Lissu: Naishi kwenye makazi ya balozi(Ujerumani) kwa sababu maisha yangu hayako salama, nitarejea Ubelgiji

Lissu: Naishi kwenye makazi ya balozi(Ujerumani) kwa sababu maisha yangu hayako salama, nitarejea Ubelgiji

Hivi watu wengi humu akili mbovu tu siyo? Mnatetea udhalimu siyo tu aliofanyiwa, bali anaoendelea kufanyiwa Lissu, na sisi watanzania tulioporwa haki yetu ya kuchagua viongozi tunaowataka? Bure kabisa nyote humu mnaounga mkono ushetani unaoendelea! Au ni sheitwani, au MATAGA wachumia tumbo! Mtu wa kawaida hawezi kuwa upande wa hawa manyang'au wanaoendelea kuitesa na kuifilisi nchi hii!
Naomba ujibu maswali yangu hayo kisha nitakujibu ya kwako.

Nyie wafuasi wa Lisu, naomba mjiulize hivi, kwann Lisu asipewe uraia na uongozi kwenye hizo nchi zote za ulaya anazokimbilia huku akiipaka mavi Tanzania?

Kama hao wazungu wanampenda saana na wanamkubali kwann hawampi uongozi kuwaongoza raia wao huko kwenye nchi zao?!! Badala yake wanampa pesa ya kurubuni baadhi ya watanzania kutokua na uzalendo na nchi yao.

Naomba mnijibu tafadhali
 
Tundu Lissu akihojiwa na redio Ujerumani DW anasema amepata simu za kutishiwa amani na ameamua kujificha kwenye makazi ya Balozi wa Ujerumani

Anasema maisha yake yako hatarini na anajipanga kuondoka na kurudi Ubeligiji

Tundu ni mwanasheria na very treak man tujihadhari naye sana

=========

LISSU: Niko katika makazi ya balozi wa Ujerumani, Dar es Salaam tangu siku ya Jumatatu.

MWANDISHI: Kulikoni?
LISSU: Naishi kwenye makazi ya balozi kwa sababu maisha yangu hayako salama tangu siku ya Jumamosi iliyopita, napata ujumbe wa kunitishia maisha kwa hiyo niliondoka nyumbani kwangu siku ya Jumapili na siku ya Jumatatu nikaenda ubalozini, nikafatwa na askari polisi wa Tanzania wakiwa kwenye magari mawili, nikakamatwa nikapelekwa kituo cha polisi Central na isingekuwa uwepo wa maafisa wa kibalozi wa Ujerumani siku hiyo pengine nisingerudi nyumbani kwangu.

MWANDISHI(LILIAN MTONO): Unasema kwamba ulianza kupata vitisho siku ya Jumamosi kabla hujahamia kwenye makazi ya balozi, ni vitisho vya aina gani ulivipata na nani hasa alikuwa anakutisha?
LISSU: Siku ya Jumamosi nilipigiwa simu na mtu ambae hakujitambulisha akaniambia kwamba, mheshimiwa maagizo tuliyopewa ni kumalizana na wewe, once and for all na baadae kidogo nikaletewa simu nyingine na mtu mwingine aliniambia hivyo hivyo kwamba mheshimiwa oda ya kukumaliza imetolewa kwa hiyo kama unaweza kujiokoa jiokoe.

MWANDISHI: Kwa hiyo hawa waliokupa taarifa ni wale waliotumwa ama labda ni wasamaria wema?
TUNDU LISSU: Nafikiri kwa jinsi walivyojitambulisha ni wako katika hilo kundi la watu waliotumwa lakini hawakubaliani na mambo haya.

MWANDISHI: Utakuwa hapo hadi lini?
TUNDU LISSU: Nitakuwa hapa mpaka hapo usalama wangu utakapohakikishwa, sipendi kukaa hapa, mimi ni mtu mwenye shughuli nyingi kwa hiyo nataka niondoke hapa haraka iwezekanavyo na bahati mbaya siwezi nikajua itakuwa lini kwa sababu wale wanaopaswa kuhakikisha usalama wangu wanaonekana kama hawataki kujicommit kwamba kama nikitoka nje nitakuwa salama.

