Wanabodi,
Hili la kuamua ni Magufuli, limenistua kidogo kwa sababu kwa sisi tuliomfuatilia utendaji kazi wa Magufuli kwa kauli na matendo tangu akiwa waziri, japo kiukweli ni mchapa kazi, yaani ni jembe kazi la ukweli, lakini mtu huyu ameonyesha wazi sio mzuri sana in terms of stability in decision making!, amefanya baadhi ya maamuzi mengi tuu kwa jazba, pupa, papara na kukurupuka kwa mtindo wa nimeamua mimi na liwalo liwe!, mwisho wa siku baadhi ya maamuzi yake ambayo mengine ni very rational yanakuja kutu cost sisi kama taifa, mifano ipo, ikiwemo kuvunjwa ile Petro Station Mwanza, Uuzaji wa nyumba za serikali, Samaki wa Magufuli, just to mention but few, hivyo akipita na kuwa rais wa nchi hii, kama huu ndio mfumo wake wa kufikia maamizi, then you can just imagine, akiwa rais, atafanya maamuzi mangapi ambayo yatatucost kama taifa, ila pia kwa hulka yake, ana chance ya kuja kuwa the worst dictator this nation has ever had!. Tuombe Mungu asaidie, hili likitimia, huyu mtu abadilike, na kuwa a benevolent one, labda karma ije kuingilia kati, vinginevyo...!.