Je akijibu kuwa suala hilo aulizwe muislamu mwenzao aliyepita yeye halimuhusu kwani siku zote damu ni nzito kuliko maji...iweje leo mmumkomalie yeye wakati aliyelianzisha yupo?
Kwa vile Magufuli ni Rais wa wote nafikiri ni muhimu kumwomba atumie mamlaka aliyopewa atowe msamaha kwa hao mahabusu kama vile anavyotoa misamaha kwa wafungwa wengine au afuate nyayo za Mwalimu Nyerere alivyokuwa anatoa misamaha kwa wafungwa wa kisiasa kama Mzee Mapalala, Chief Fundikira, Kaselabantu, Ziota Humbi, Chris Kasanga Tumbo wote hao ni kutoka Tabora, na akina Seif Sharif Hamadi, Abdullahman Mohhamed Babu, Sheikh Muhhamad Nasor Abdullah, Chief Hussein M Makwaia na mdogo wake bila kuwasahau .....
" The detainees at Liwangula started questioning their detention for cattle raiding when those Maasai were not detained for stealing cattle and killing many people. They argued that Prime Minister Edward Moringe Sokoine, who had ordered their detention, was favouring members of his own ethnic group, the Maasai. They wrote to President Nyerere, who finally released them"
Kwa hiyo ukiangalia jambo hili kwa undani kabisa sio geni na linaongeleka pale palipo na nia ya dhati kabisa kumaliza uhasama unaotaka kujengeka bila sababu ya maana