MWANDISHI: Kwanini unasema hivyo?
LISSU: Kwa sababu tangu nimekuwa hapa kumekuwa na jitihada za mabalozi wa nchi mbalimbali kuiambia serikali ya Tanzania kwamba haya mambo yanatokea sio masuala sahihi na mpaka sasahivi hizo jitihada hazijafanikiwa bado.

MWANDISHI: Utakapofanikiwa kuondoka, utabakia nchini au utarudi Ubelgiji?
LISSU: Nitaondoka kurudi Ubelgiji kwasababu hali ya usalama sasa hivi sio nzuri hata kidogo, hivi vitisho ni vitu ambavyo lazima nivichukulie kwa uzito mkubwa na wa kipekee.

MWANDISHI: Bado unajiona utasimama tena kwenye kinyang'anyiro kijacho cha Urais na utaendelea na harakati zako za kisiasa?
LISSU: Tuombe Mungu atupe uzima tujue miaka inayokuja itatuweka vipi lakini nachoweza kusema waziwazi ni kwamba harakati ni maisha yangu.

Hopefully, ulimaanisha "....Tundu Lissu is very trick man, tujihadhari naye sana...."

Na siyo "...Tundu is very treak man.."

Back to the topic..

Tundu Lissu is not a trick man as you think hence trying to convince us think that way...

Ni tishio la kweli. Na bila kuchukua tahadhari na kujihami kisawasawa, Magufuli hawezi kumuacha salama huyu ndugu, atamuua na hakika lazima atamuua...!!!

Zile nyundo na spana za wakati wa kampeni, hakikuwa za kawaida. Zilikuwa nzito sana hata kumfanya Jiwe na wenzake kulala bila viatu..

Akiwa hapa nchini, trust me, watamuua..!!

Kila la kheri Tundu Lissu. Fanyia siasa zako nje ya Tanzania. Tutakusikia na tutakuelewa tu...!
 
Hivi watu wengi humu akili mbovu tu siyo? Mnatetea udhalimu siyo tu aliofanyiwa, bali anaoendelea kufanyiwa Lissu, na sisi watanzania tulioporwa haki yetu ya kuchagua viongozi tunaowataka? Bure kabisa nyote humu mnaounga mkono ushetani unaoendelea! Au ni sheitwani, au MATAGA wachumia tumbo! Mtu wa kawaida hawezi kuwa upande wa hawa manyang'au wanaoendelea kuitesa na kuifilisi nchi hii!n
Mwenye akili mbovu ni yule mwanasheria anayetangaza na kuhamasisha maandamano yasiyo na kikomo huku akijua fika katiba ya nchi hairuhusu kupinga matokeo ya uchaguzi wa raisi.

Mwambieni afuate taratibu na sheria za nchi bila kujichafulia taaluma yake.
 
Naomba ujibu maswali yangu hayo kisha nitakujibu ya kwako.

Nyie wafuasi wa Lisu, naomba mjiulize hivi, kwann Lisu asipewe uraia na uongozi kwenye hizo nchi zote za ulaya anazokimbilia huku akiipaka mavi Tanzania?
Kama hao wazungu wanampenda saana na wanamkubali kwann hawampi uongozi kuwaongoza raia wao huko kwenye nchi zao?!! Badala yake wanampa pesa ya kurubuni baadhi ya watanzania kutokua na uzalendo na nchi yao.
Naomba mnijibu tafadhali

Be honest dude.

Tanzania inapakwa "mavi" na viongozi wako hawa hawa mnaowa "cherish", kina Magufuli na wenzake.

Huwezi kujinyea na kujipaka mavi mwenyewe kwa sababu ya ulevi wa kupenda madaraka halafu unaanza kulaumu watu wengine..

Tundu Lissu is always speaking the truth!

Nyie na viongini wenu msiopenda watu wa ndani ya nchi hii na wa mataifa mengine kujua ukweli juu ya watawala wa Tanzania walivyo wezi, mafisadi, wauaji na waongo mnaona ni KUPAKWA MAVI...!!

Kama unabisha, toa mfano wa jambo moja alilosema ama kutenda Tundu Lissu linaloipaka mavi Tanzania, nami nitakuamini na kushawishika na wewe.
 
Ili iwe fundushisho kwa wavurugaji wote wa nyakati za sasa na zijao, moja: wahakikishe nchini hachomoki, mbili: anashitakiwa na kutiwa hatiani, na tatu: hukumu atakayopata iwe ni ya kifungo cha jela tena cha muda mrefu miaka 30.

