Ametafuta justification ya kuhalalisha kuishi Brussels. Nani ahangaike na Lissu wakati huu ambapo hana madhara. Labda ndani ya CHADEMA huenda anatishia uenyekiti wa mtu ambapo ni sawa na uhaini.
Kwa sasa Lisu ni adui mkubwa zaidi wa CCM kuliko wakati wowote.
Kwanza Hawakutegemea kuwa watanzania wanampenda Lisu kuliko mtu yeyote katika Dunia hii.
Pili kwa Sasa Lisu ni mpinzani mkubwa sana wa Waroho wa URAIS 2020.
WALE wote ndani ya CCM wanaotegemea kugombea Urais ndani ya CCM na nje ya CCM hawana namna yoyote ya kupenya kwa kura halali mbele ya Lisu. Hata yule anayetegemewa kupewa Urais wa maisha hawezi kuupata Lisu akiwa Hai.
Hivyo suala la kumlinda Lisu ni la watanzania wote wapenda haki na utu. Uongozi wa nchi huu umegeuka kuwa ni wa kutumia ukatili na kila aina ya udhalimu kuupata. CCM wana hofu kubwa kuliko wakati wowote.
Kwa hiyo tusimdanganye Lisu kuwa usalama wake upo chini ya utawala wa CCM wakati hakuna kiongozi yeyote wa CCM aliyewahi kutamka kuwa Wapinzani sio maadui. Bahati mbaya kabisa hata mkuu wa nchi alisema wazi wakati wa kampeni kuwa atakasirika sana wakimchagua hata diwani wa Upinzani na hata wapa maendeleo.
Sasa kama wananchi kwa malaki wataadhibiwa kwa kumchagua mpinzani itakuaje kwa huyo kiongozi wa upinzani anayeonekana kama MTU jeuri asiyemuogopa mtu yeyote kwenye siasa.
Siasa za Tanzania tangu awamu hii siasa zimekua ni uadui mkubwa sana hata kuwaza kuuana badala ya kupingana kwa hoja.
Kama huyu anasema maendeleo ni ya vitu na huyu anasema maendeleo ni ya watu ,sasa hapo mnauana ili nini !? Hata shetani anawashangaa watu wanaowindana ili kuuana wakijifanya ni uzalendo kumbe wanahofisa nafasi zao za madaraka yanayowapa mapesa na mali.