Ngamanya Kitangalala
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 501
- 1,214
Binafsi nimepata wasaa wa kumsikiliza mheshimiwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, kuna baadhi ya kauli na shutuma zake kwa mawazo yangu nadhani sio sahihi sana
Ukisoma sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343,pamoja na mabadiliko yake ya mwaka 2015 ( The National Election Act,Chapter 343, Revised Edition, 2015) kwenye kifungu cha 124A, kuhusu maadili ya uchaguzi (The election code of conduct)
Sheria hiyo, inataka kila chama kitakachoshiriki uchaguzi mkuu wa October 2020, kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, ambapo kwa Chadema kilisaini makubaliano hayo tarehe 27/05/2020 kupitia katibu mkuu wake
Katika kanuni hizo ( Maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ya mwaka, 2020), kwenye sehemu ya pili, kifungu cha 2, kinaongelea maadili ya vyama vya siasa na wagombea katika kuendesha shughuli za siasa wakati wa kampeni
Ukiendelea kwenye kifungo hicho 2.2 ( h), kanuni inaelekeza wazi kabisa kuwa, kukosoana kati ya vyama na wagombea kunapofanyika, inabidi kujikita katika sera, programu na kazi zao walizofanya, ukosoaji wa vyama vingine au wagombea wengine kwa tuhuma zisizothibitishwa ni lazima uepukwe
Lakini mara kadhaa, mheshimiwa mgombea wa CHADEMA, amekuwa akitoa tuhuma kwa mgombea wa chama kingine, bila hata ya kuwa na uthibitisho wa tuhuma hizo
Binafsi kama mzalendo, napenda kutoa wito kwa wagombea wote kufanya kampeni kwa kutumia lugha ya staha huku wakijikita zaidi kwenye kueleza ilani ya vyama vyao kwa wananchi
Ngamanya Kitangalala Mwaswala
kngamanya@yahoo.com