Ninaelewa baadhi ya mambo mengi uliyoandika hapo kwenye gazeti hilo la nipashe.
Ila kwa kifupi, Mungu ndio anapanga nani awe kiongozi, dua lako la kuku halitompata mwewe. Pili, kelele za chura hazimnyimitembo kunywa maji.
Mungu anapanga lakini ukumbuke kuwa Duniani kuna roho ya nuru na roho ya giza .
Hizi zote zina nguvu kama ilivyo kwa usiku na mchana. Yote ni masaa 12.
Aina ya utawala unaoishi kwa ufahari na maslahi makubwa na kila aina ya mamlaka mkubwa kwa kodi za watu wote lakini unabagua watu huwezi kuuita utawala wa Mungu.
Yesu hakukosea aliposema tuombe siku zote kuwa Ufalme wa Mungu uje?
Alijua kuna ufalme wa Giza au shetana ambao upo hivyo tuombe wa Mungu uje.
Suala sio Dua la kuku mana kwa Tanzania ukishabikia mauaji ujue sio muda mrefu yaterejea kwenye familia yako.
Unajua Msigwa na JPM ni MTU na mkwe wake!!
Unajuaje kama Mimi na wewe watoto wetu hawataoana au wajukuu zetu?
Ndio maana tunapinga taifa la watu wanaojengeana chuki za kuuana kwa sababu ya vyama visivyo na roho wala nafsi.
Kwani CCM ikifa kihalali au chadema watu si watabaki hai? Lakini mkianza kuwamaliza watu ili CCM ibaki itabaki na nani?
Hamuoni jinsi taifa lilivyopooza kwa ushindi wa 84%+ ?
Huoni ni bora mngeshinda kwa 51% ya hapali na furaha ingekua kubwa sana na kila mtu angempania mwenzake awamu ijayo na watu wangeishi kwa raha na upendo.?
Unategemea nini Siku Simba ishinde yanga kwa Goli kumi na mbili za kubebwa na refa wazi wazi ?
Huoni ni bora Ingeshinda Goli moja la halali na kwa haki kuliko kumi na mbili ya dhulma? Huwezi kukubali ukweli wa asili mpaka asili itakapokuhukumu mana Damu hua inalipwa kwa damu. Hakuna mbadala wa Damu ya MTU inapomwagwa ardhini. Ni kanuni ya asili.