This is your worst wish ever. Haitatokea milele.

He's alive physically and spiritually.

Wataanza kufungwa na kufa kwanza hao hao kina Magufuli na wenzake mnaowaabudu.
 
Be honest dude..

Tanzania inapakwa "mavi" na viongozi wako hawa hawa mnaowa "cherish", kina Magufuli na wenzake...

Huwezi kujinyea na kujipaka mavi mwenyewe kwa sababu ya ulevi wa kupenda madaraka halafu unaanza kulaumu watu wengine..

Tundu Lissu is always speaking the truth...!

Nyie na viongini wenu msiopenda watu wa ndani ya nchi hii na wa mataifa mengine kujua ukweli juu ya watawala wa Tanzania walivyo wezi, mafisadi, wauaji na waongo mnaona ni KUPAKWA MAVI...!!

Kama unabisha, toa mfano wa jambo moja alilosema ama kutenda Tundu Lissu linaloipaka mavi Tanzania, nami nitakuamini na kushawishika na wewe...
Mfano, Lisu kutetea migodi ya madini iendelee kusimamiwa na wale wamiliki, huku mchanga wa makinikia ukipelekwa nchini mwao.
 
Ametafuta justification ya kuhalalisha kuishi Brussels. Nani ahangaike na Lissu wakati huu ambapo hana madhara. Labda ndani ya CHADEMA huenda anatishia uenyekiti wa mtu ambapo ni sawa na uhaini.
Hulka ya pekee ya madikteta ni woga, hakuna dikteta asiye muoga. Please refer history. Madikteta wanafika wanaogopa hata familia zao.
 
Be honest dude..

Tanzania inapakwa "mavi" na viongozi wako hawa hawa mnaowa "cherish", kina Magufuli na wenzake...

Huwezi kujinyea na kujipaka mavi mwenyewe kwa sababu ya ulevi wa kupenda madaraka halafu unaanza kulaumu watu wengine..

Tundu Lissu is always speaking the truth...!

Nyie na viongini wenu msiopenda watu wa ndani ya nchi hii na wa mataifa mengine kujua ukweli juu ya watawala wa Tanzania walivyo wezi, mafisadi, wauaji na waongo mnaona ni KUPAKWA MAVI...!!

Kama unabisha, toa mfano wa jambo moja alilosema ama kutenda Tundu Lissu linaloipaka mavi Tanzania, nami nitakuamini na kushawishika na wewe...
Kwa maneno mengine Lisu anasema Magufuli anafukuza wafadhili migodini.

Kwaniongeza Lisu alipokua hizo nchi za ulaya alikua akipita akiwaambia wadau wanaotoa misaada ya elimu wasipeleke tena Tanzania. Sababu Magufuli anazuia watt waliopata mimba za utotoni kurudi mashuleni.
 
Karungikana na the Palm Tree naomba mnijibu haya maswali ninayowauliza kama mimi ninavyowajibu maswali yenu.

Naomba mjiulize hivi, kwann Lisu asipewe uraia na uongozi kwenye hizo nchi zote za ulaya anazokimbilia huku akiipaka mavi Tanzania??
Kama hao wazungu wanampenda saana na wanamkubali kwann hawampi uongozi kuwaongoza raia wao huko kwenye nchi zao?!! Badala yake wanampa pesa ya kurubuni baadhi ya watanzania kutokua na uzalendo na nchi yao.
Naomba mnijibu tafadhali
 
Hahahah! Kawadanganye bavicha. Rudi tu kwenu hamna atakae kumiss. Tumekukataa kwenye sanduku la kura ila pia tumekukataa barabarani so hamna anaekuhitaji, ondoka acha visingizio.
 
Ibilisi bado anainyemelea damu ya Lissu !! Hapa ndipo tulipofikia watanzania... Siasa za uadui..siasa za vita!!

Lawama hizi zote ni kwa CCM, majonzi haya yote ya watanzania ni kwa CCM.
 
Be honest dude..

Tanzania inapakwa "mavi" na viongozi wako hawa hawa mnaowa "cherish", kina Magufuli na wenzake...

Huwezi kujinyea na kujipaka mavi mwenyewe kwa sababu ya ulevi wa kupenda madaraka halafu unaanza kulaumu watu wengine..

