Pre GE2025 Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa

Pre GE2025 Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Dogo we unajua uonevu wa ccm?
Yes,
actually Lazima nile, lakini pia lazima nilale vizuri,

ila wananchi ninao waongoza, wanao nipenda sana, wanao niamini mno na kunikubali lazima niwatimizie vipaumbele na mahitaji yao muhimu kwa wakati muafaka, kadiri tulivyokubaliana, tulivyopanga na kuamua kutekeleza pamoja 🐒

sinaga mbambamba na mtu kwenye suala la kazi za maendeleo hata kidogo 🐒
 
Unatia petrol kwenye mafuta kea kutumia lugha ya kukera. Ilichukua watu na.maneno ya aina hii kwa walio wengi kujenga hasira kali iliyosababisha mauaji ya kimbari
ndivyo ukweli ulivyo, ni mchungu sana halafu una kera sana, lakini itakubidi uzoee tu maana hakuna namna nyingine 🐒

hazira, kiburi, ujuaji na mihemko ya kihalifu itadhibitiwa vizuri sana na jeshi letu imara sana la police....

ni muhimu kuchukua tahadhari na kujitenga na magenge yote ya kihalifu yanayojificha nyuma ya siasa, ili kuepuka mkono mrefu wa jeshi la police ambao haukwepeki 🐒

ishara za za kihalifu zitadhibitiwa vizuri sana mapema na majambazi na magenge ya kihalifu yatasambaratishwa mapema tena bila aibu wala huruma...

Ole wako, ewe muhalifu 🐒
 
Kinachotokea ni Sawa na Kuwapa wananchi chanjo ya kupambana na polisi. Ni suala la muda tu kwa wananchi kuanza kupambana na polisi. Itakpotokea polisi watavikimbia vituo na kutupa uniform zao.. Rejea hadithi ya sativa.
hakuna suala la hadithi wala story kwenye kudhibiti uhalifu na ujambazi...

amani kwa wananchi ndio kipaumbele muhimu zaid cha ustawi wa Taifa...

utakabiliwa vikali sana, utadhibitiwa vizuri sana na utachukuliwa hatua za kisheria inavyostahili pamoja na stori na porojo zako sijii ati nini na nini huko 🐒
 
Hizi kazi za kutumwa, tumwa huwa za kijinga sana. Nenda kamata yule, piga huyu, teka wale, weka ndani huyu. Ushamba tu wa madaraka, tumewaweka kufanya maendeleo wao wanadeal na upinzani, ambao haidadii kupunguza umasikini kwenye jamii.
 
'4R' - usanii?
Mtu mwenyewe ni 'illiterate' halafu anatangaza jambo ambalo alipangiwa na wengine, huku yeye mwenyewe hajui inahusu nini!
Ulisha wahi kusikia akiizungumzia kwa umakini stahiki kuelezea 'philosophia hiyo ya 4R?
Alisha toa hotuba ya kufikirisha watu kuhusu hizo 4Rs?
Anachoweza yeye ni kuweka vimaneno vyepesi vyepesi tu na mipasho ya hapa na pale basi!
Ila kweli. Hana uwezo wa kuchambua hata falsafa anayodai ni yake. Yani hakunaga kitu chochote huwa anakielezea in deep
 
Wajomba wanalipwa vibaya sana, ndio wanaongoza kwa njaa, nyumba zao ni huruma, kiufupi wana maslahi na maisha duni sana ila ndio wa kwanza kutumika kisiasa 😂
 
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limewakamata watu wote waliokuwa ofisi za CHADEMA kanda ya Nyasa akiwemo Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu. John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda Joseph Mbilinyi (SUGU) pamoja na viongozi wa BAVICHA.

Pia soma: Jeshi la Polisi lapiga marufuku mkutano wa BAVICHA siku ya vijana duniani

Viongozi hao wamekamatwa mda mfupi baada ya kumaliza kikao cha ndani kwenye ofisi hizo pamoja na viongozi waandamizi wa Bavicha na waandishi wa Habari wa Jambo TV Online waliokuwa wamepiga kambi kwenye ofisi hizo nao wamekamatwa

Lissu aliongea na vyombo vya habari leo ambapo alisema;

1. Kwa vile ofisi ya Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara basi Leo atazigeuza ofisi hizo kuwa darasa ameliita ni darasa la kufundisha juu ya ukombozi ,yaani Teach in Resistance.

