Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mgombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema ni kweli ana tiketi ya ndege ya kuondoka nchini kwenda Ubelgiji Desemba 18, 2020.
Amesema hayo kumjibu mgombea wa urais kupitia CCM, Dkt. John Magufuli ambaye alisema ana taarifa kuna baadhi ya wagombea wana tiketi za ndege ili wakimbie wakisababisha fujo nchini.
Lissu amesema ataenda kutokana na matatizo ya kiafya aliyoyapata baada ya kupigwa risasi mwaka 2017. Ambapo daktari wake amemuambia Desemba 20 arudi Ubelgiji ili aangalie maendeleo yake.
Amewaambia Wananchi wa Lindi kuwa, kwanza alipigwa kwa amri ya Rais na kama kukimbia angekimbia alipopigwa risasi hawezi kukimbia wakati huu.