Uchaguzi 2020 Lissu: Nikichaguliwa, ndani ya siku 100 za kwanza masheikh wa Uamsho wataachiwa huru

Akizipata pia ni sawa tu. Waislamu wanaojielewa akina Ponda wamepiga kelele sana. Lissu anaongelea sheria na haki. Sheria ya Tanzania haina sehemu ambayo inaruhusu mtu kuwa kizuizini kwa miaka 6 bila kupelekwa mahakamani. Lissu ni mtu haki. Atamtetea hata Magufuli akiona haki zake zinakiukwa. Kama haujamuelewa Lissu mpakaa leo basi utakwenda tu kaburini bila ya kumwelewa.
Ila anavyowataja Waislamu kama specific group linaloonewa hapo hayuko sawa naona kama kuna Udini ndani yake, anataka kura za huruma kutoka Dini hiyo
 
kwa nini kila uchaguzi wanasiasa wanatumia Mashek wa uamsho kama kete ya kutaka kura? kama hao mashee wana haki kwa nini hawapewi lkn ktk kila kipindi cha uchaguzi utasikiaa wagombea wana watumia kama kete....halafu uchaguzi ukiisha hakuna atakaye wazungumzia!! Lowasa aliiahidi hivyo hivyo ktk uchaguzi wa mwaka 2015 Lisu naye tena mwaka huu 2020...kuna jambo la kutafakari
Kwani lissu ni lowassa?
Je una uhakika gani lissu hatowazungumzia hata baada ya uchaguzi? Ni Yeye keshasema atawatoa hao mashehe mahabusu over!! Kama huamini tarehe 28 mpigie kura halafu uone.
 
Kwanza jielimishe uzijue tofauti kati ya "Kifungo" na "Mahabusu" , hapo utazijua status za hao wanazuoni wa dini kuwa wamefungwa ama wako mahabusu..

Asante.
Kwanza jifunze kunukuu vizuri hapa JF.

Kwa nini unafikiri nahitaji kujifunza tofauti ya kifungo na mahabusu?

Kifungo ni nini na mahabusu ni nini? Mahabusu ina ukomo gani? What is the letter and spirit of the law?

Nimesoma ripoti ya Jaji Nyalali kuhusu sheria 40 kandamizi, unaijua? Umeisoma?

Unajua indefinite detention ni nini na madhara yake?
 
Nadhani hujanielewa mimi nataka hao watoke na wengine sitaki hii itumike kama yale ya babu Seya. Hawa walifungwa toka wakati wa Kikwete na Kikwete ana mkono katika hili, huwezi kuwafunga watu bila kesi na hizi sheria zao za baadhi ya kesi kukosa dhamana mimi nataka aseme makosa yote yatakuwa na dhamana ili kuruhusu haki itendeke. Naunga mkono hilo na wengine wengi wanaosota ndani bila kesi, Haki ni msingi wa kila kitu.
Kwa nini unadhani sijakuelewa?

Kwani Tundu Lissu kasema watoke hao tuu, wengine wasitoke?
 
kwa nini kila uchaguzi wanasiasa wanatumia Mashek wa uamsho kama kete ya kutaka kura? kama hao mashee wana haki kwa nini hawapewi lkn ktk kila kipindi cha uchaguzi utasikiaa wagombea wana watumia kama kete....halafu uchaguzi ukiisha hakuna atakaye wazungumzia!! Lowasa aliiahidi hivyo hivyo ktk uchaguzi wa mwaka 2015 Lisu naye tena mwaka huu 2020...kuna jambo la kutafakari
Kwani umesahau kama miaka mitano midomo yetu ilitiwa zipu

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza jifunze kunukuu vizuri hapa JF.

Kwa nini unafikiri nahitaji kujifunza tofauti ya kifungo na mahabusu?

Kifungo ni nini na mahabusu ni nini? Mahabusu ina ukomo gani? What is the letter and spirit of the law?

Nimesoma ripoti ya Jaji Nyalali kuhusu sheria 40 kandamizi, unaijua? Umeisoma?

Unajua indefinite detention ni nini na madhara yake?

Very good Mkuu, so kama unajua kuwa hao wapo mahabusu na kuwa bado hawajahukumiwa na kufungwa, then ingefaa ukaongelea 'madhara' ya kuwaweka mahabusu kwa muda mrefu kabla ya kesi yao kumalizika.

Bottom line - Masheikh wapo Mahabusu, bado hawajahukumiwa kufungwa..!!
 
kwa nini kila uchaguzi wanasiasa wanatumia Mashek wa uamsho kama kete ya kutaka kura? kama hao mashee wana haki kwa nini hawapewi lkn ktk kila kipindi cha uchaguzi utasikiaa wagombea wana watumia kama kete....halafu uchaguzi ukiisha hakuna atakaye wazungumzia!! Lowasa aliiahidi hivyo hivyo ktk uchaguzi wa mwaka 2015 Lisu naye tena mwaka huu 2020...kuna jambo la kutafakari
Waulize waliowashikilia kwanini wanaendelea kuwashikilia nakutoa mwanya kwawapinzani kilainapo fika uchaguzi wanawatumia kama mtaji wawa funge au wawaachie kwajambo hili linaumiza sana
 
View attachment 1602807

Mgombea urais Tundu Lissu ameendelea kusisitiza na kumtaka Rais Magufuli awaachie mara moja mashekhe wa Uamsho na mahabusu wengine waliofungwa kwa hila.