Tundu Lissu is always speaking the truth...!

Nyie na viongini wenu msiopenda watu wa ndani ya nchi hii na wa mataifa mengine kujua ukweli juu ya watawala wa Tanzania walivyo wezi, mafisadi, wauaji na waongo mnaona ni KUPAKWA MAVI...!!

Kama unabisha, toa mfano wa jambo moja alilosema ama kutenda Tundu Lissu linaloipaka mavi Tanzania, nami nitakuamini na kushawishika na wewe...
Sikatai kila nchi ina mapungufu yake, lakini huwezi sikia kiongozi wao wa kisiasa ameenda nchi nyingine hadharani kusema mapungufu ya nchi yake.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Be honest dude.

Tanzania inapakwa "mavi" na viongozi wako hawa hawa mnaowa "cherish", kina Magufuli na wenzake.

Huwezi kujinyea na kujipaka mavi mwenyewe kwa sababu ya ulevi wa kupenda madaraka halafu unaanza kulaumu watu wengine.

Tundu Lissu is always speaking the truth.

Nyie na viongini wenu msiopenda watu wa ndani ya nchi hii na wa mataifa mengine kujua ukweli juu ya watawala wa Tanzania walivyo wezi, mafisadi, wauaji na waongo mnaona ni KUPAKWA MAVI..

Kama unabisha, toa mfano wa jambo moja alilosema ama kutenda Tundu Lissu linaloipaka mavi Tanzania, nami nitakuamini na kushawishika na wewe.
Ni pale Lissu aliposema watu wote wanaomtumainia Mungu kwenye kupambana na corona ni idiots
 
Sikatai kila nchi ina mapungufu yake, lakini huwezi sikia kiongozi wao wa kisiasa ameenda nchi nyingine hadharani kusema mapungufu ya nchi yake.

..ukimuona mwanasiasa anazungumza mapungufu ya serikali yake nje ya nchi ujue kwamba hana uhuru wa kufanya hivyo akiwa ndani ya nchi.

..utawala huu umewanyima wananchi uhuru wa kuikosoa serikali yao na watendaji wake. matokeo yake ndiyo hayo, watu wanakwenda kuzungumzia nje ya nchi.

..wakati wa utawala wa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kulikuwa na uhuru fulani wa kuzungumza na kukosoa. Na kipindi hicho hatukumshuhudia Tundu Lissu akiikosoa serikali akiwa nje ya Tanzania. Hali hiyo imebadilika miaka ya karibuni wakosoaji wanaumizwa, wanasumbuliwa, wanatishwa, na ndio maana wengine wanasema-sema huko nje.
 
Sawa, hata kama serikali ya sasa hivi haitoi uhuru huo uliosema, je ni busara kwenda kusemea nchi za nje kuhusu mapungufu ya nchi yako??

Unategemea hao wazungu watamsaidia Lissu kutatua hayo mapungufu ya serikali ya Tanzania bila malipo yoyote??
 
Sawa, hata kama serikali ya sasa hivi haitoi uhuru huo uliosema, je ni busara kwenda kusemea nchi za nje kuhusu mapungufu ya nchi yako ??
Unategemea hao wazungu watamsaidia Lisu kutatua hayo mapungufu ya serikali ya Tanzania bila malipo yoyote??

..Kama hakuna usalama wa kuzungumza ndani ya nchi, basi busara ni kuzungumza nje ya nchi.

..Matatizo ya nchi yanatatuliwa kwa njia na watu wengi, ikiwemo wa ndani na nje.

..Nategemea wazungu watasaidia kutatua mapungufu ya serikali ya Tanzania bila malipo, kama sisi Watanzania tulivyosaidia nchi za Kusini mwa Afrika bila malipo.

..Wazungu pia walisaidia ukombozi wa Kusini mwa Afrika bila malipo. Misaada ya kibinadamu[humanitarian] na mashinikizo ya kidiplomasia kutoka nchi za Ulaya yalikuwa na msaada mkubwa ktk harakati za ukombozi kusini mwa Afrika.
 
Wakati anafanya kampeni maisha yake hayakua hatarini?
Huyu jamaa hovyo sana. Ni afadhali watz tumemkataa...apeleke ripoti kwa waliomtuma kuwa hatutaki ujinga
 
Back
Top Bottom