Uchaguzi 2020 Lissu: Nikichaguliwa, ndani ya siku 100 za kwanza masheikh wa Uamsho wataachiwa huru

Uchaguzi 2020 Lissu: Nikichaguliwa, ndani ya siku 100 za kwanza masheikh wa Uamsho wataachiwa huru

Tangu wamekamatwa mambo ya uamsho yakakoma kabisa Zanzibar. Badala ya Lisu asifu hali mbaya ilivyofanikiwa kudhibitiwa yeye anaona walionewa. Hebu chukulia mfano ile hali isingedhibiwa huko Zanzibar unafikiri leo hii Lisu angesemaje. Lisu anaeleweka na genge tu la wahuni wafuata upepo basi.

MAGUFULI4LIFE.
 
Unadhibiti kwa kupoka haki za watu??
 
Kama kweli wana makosa basi wapelekwe mahakamani na ushahidi usiotia shaka kama bado hawajakamilisha uchunguzi ni bora wawaachie.....Magaidi wa ukweli wapo mtwara-mozambiki wakawatawanye kule.
 
lissu huna akili hivi jakaya kawaacha humo ndani na walikamatwa kipindi chake na yeye ni muislamu mwenzao wewe na upuuzi wako hujui hta kuomba kura unafikiri ndiyo njia ya kupatia kura hiyo? honi sasa zanzibar imetulia? wana kesi ya kujibu hao usifikiri watu hawajui wewe pekeyako ndiyo hujui au unajua akini unajitoa akili tu

Kinachotakiwa ni kufuata Sheria sio mambo ya Jah kaya alikuwa muislam mwenzao na blah blah tu za hapa na pale.
 
Mgombea wetu anatetea magaidi? Maana wanatuhumiwa kufanya ugaidi Zanznibar, mwaka huu chama chetu kimechemka sana.
Kama unawaita watuhumiwa

Iweje unawazungumzia kama ni wahalifu
Mtuhumiwa si mhalifu ana haki ya kuwa huru kama raia wengine.
Ana haki ya kujitetea na kutetewa.
 
View attachment 1602807

Mgombea urais Tundu Lissu ameendelea kusisitiza na kumtaka Rais Magufuli awaachie mara moja mashekhe wa Uamsho na mahabusu wengine waliofungwa kwa hila.

Tundu Lissu ameahidi ndani ya siku 100 za kwanza atakapo ingia madarakani ataawachia mashekhe wa Uamsho kwani kesi yao haina msingi wowote.

Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru.

Tundu Lissu ameshangaa iweje mashekhe hao wasipelekwe mahakamani kama kweli wana kesi ya kujibu ili mahakama iweze kuamua kama wamevunja sheria ama lah.
Utakuwa unaingilia uhuru wa Mahakama! Halafu AHADI nyingine ni KUJIPENDEKEZA tu wakati unajua fika kuwa kuna mihili tofauti kwa masuala tofauti. Au ni ushauri wa Bob Amsterdam kuwa useme "the impossible" na uongo kwa nia na lengo la kutafuta umaarufu wa haraka haraka!?
 
Kwa nini unadhani sijakuelewa?

Kwani Tundu Lissu kasema watoke hao tuu, wengine wasitoke?
Mleta mada kasema nini? Lissu kasema siku 100 za mwanzo mashekh wa uamsho kuachiwa, ndio kichwa cha habari au kuna mengine alisema na wengine kama alisema basi hakuna katika uzi huu
 
Utakuwa unaingilia uhuru wa Mahakama! Halafu AHADI nyingine ni KUJIPENDEKEZA tu wakati unajua fika kuwa kuna mihili tofauti kwa masuala tofauti. Au ni ushauri wa Bob Amsterdam kuwa useme "the impossible" na uongo kwa nia na lengo la kutafuta umaarufu wa haraka haraka!?
uhuru wa mahakama ipi?uliwahi kuwaona mahakamani hao mashekhe?hata hujui unaandika nini. Hivi unajua kama hilo jambo bado lipo kwenye mhimili wa Executive?ambao mkuu wake ni rais?
 
Mleta mada kasema nini? Lissu kasema siku 100 za mwanzo mashekh wa uamsho kuachiwa, ndio kichwa cha habari au kuna mengine alisema na wengine kama alisema basi hakuna katika uzi huu
Nimekuuliza hili swali hujalijibu.

Sijui hujaliona. Sijui umeliona umeliogopa.

Narudia tena.

Kwani Tundu Lissu kasema watoke hao tuu, wengine wasitoke?
 
"Nikishinda... na kule Bara nna uhakika atashinda Lissu... atanrudishia watu wangu" Maalim Seif. Hao Masheikh hakuna mtu ndani ya sisiemu anawazungumzia!
Hivi wakishinda kisha wasipowakuta huko watafanya nini? Naomba watujibie hilo.
 
Nimekuuliza hili swali hujalijibu.

Sijui hujaliona. Sijui umeliona umeliogopa.

Narudia tena.

Kwani Tundu Lissu kasema watoke hao tuu, wengine wasitoke?
Kasema specific mashekh wa uamsho na wengine sasa nauliza hao wengine kina nani na anawajuaje hao wengine huko tunaelekea kulekule kwa kina Babu Seya. hii ni kutafuta points tu ila kama asingetaja kikundi chochote na kuongelea kiujumla system yote ya watu kukamatwa bila kufungulia kesi halafu ndio angechambua ni kina nani na nani.
 
uhuru wa mahakama ipi?uliwahi kuwaona mahakamani hao mashekhe?hata hujui unaandika nini. Hivi unajua kama hilo jambo bado lipo kwenye mhimili wa Executive?ambao mkuu wake ni rais?
Unless umeingia Dar juzi, hao masheikh wamekuwa wakifika Kisutu mara nyingi tu tena chini ya ulinzi mkali. Kama liko kwenye Executive, Mahakamani walikuwa wakipelekwa kufanya nini? Kusalimia?
 
Maana mashekh amekuwa specific ila kusema na hao wengine, wengine kina nani?
Nikuulize wewe unayeleta hoja ya wengine.

Wengine kina nani?

Tundu Lissu mara nyingi sana kiujumla amekemea serikali kutofuata utawala wa sheria.

Na amesema akipata nafasi kuwa rais atasimamia utawala wa sheria.

Msingi mkubwa wa utawala wa sheria ni haki sawa kwa wote.

Ila, katika uandishi wa habari, katika historia, katika siasa, katika ualimu, katika falsafa, katika hotuba, mambo yanasemwa kwa specificity, kwa mifano.

Kesi ya masheikh hawa ni mfano wa kesi maarufu.

Tundu Lissu anaitumia kama mfano wa jinsi utawala wake utakavyosimamia utawala wa sheria.

Ningemuona Tundu Lissu ni mjinga kama angetaja kesi isiyojulikana na watu wengi kama mfano, wakati kuna kesi inayojulikana na watu wengi.

Huu ni mfano mmoja unaoelezea msimamo wa Tundu Lissu kuhusu utawala wa sheria unaoheshimu the spirit and letter of the law.

Kwa nini unataka kufanya kama Tundu Lissu kakataza utawala wa sheria na haki kwa watu wengine wote isipokuwa hawa mashehe, wakati hajasema hilo?
 
Back
Top Bottom