Lissu na Lema mwezi Machi na Aprili umeisha, mbona hamrudi nchini?

Lissu na Lema mwezi Machi na Aprili umeisha, mbona hamrudi nchini?

Tafuta fedha mtoa hoja,wewe issue za Mr. Lissu na Mr.Lema zinakuhusu nini?
 
Igweeeeee

Itakumbukwa mwishoni mwa 2021 ndugu Lissu aliyeko huko Belgium na Lema aliyeko huko Canada waliutangazia umma wa watanzania na wafuasi wa CHADEMA kuwa watarudi nchini mwezi March au April kwa kigezo cha kufanya maandalizi

Leo ni May 1st, wananchi na wanachadema tunataka kujua ni nini kimewakuta hawa viongozi wetu mpaka sasa wameshindwa kurejea nchini ili waje kuunganisha nguvu kuipambania katiba mpya na Tanzania kwa ujumla?

NB
ukitukana nakutukana pia
Ndugu Kifurukutu,kwani wamekuambia kama ombi lao maalumu walisha jibiwa(kukukumbisha TU waliomba hakikisho juu ya usalama wao)
 
Pia wanaogopa kuuwawa na Chadema, si mlisikia kauli ya Dk Slaa, Mbowe hataki mtu yeyote amzidi umaarufu
Wewe mwana Sgang unaichukia chadema kiasi ya kuichafua Kwa uongo wako.
 
Bila mbowe chadema ni CHAUMA ....

Wanachama wengi wa chadema wandai haki ya kutoa maoni... Ila ukitoa maoni tofauti na wao... Wanaanza matusi na kukejeli...

Mtu kama Lema hana sababu ya msingi kukimbilia nje ya nchi... Hakuna mtu anashida na lema kiserikali labda kama kakimbia kwa sabbu zake binafs..

Lissu nae ni janja janja tu.... Ni mpenda fursa.. Ndio maana mpka leo bado yupo huko wakati mtesi wake hayupo duniani tena..

Umoja part ije tu.. Ichukue chama kikuu ya upinzani na wakikaza wanaweza kuchukua nchi japo itaiyajika mda wa kujipanga zaidi kwa maana CCM wananchi wengi hatuitaki. .
Lema mpaka anamaliza ubunge alikuwa amelipa crdb milioni 250 kati ya mill 600 alizokopa. Tuseme hata marupurupu yake yalipoingizwa tu kwenye akaunti yakamezwa na crdb. Kwake ilikuwa bora ajitundike lebo ya ukimbizi kuliko kuishi TZ. Asingetoboa.
 
Ndugu Kifurukutu,kwani wamekuambia kama ombi lao maalumu walisha jibiwa(kukukumbisha TU waliomba hakikisho juu ya usalama wao)
wao ni akina nani hasa?
awamu ya sita imejaa amani tele, kwa kigezo kipi na usalama upi wanaoutaka?
 
Igweeeeee

Itakumbukwa mwishoni mwa 2021 ndugu Lissu aliyeko huko Belgium na Lema aliyeko huko Canada waliutangazia umma wa watanzania na wafuasi wa CHADEMA kuwa watarudi nchini mwezi March au April kwa kigezo cha kufanya maandalizi

Leo ni May 1st, wananchi na wanachadema tunataka kujua ni nini kimewakuta hawa viongozi wetu mpaka sasa wameshindwa kurejea nchini ili waje kuunganisha nguvu kuipambania katiba mpya na Tanzania kwa ujumla?

NB
ukitukana nakutukana pia

Hawa ni binadamu wamehama na familia Watoto wapo shule, inawezekana wana kazi, biashara …. Sasa huwezi kuondoka ti bila mpangilia hasa ukizingatia ni watu binafsi ambao hawategemei mshahara.
 
LEMA UNATAKIWA KUNAWA MIKONO YAKO KWANZA

GOBLESS LEMA, Mbunge wa zamani wa Arusha, amekosoa Uongozi wa Prof. Hoseah kama Rais wa TLS.

Amelaumu juu ya ukimya, na kujaribu kusimulia habari za kusadikika kwamba eti, TLS inatakiwa kupigia kelele uonevu, rushwa, ukandamizaji, na mambo mengine.

Huyu jamaa ni MNAFIKI wa kiwango cha juu sana.

Kuna msemo wa kizungu unasema Charity begins at home. Yaani Hisani/Utu wema huanzia nyumbani mwako.

Pia kuna msemo wa kizungu kwa jamii ya Wanasheria, usemao He who comes to an Equity must come with clean hands. Yaani "Mtu anayekwenda kudai Haki ni lazima awe na mikono misafi."

Kwamba, huwezi kuwa na Haki ya usafi wa kudai Haki kwa Mahakama dhidi ya Mtu ambaye hukumtendea haki ulipotakiwa kutenda haki. Unapoteza 'Moral authority.'

Hii haiongozi taratibu za kudai haki mahakamani tu, hata kwa jamiii. Umma ndiyo Mahakama Kubwa zaidi.

Biblia inasisitiza Luka 6:41
"Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?"

Mtazame Lema alivyochafuka;

1. Lema ni M/Kiti wa Programu ya CHADEMA maarufu kwa jina la JOIN THE CHAIN iliyolenga kukusanya mapato ya chama kupitia hamasa ya Michango kwa Wanachama, Wafuasi, Wadau, Wahisani na Wapenzi wa chama hicho.

