairobi! Aliisha anza kwa kudai kuwa ni Msigwa ndie aliyeshika chupa ya drip sio Mbowe. Kinachofuata ni kumshushia mzigo wa kuhusika kwa watu wa Chadema kuuawa, kupotea na yeye kupigwa risasi. Amaisha muingiza kinamna Marehemu Kibao. Lissu sio huyo mnaemdhania kuwa atawafikisha katika nchi ya ahadi.
Nasikitika kuwa Lissu amechangia sana kwenye hili. Historia itamhukumu vibaya.
Amandla...
..hapo kwenye jinsi safari ya kumpeleka Nairobi Lissu hajawahi kukana kwamba Mbowe na Msigwa walikuwa naye kwenye ndege.
..hiyo ya kusema Mbowe alishika drip, na Msigwa alishika mtungi wa gesi, or vice versa ni suala ambalo yeyote anaweza kulichanganya, siamini kama Lissu alikuwa na nia ya kumkana au kudogosha mchango wa Mbowe.
..kuhusu masuala ya biashara za Mbowe, Lissu alikuwa akizungumzia kwa muktadha wa biashara kuchangia chama. Je, ni kweli Chadema imekuwa ikiendeshwa kwa kutumia biashara za Mbowe? Bila kujali kama ni kweli au sio kweli nadhani Chadema inapaswa kutafuta namna yenye uwazi zaidi katika kuendesha chama.
..kuhusu Lissu na harakati za Katiba naamini mchango wake utakuwa mkubwa zaidi ikiwa atatumia jukwaa la Chadema kuliko akiwa nje. Pia naamini faida za Lissu kuwa ndani ya Chadema ni kubwa kuliko akiwa nje.
..Kuna jambo limetokea kati ya Mbowe na Lissu. Naamini jambo hilo halina afya kwa Chadema. Ushahidi ni hayo madai kwamba walikwenda kusuluhishwa kwa viongozi wa Dini.
NB:
..Mbowe ametoa mchango mkubwa kuijenga Chadema. Lakini kwa sasa hivi haonekani kuwa na nguvu za kiakili na kimwili kuendelea kuwa Mwenyekiti. Kwa mtizamo wangu amechoka.