Uchaguzi 2020 Lissu: Nikichaguliwa, ndani ya siku 100 za kwanza masheikh wa Uamsho wataachiwa huru

Unless umeingia Dar juzi, hao masheikh wamekuwa wakifika Kisutu mara nyingi tu tena chini ya ulinzi mkali. Kama liko kwenye Executive, Mahakamani walikuwa wakipelekwa kufanya nini? Kusalimia?
DPP kaambiwa na mahakama ama akamilishe uchunguzi ndani ya mwezi mmoja, ama aahirishe mashtaka na watuhumiwa waachiwe mpaka DPP atakapokuwa tayari.

Hiyo ilikuwa September 14 2019.

Mahakama imesemanhivyo September 14 2019.

Hata mahakama inaona hoja anayoisema Tundu Lissu.

Kwa sababu sasa hivi watuhumiwa wanapigwa danadana huku wako ndani miaka nenda rudi kwa style ya "uchunguzi unaendelea".

 
"Tundu Lissu ameahidi ndani ya siku 100 za kwanza atakapo ingia madarakani ataawachia mashekhe wa Uamsho kwani kesi yao haina msingi wowote.

Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru". hayo ni maneno ya Lissu sasa kama sikutafuta kura ni nini? ndio anataka haki lakini pia anatumia kesi hii kupata kura, hilo wala halihitaji akili. anataka kura za waislamu wenye uchungu na mashekh
 
Unless umeingia Dar juzi, hao masheikh wamekuwa wakifika Kisutu mara nyingi tu tena chini ya ulinzi mkali. Kama liko kwenye Executive, Mahakamani walikuwa wakipelekwa kufanya nini? Kusalimia?
Mpaka September 14 2019, na mpaka sasa nafikiri, kesi yao inasubiri uchunguzi wa DPP. DPP ni executive.

Mahakamani wanapelekwa, kesi inatajwa, DPP anasema warudishwe lupango uchunguzi unaendelea.

They do not get their day in court.

Hii ni mbinu inayotumika sana utawala huu pale serikali inapoona haina kesi ya maana lakini inataka kufungia watu tu.

Mtu kafungwa miaka 6 tayari, uchunguzi unaendelea.

Ukija kumuachia mwaka wa saba, ukisema uchunguzi umeonesha hana hatia, tayari ushamfunga jela miaka saba.

Utamlipa kwa hiyo miaka saba uliyomfunga bila hatia?

Hata ukimlipa hela, kitu ambacho hakifanyiki Tanzania, miaka yake saba hairudi tena.
 
Kwani mwanasiasa kutafuta kura imekatazwa?

Unategemea mwanasiasa asitafute kura? Nini maana ya kampeni?

Kama anataka kusimamia haki na ili asimamie haki anahitaji kura, kutafuta kura ili asimamie haki kuna tatizo gani?
 
Muislam safi mpenda haki LAZMA AMPE LISSU KURA, ma-Shehe ni sawa na Ma-padri au wachungaj, hivi kweli Mapadri 50 wangewezwa kuwekwa ndani muda wote huo? tuamke
 
siasa bana
 
Ukiwa kichaa kabisa kabisa, unaweza kumpigia kura Ndugu.
Ukiwa na akili timamu unaweza kumpigia kura Dkt. JPM.
Hao waliwekwa jela bila kufikishwa mahakamani unalizungumziaje hilo wewe mwenye akili zako timamu?
 
Kwahiyo kama walikamatwa awamu ya kikwete ndio iwe guarantee ya awamu ya jiwe kuendelelea kuminya haki zao, wacha undezi we gamba, kwani babu seya na wanawe walikamatwa awamu ipi na wameachiwa awamu gani! Grow up kiddo
 
Ila anavyowataja Waislamu kama specific group linaloonewa hapo hayuko sawa naona kama kuna Udini ndani yake, anataka kura za huruma kutoka Dini hiyo
eeh fita ni fita mura..usimchagulie silaha
 
Gereza la Kisongo kuna Mashekhe 200 wa answari suna
Gereza la Mtwara kuna Mashekhe 400 wa Answari suna
Magereza ya Keko na Ukonga Mashekhe wa Uamsho na wengine wanaopinga Bakwata nao wanaweza humo
 
Hizi sheria kandamizi za kuweka watu ndani kwanza Kisha ndo utafute ushahidi huu ni uhuni, uuaji, unyama. Ambao hata mkoloni akumfanyia mtu mweusi why sisi kwa sisi, ofisi ya DPP inapwaya Sana. Kama ushahidi haujakamilika kwann umweke mtu ndani
 
Gereza la Kisongo kuna Mashekhe 200 wa answari suna
Gereza la Mtwara kuna Mashekhe 400 wa Answari suna
Magereza ya Keko na Ukonga Mashekhe wa Uamsho na wengine wanaopinga Bakwata nao wanaweza humo
Takwimu za kijiwe cha kahawa?
 
Njia zingine za kuomba kura duh ...........
 
Wale masheikh bakwata kazi yao kusifia tu wakipewa vizawadi vidogovidogo tu sababu ya uvivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…