Hadi sasa zoezi hilo limedorora kutokana na "Upigaji" na Ukosefu wa UWAZI juu ya maendeleo ya makusanyo hayo ili Watu wote wajue zimekusanywa jumla kiasi gani, na inapungua kiasi gani katika malengo yaliyowekwa ya kukusanya jumla ya Sh.1bilioni kwa mwezi.

Ndani ya Kamati yao maalumu ya JOIN THE CHAIN tayari mtafaruku umetokea, Lema anatuhumiwa kutwanga pesa hizo kwa mambo yake binafsi, ndiyo maana hadi leo anashindwa kutoa data za kiasi halisi zilizopatikana.

Unasemaje unapiga kelele dhidi ya Uonezi, Rushwa, na madhambi mengine kwa jamii, huku unaiba pesa za Wanajamii wanaokipenda chama na kujitolea kuchangia?

2. Lema alihusika kuhamasisha Makusanyo ya pesa kwaajili ya Kuwalipa na kuwahudumia Mawakili waliounda jopo la Utetezi kwaajili ya Freeman Mbowe na wenzake. Kesi ya Ugaidi.

Kupitia Program maalumu iliyopewa 'hashtag' ya "GO FUND ME" ambayo kwa asilimia kubwa ilisimamiwa na "Tanzania Diaspora" (Watanzania waishio nje ya nchi).

Hadi kufikia tarehe 01.02.2022 kwa mujibu wa Mtandao maalumu ulioanzishwa kwa malengo hayo, Jumla ya USD13,813 ambazo ni Takribani TSh. 30Milioni zilikusanywa hadi tarehe hiyo.

Pesa hiyo haikuwafikia Mawakili wote waliohusika kwenye kesi hiyo tangu mwanzo hadi mwisho.

Wakili kiongozi waliyeongoza jopo hilo aligawana na wachache aliowapenda yeye.

[emoji1607] Malalamiko ya baadhi ya Mawakili walionyimwa pesa hizo yalifikishwa kwa Viongozi mbalimbali, GODLESS LEMA ni mmojawapo.

Lema kama alivyofanya Askofu Mwamakula, hajawahi kuchukua hatua yoyote kuwatetea Mawakili hao walionyimwa malipo halali ambayo walistahili kutokana na Michango ya Wasamaria waliojitolea kuwafanya Mawakili wote waendelee na majukumu yao kwenye kesi ya Mbowe angalau kwa amani na uhakika wa angalau "Nauli/Mafuta, Chakula, na pesa ya Kujikimu" kwa miezi yote ya kesi husika.

Hao ni Mawakili ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa ni Wanachama wa CHADEMA ambao Lema ni Kiongozi wao, lakini ameshindwa kuwasemea.

Je, hiyo ndiyo Haki unayopigania kwa jamii na umma wa Tanzania?

Kama huna uwezo wa kuwasemea watu Wachache ndani ya nyumba yako (CHADEMA) mawakili wasiozidi 15, huo ujasiri na usafi wa Kujifanya unawasemea Watanzania wote milioni 60 unaupata wapi?

Biblia inaongeza; Luka 6:42
"...utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako." (Msisitizo umeongezwa 'bold').

Lema anatoa "Lecture" bandia kwa Mawakili, eti wanapaswa kubadilisha Uongozi...huku wakitafakari juu ya nchi.

Ni vyema Lema akumbushwe, Kunawa kwanza Mikono yake kabla hajaja kwa umma wa Mawakili na Watanzania, kujaribu kuisemea HAKI.

Jamii ya Mawakili ni jamii ya Wasomi ambayo mtu mwenye elimu ya chini ana "Degree moja na Nusu" (LL + PGDLP), hawahitaji "lecturer Kanjanja" kama Lema, ili kumpata Rais wao.

Tengeneza kwanza mambo ya nyumbani mwako, watendeeni haki watu wa kwenu, watendee haki watu waliokichangia chama michango yao; ili upate kibali cha usafi kwa umma. UNAFIKI hautakusaidia!

Au umeamua kutumia msemo wa Nyani haoni kundule, unajifanya huoni maovu yako?

Ugali uliobebwa kwenye sahani chafu yenye kinyesi hauliki, hata kama mboga imeungwa sana.

BADILIKA!
 
Ukweli haufichwi.ukijaribu kuuficha ipo siku utajidhihirisha.Lissu na Lema hawakwenda huko nje kwa insecurity reasons ni geresha tu..
 
Igweeeeee

Itakumbukwa mwishoni mwa 2021 ndugu Lissu aliyeko huko Belgium na Lema aliyeko huko Canada waliutangazia umma wa watanzania na wafuasi wa CHADEMA kuwa watarudi nchini mwezi March au April kwa kigezo cha kufanya maandalizi

Leo ni May 1st, wananchi na wanachadema tunataka kujua ni nini kimewakuta hawa viongozi wetu mpaka sasa wameshindwa kurejea nchini ili waje kuunganisha nguvu kuipambania katiba mpya na Tanzania kwa ujumla?

NB
ukitukana nakutukana pia
Unawadai?
 
Back
Top Bottom