Pia soma: Msajili apiga Marufuku Kongamano la CHADEMA mkoani Mbeya, asema matamko yao yanahusisha vitendo vya uvunjifu wa amani

2. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara Mh LISSU amesema atabaki hapo na ikibidi atalala hapo na amesema na yupo tayari kulala hapo na yeye amesema atakuwa Mwl wa kufundisha Hilo darasa la teach in Resistance. Ila kaomba iwepo namna ya kupasha joto mwili kwa sababu hali ya mbeya ni baridi,amewataka watu wakeshe pale.

3. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara basi wataanzia safari Yao kuelekea Ruanda nzovwe kwenye ofisi hizo za Kanda ya Nyasa

4. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zipo mateka amesema wananchi na vijana wasikubali kutishika na Rais Samia, amesema yeye atabaki ofisini hapo kufundisha darasa la teach in Resistance waje wankamatie pale.
View attachment 3067418
Ila safari hii naona mtapata kiki tofauti na awamu Ile
 
Chadema una nguvu sana. Polisi wetu wanasumbuka bure kabisa kwa masalahi ya watu wachache...sometimes polisi nawaonea huruma.
 
Hapo wana wapa kiki tu na umaarufu ili waanze kutrend, kipindi mama amesema maandamano ni ruhusa yalifika wapi? Wameandamana wakaona wananchi wako busy na maisha yao wakaamua kusitisha maandamano.
Sasa imekuwaje tena wakazuiliwa tena siku maalumu ya Kidunia? Hofu ya kuzidiwa.
 
Snapinsta.app_455062202_894287479402263_4982395935248871841_n_1080.jpg

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linadaiwa kuwakamata viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwemo Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara.

Mbali na Lissu, wengine ni Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu.

Viongozi hao wamedaiwa kukamatwa usiku wa leo Jumapili, Agosti 11, 2024 wakiwa ofisi za Chadema Kanda ya Nyasa ikiwa ni saa chache tangu wawasili jijini Mbeya, kushiriki maadhimisho ya siku ya vijana duniani kesho Jumatatu yaliyoandaliwa na vijana wa Chadema (Bavicha).

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema akizungumza na Mwananchi usiku huu, amesema wanaendelea kufuatilia kujua Lissu na wenzake waliokamatwa wamepelekwa wapi.
 
Attachments

  • Snapinsta.app_455062202_894287479402263_4982395935248871841_n_1080.jpg
    Snapinsta.app_455062202_894287479402263_4982395935248871841_n_1080.jpg
    134.8 KB · Views: 1
Kwa Mbeya Mjini Mbunge aliyepo sasa hawezi kushinda Ubunge tena labda Jimbo ligawanywe.
 
Ccm weupe sana ndio maana wanapenda sana watu toka chadema
 
ni muhimu kujiepusha na ukaidi, ni vyema kutii Sheria, makatazo na maonyo ya kiusalama bila shuruti,

vinginevyo,
jeshi la polisi litakabiliana na kiburi na majivuno ya mtu yeyote vizuri tu 🐒
Polisi wetu ni sawa na mgambo tu mbele ya raia siku wakiamua, ratio ya polisi na raia haijakaa vizuri!

Siku raia wakiamua Polisi wanakimbia na kutelekeza magari yenye maji ya kuwasha, mbwa farasi, na land cruiser pickup 🛻.

Wanaweza pia kutelekeza vituo vya Polisi siku nguvu ya umma ikiamua.
 
wataamua lini sasa gentleman?🐒

kuamini ushirikina ni jambo la faragha lakini naona unaliweka wazi kabisaaaa kulikoni 🐒
 
wataamua lini sasa gentleman?🐒

kuamini ushirikina ni jambo la faragha lakini naona unaliweka wazi kabisaaaa kulikoni 🐒
Endeleeni kujiziuka, mnadeal na CHADEMA mnaacha wahamiahaji haramu wanapewa nyazifa za maamuzi ndani ya serikali,Rejea Kauli ya Mkuu wa majeshi mbele bya Samia.
 
Endeleeni kujiziuka, mnadeal na CHADEMA mnaacha wahamiahaji haramu wanapewa nyazifa za maamuzi ndani ya serikali,Rejea Kauli ya Mkuu wa majeshi mbele bya Samia.
Jeshi la police nchini linashughulika na kila aina ya uhalifu na kila ishara au viashiria vya kihalifu popote nchini...

hakuna kuona aibu wala kuona haya kwenye kudeal na kupambana na wahalifu 🐒
 
Back
Top Bottom