..uliniuliza kama Wazungu wamewahi kusaidia nchi za Kiafrika kutatua matatizo ya ndani.
..Jibu langu ni kwamba zipo nchi za Ulaya zilitoa misaada ya kibinadamu kwa vyama vya ukombozi vya kusini mwa Afrika.
..Zipo nchi za Ulaya na Marekani, hao unaowaita Wazungu, ambazo ziliweka mashinikizo ya kidiplomasia kama sehemu ya harakati za ukombozi wa Afrika.
..Pia siyo kweli kwamba ili nchi moja iisaidie nchi nyingine ni lazima nchi hiyo iwe imemaliza matatizo yote ya wananchi wake. Tulipokuwa tukisaidia harakati za ukombozi, je tulikuwa hatuna changamoto mbalimbali nchini kwetu?
..Mwisho, Wazungu wanaonyonya rasilimali za Afrika hufanya hivyo kwa kushirikiana na viongozi Madikteta na Mafisadi wa Kiafrika. Katika nchi ambayo kuna demokrasia, kuna uwazi, na utawala bora, Wazungu hawawezi kuingia na kuiba kama inavyofanyika ktk nchi zinazoongozwa na Madikteta waliowafunga midomo wananchi wao.