Tundu Lissu ameahidi ndani ya siku 100 za kwanza atakapo ingia madarakani ataawachia mashekhe wa Uamsho kwani kesi yao haina msingi wowote.

Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru.

Tundu Lissu ameshangaa iweje mashekhe hao wasipelekwe mahakamani kama kweli wana kesi ya kujibu ili mahakama iweze kuamua kama wamevunja sheria ama lah.
Sawa kabisa.
 
Very good Mkuu, so kama unajua kuwa hao wapo mahabusu na kuwa bado hawajahukumiwa na kufungwa, then ingefaa ukaongelea 'madhara' ya kuwaweka mahabusu kwa muda mrefu kabla ya kesi yao kumalizika.

Bottom line - Masheikh wapo Mahabusu, bado hawajahukumiwa kufungwa..!!
Suala lipo mahakamani,Lissu anakuwa na kiwewe cha kutaka kick ili iweje??
 
View attachment 1602807

Mgombea urais Tundu Lissu ameendelea kusisitiza na kumtaka Rais Magufuli awaachie mara moja mashekhe wa Uamsho na mahabusu wengine waliofungwa kwa hila.

Tundu Lissu ameahidi ndani ya siku 100 za kwanza atakapo ingia madarakani ataawachia mashekhe wa Uamsho kwani kesi yao haina msingi wowote.

Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru.

Tundu Lissu ameshangaa iweje mashekhe hao wasipelekwe mahakamani kama kweli wana kesi ya kujibu ili mahakama iweze kuamua kama wamevunja sheria ama lah.
Haujui ughaidi huyo anasema tu.
 
kwa nini kila uchaguzi wanasiasa wanatumia Mashek wa uamsho kama kete ya kutaka kura? kama hao mashee wana haki kwa nini hawapewi lkn ktk kila kipindi cha uchaguzi utasikiaa wagombea wana watumia kama kete....halafu uchaguzi ukiisha hakuna atakaye wazungumzia!! Lowasa aliiahidi hivyo hivyo ktk uchaguzi wa mwaka 2015 Lisu naye tena mwaka huu 2020...kuna jambo la kutafakari
Lowasa alishinda?
 
View attachment 1602807

Mgombea urais Tundu Lissu ameendelea kusisitiza na kumtaka Rais Magufuli awaachie mara moja mashekhe wa Uamsho na mahabusu wengine waliofungwa kwa hila.

Tundu Lissu ameahidi ndani ya siku 100 za kwanza atakapo ingia madarakani ataawachia mashekhe wa Uamsho kwani kesi yao haina msingi wowote.

Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru.

Tundu Lissu ameshangaa iweje mashekhe hao wasipelekwe mahakamani kama kweli wana kesi ya kujibu ili mahakama iweze kuamua kama wamevunja sheria ama lah.
Huku ni kutaka kuungwa mkono na mafungu mbalimbali ya Watanzania, hata kama ni mafungu ya waharifu. Kwa nini mashehe tu ndiyo waachiliwe na si wafungwa wengine? Lissu anamaanisha kwamba hao mashehe wanashikiliwa kwa ajili ya Uislamu wao na hivyo anataka apate sapoti ya Waislamu. Ikumbukwe kwamba hao mashehe walishikwa wakati wa utawala wa Kikwete ambaye ni Muislamu.

Kama lingekuwa suala la dini, Kikwete asingewaweka ndani Waislamu wenzake. Aidha, mbona leo hii bado kuna mashehe wa Kiislamu wengi tu mitaani wanakwenda misikitini bila kificho na hamna yo yote anayewabugudhi? Iweje hao wachache tu ndio wachukuliwe kama nia ni 'kuthibiti' Uislamu jinsi Lissu anavyoashiria? Kuna vikundi kama ISIS, Boko Haram, Al-Shabaab, n.k. vinavyotumia jina la Uislam ambapo kiukweli wana ajenda zao zaidi ya dini na ndiyo maana hata nchi za Kiislamu kama Syria, Iraq, Algeria, n.k. wanapigana navyo.

Sasa Lissu anasema atawaachilia hao mashehe bila kudadisi kilichowafanya washikwe. Kama mwanasheria, ningedhani Lissu angependekeza kwenda kuwatetea mahakamani na muafaka ufikiwe kadiri mahakama itakavyoamua. Siyo kuwaachia tu eti kwa kuwa ni mashehe. Suala la hao mashehe JPM alilikuta alipoingia Ikulu. Hana tatizo na Uislamu. Ndiyo maana alidiriki hata kuchangisha fedha za kujengea msikiti. Lissu asitafute kiki kwenye vikundi ambavyo wala havistahili. Analeta uchonganishi wa dini mahali ambapo hakuna tatizo hilo.
 
Back
Top Bottom