Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,075
- 11,682
Sidhani kama ni mahasimu wa kisiasa. Wanatofautiana katika approach lakini lengo lao bado ni moja. Lakini hawako karibu na si marafiki.Mpaka sasa nikiyaangalia mahusiano ya Lissu na Mbowe napata utata kama ni washirika wa kisiasa ama ni mahasimu.
Inasemekana alianza kukosa imani na Mbowe akiwa kama mkimbizi. Palikuwa na presha kubwa kutoka kwa baadhi ya wanaotaka mageuzi ili agombee uchaguzi dhidi yake. Mipango ya kumrithi Mbowe ilikomaa wakati Mbowe yuko rumande. Sidhani kama Lissu alipanga kugombea uenyekiti muhula huu kwa namna ilivyotokea. Nahisi aliamini presha kutoka kwa wapambe wake zingemfanya Mbowe aamue kutogombea na hivyo kumpa yeye nafasi ya kugombea. Lissu mwenyewe anadai alisukumwa na tendo la Mbowe kumtangaza Wenje kuwa mgombea mwenza na hivyo kwenda kinyume na kile alichoamini kuwa asingewekewa mshindani na Mbowe katika nafasi hiyo. Akaamua kuachana na Umakamu na kupambana na aliyemtuma Wenje.Lissu mara kadhaa alikuwa anasema cheo chochote atakachogombea Mbowe yeye hatogombea... Ilikuwaje mwaka 2025 akachuana na Mbowe kwenye nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa?
Wengi tu waliamini hivyo.Mbowe mwaka 2023 alisema hatogombea tena nafasi ya uenyekiti Taifa ndani ya CHADEMA. Wengi wetu tukaamini ni zamu ya Lissu kushika hatamu ya uongozi ndani ya CHADEMA.
Kilichomsukuma Mbowe ni siasa chafu zilizofanya kumshinikiza asigombee nafasi hiyo. Asinge gombea ingeleta imani kuwa amefanya hivyo kwa shinikizo na sio utashi wake. Angalau sasa ametoka kwenye Uenyekiti kwa kushindwa uchaguzi na sio kwa kumuogopa mtu au kufukuzwa kwa matusi na kejeli.Ilikuwaje tena Mbowe akatengua kauli yake ya kutogombea aliyoitoa mwaka 2023 na kuamua kugombea uenyekiti na aliyekuwa makamu wake wakati huo?
Kwa sehemu kubwa ya muda huo walishirikiana vizuri tu.Lissu anasema kwa zaidi ya miaka 20 amekuwa anafanya siasa pamoja na Mbowe. Jee kwa miaka yote hiyo walikuwa washirika ama mahasimu?
Ilianza kampeni chafu ya matusi na kejeli dhidi ya Mbowe kumtaka asigombee ili Lissu awe Mwenyekiti. Alipoamua kugombea, kampeni hizo ziliendelea. Upande wa Mbowe wakajitokeza watu nao walioamua nao kuelekeza shutuma dhidi ya Lissu. Tofauti kati yao ni kuwa Mbowe alizikemea na aliwakataza hadharani watu wanaofanya mchezo huo. Lissu hajawahi kukemea wala kuwakataza wanaofanya huo mchezo. Na mpaka leo kampeni hizo chafu dhidi ya Mbowe zinaendelea na uongozi wa Chadema wanazinyamazia. Kunyamaza kwao kunaweza kutafsiriwa kuwa wana ziunga mkono.Wote wawili ilipofika kwenye kugombea uenyekiti walichukua njia moja ya kushutumiana lakini walipishana kwenye kutafsiri kama hali hiyo ilikuwa ni demokraisa au lah. Kilitokea nini?
Wenje alikuwa karibu na Lissu maana wote walikuwa uhamishano. Wenje anadai kuwa Lissu alianza kumchimba Mbowe katika kikundi chao wakati ule. K.m. alidai kuwa Mbowe ametumia pesa za Chadema kujinunulia mashangingi. Kundi hilo lilikuwa na Lissu, Lema, Wenje na Msigwa. Wenje alipoteza imani na Lissu alipothibitishiwa na Mbowe kuwa alinunua magari yale katika mnada wa mali za shirika moja la kitaifa. Wenje akaachana na Lissu akahamia kwa Mbowe.Lissu alikuwa na John Heche na Mbowe akaja na Ezekia Wenje. Jee kabla ya ule uchaguzi Wenje na Heche mitizamo yao kuhusu Lissu na Mbowe ilikuwa inatofautiana ama ni mambo ya uchaguzi tu yaliwafanya watofautiane?
Nadhani Heche hakuwa na tatizo na Mbowe na mpaka leo hana tatizo nae. Tukumbuke kuwa Heche nae alikuwa Mwenyekiti wa Bavicha kama alivyokuwa Mbowe. Na Heche amekaa jela ( sio rumande) na Mbowe.
Heche aliposhindwa kwenye uchaguzi wa jimbo na Esther Matiko, bado Mbowe alimuingiza katika Kamati Kuu. Imani ya Mbowe kwa Heche ilikuwa kubwa kiasi cha kumfanya mjumbe wa Chadema katika mazungumzo ya kuelekea kwenye maridhiano na CCM.
Heche hajawahi kumsema vibaya Mbowe kama ambavyo anawasema wengine waliotofautiana nae kimtazamo. Nadhani Heche aliamini kwa dhati kuwa chama kinahitaji nguvu mpya ambayo ni aggressive zaidi ndio maana aliungana na Lissu. Hakuwa na personal animus dhidi ya Mbowe. Hilo liliwekwa wazi kwa namna ambavyo Heche alivyokuwa anawasiliana na kumpa heshima Mbowe kwenye msiba wa Mkwe wake Mbowe na mmoja wa waasisi wa Chadema. Ilikuwa tofauti kabisa na jinsi wapambe walivyotaka tuamini.
Hivyo hivyo sidhani kama Mbowe ana personal animus dhidi ya Heche kama alivyokuwa nayo dhidi ya Lissu.
Amandla...