Uchaguzi 2020 Lissu: Nikichaguliwa, ndani ya siku 100 za kwanza masheikh wa Uamsho wataachiwa huru

Hivi hii hoja Magufuli aliwahi kuijibu popote?
Waliwekwa ndani tangu awamu ya 4 ipo madarakani nadhani kuanzia 2012 (Kama nimekosea nirekebishwe) na kuhamishiwa huku bara.

Kuna kipindi mahakama ya Zanzibar iliamuru warejeshwe huko wakajibu mashitaka (Kuna Uzi kuhusu hilo uliletwa humu) ila sikufatilia kujua kama walirejeshwa huko.

Anyway ni vyema upelelezi ukamilishwe (kama bado) ili kesi yao isikilizwe na kutolewa hukumu maana wamesota mahabusu muda mrefu sana.
 
8years upelelezi gani huu?? Mental na Spiritual torture, wakitoka huko wameharibiwa kisaikolojia wawe na hatia wasiwe na hatia.

Walipaswa wahukumiwe au waachwe huru.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Safi sana. Wanaonewa sana kama wana makosa iweje 6yrs hawajakutwa na hatia?
 
Lissu anawasha moto msitu wenye nyasi kavu kimasihara...ataujua mtiti wake.
 
Jakaya kawaacha humo ndani na walikamatwa kipindi chake na yeye ni muislamu mwenzao wewe na upuuzi wako hujui hta kuomba kura unafikiri ndiyo njia ya kupatia kura hiyo? honi sasa zanzibar imetulia? wana kesi ya kujibu hao usifikiri watu hawajui wewe pekeyako ndiyo hujui au unajua akini unajitoa akili tu
 
Hivi hii hoja Magufuli aliwahi kuijibu popote?

Je akijibu kuwa suala hilo aulizwe muislamu mwenzao aliyepita yeye halimuhusu kwani siku zote damu ni nzito kuliko maji...iweje leo mmumkomalie yeye wakati aliyelianzisha yupo?

Kwa vile Magufuli ni Rais wa wote nafikiri ni muhimu kumwomba atumie mamlaka aliyopewa atowe msamaha kwa hao mahabusu kama vile anavyotoa misamaha kwa wafungwa wengine au afuate nyayo za Mwalimu Nyerere alivyokuwa anatoa misamaha kwa wafungwa wa kisiasa kama Mzee Mapalala, Chief Fundikira, Kaselabantu, Ziota Humbi, Chris Kasanga Tumbo wote hao ni kutoka Tabora, na akina Seif Sharif Hamadi, Abdullahman Mohhamed Babu, Sheikh Muhhamad Nasor Abdullah, Chief Hussein M Makwaia na mdogo wake bila kuwasahau .....

" The detainees at Liwangula started questioning their detention for cattle raiding when those Maasai were not detained for stealing cattle and killing many people. They argued that Prime Minister Edward Moringe Sokoine, who had ordered their detention, was favouring members of his own ethnic group, the Maasai. They wrote to President Nyerere, who finally released them"

Kwa hiyo ukiangalia jambo hili kwa undani kabisa sio geni na linaongeleka pale palipo na nia ya dhati kabisa kumaliza uhasama unaotaka kujengeka bila sababu ya maana
 
Unaji contradict.

Kama wamefungwa bila kufikishwa mahakqmqni, na wewe ni muumini wa sheria na watu kupelekwa mahakamani kabla ya kufungwa jela, basi walivyofungwa sasa bila kufikishwa mahakqmqni si sawa, na Tundu Lissu kubatilisha kifungo hicho ni sawa.

Tundu Lissu hajakataza mashehe kushitakiwa mahakamani, amekataa mashehe kufungwa bila kufikishwa mahakamani.
 
mkuu hilo ndilo la muhimu kuliko huyo anayekuja nasera ya kuombea kura bila kuangalia uzito wa kitu
 
Lissu kabla ya kushambuliwa alikua anazungumza ndani ya bunge
Anyway watu wanashangaa kulikoni CCM hawasemi chochote?
Na sisi waislamu Ndio mtaji wa CCM!!
Sio wakiristo wengi watakaopigia kura CCM
Tatizo letu waislamu wengi ni wanafiki..... That's All,,,,,,,,,,, ***!!
 
Nadhani hujanielewa mimi nataka hao watoke na wengine sitaki hii itumike kama yale ya babu Seya. Hawa walifungwa toka wakati wa Kikwete na Kikwete ana mkono katika hili, huwezi kuwafunga watu bila kesi na hizi sheria zao za baadhi ya kesi kukosa dhamana mimi nataka aseme makosa yote yatakuwa na dhamana ili kuruhusu haki itendeke. Naunga mkono hilo na wengine wengi wanaosota ndani bila kesi, Haki ni msingi wa kila kitu.
 
Kwani Lowassa alishinda uchaguzi? Hoja yako haina msingi
 
Mgombea wetu anatetea magaidi? Maana wanatuhumiwa kufanya ugaidi Zanznibar, mwaka huu chama chetu kimechemka sana.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…