Uchaguzi 2020 Lissu: Nikishindwa kwa haki nitakuwa wa kwanza kujitangaza

Uchaguzi 2020 Lissu: Nikishindwa kwa haki nitakuwa wa kwanza kujitangaza

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mgombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema akishindwa kwa haki atakuwa wa kwanza kusema kuwa ameshindwa kwa haki.

Amesema wakishinda lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikawapora ushindi wao, atawaingiza watu barabarani kuteteta ushindi wao.

Amesema CHADEMA wakishinda ni lazima Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itangaze kwa heri au kwa shari.

Amesisitiza wanataka Uchaguzi wa Amani, lakini hawatakuwa tayari kugeuza shavu la pili ili waumie zaidi. Ameyasema haya alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni Tabora.
 
Magufuli naye atoe tamko,yupo tayari kuachia madaraka?
SALAAM ZA GWAJIMA KUTOKA MWISHO WA RELI.
1. Ulituaidi Chuo Cha Marubani hukutimiza.
2. Uliaidi kujenga Chuo Cha Biblia, hukutimiza.
3. Uliaidi kujenga Hospitali Kata ya Salasala, hukutimiza Hilo.
4. Uliaidi kumfufua Amina Chifupa, Hukutimiza pia.
5. Uliaidi kugeuza Misikiti kuwa Sunday schools, Hujatimiza.
6. Umeshindwa kulipia semitrailer mbili bandalini (90Mil.)
7. Ulituaidi na ukatutaka kuchanga fedha za kuanzisha TV lkn hujatimiza.
8. Ulituaidi na kutuchangisha fedha za kuanzisha Radio, lkn hujatimiza.
9. Ulituuzia viwanja (2015) kule Kiluvya (Mwanakondoo), lkn mpaka Leo hujatupatia.
10. Ulituaidi kuleta ndege 12 za abiria, lkn hujatimiza.
11. Ulituaidi treni ya umeme lkn hujatimiza.
12. Ulituaidi lujenga kanisa lenye uwezo wa Kubeba watu 250,000 kwa ibada moja, lkn hujatimiza na bado tuko chini ya mabati.
13. Leo unatuaidi kwenye kampeni kuwapeleka wananchi wa Kawe Marekani📷📷📷📷, Askofu! Askofu! Askofu! Mungu anakuona ujue.....dhambiya Uongo ni ya shetani mwenyewe kabisa.
14. Aidha, bado tunakumbuka juu ya ile video. Maana mwenendo wako baada ya ile video umebadilika Sana, ijapokuwa bado hatuamini Kama Kuna mahusiano.
Embu tuachie Kawe yetu bana...
 
Tundu Lissu ajiandae na kuingiza watu barabarani
Mama Samia.JPG
 
Hii sio Mara ya kwanza kwa Lisu kutamka hivyo,,tunachotaka sasa aje na kauli ya kumtaka mgombea wa ccm aji commit kukubali matokeo ya kushindwa pindi akishindwa uchaguzi na akabidhi madaraka kwa amani Kama ilivyo desturi ya Watanzania,la sivyo akikaidi awe tayari kulazimishwa kuondoka kwa njia mbalimbali ikiwemo maandamano na aje ku face the quencequences,huwezi msamehe mtu mkaidi
 
Magufuli Rais wa JMT kwa miaka mitano Tena[emoji106][emoji106][emoji106]

Hizi kelele Wala hazina jipya.
 
Mgombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema akishindwa kwa haki atakuwa wa kwanza kusema kuwa ameshindwa kwa haki.

Amesema wakishinda lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikawapora ushindi wao, atawaingiza watu barabarani kuteteta ushindi wao.

Amesema CHADEMA wakishinda ni lazima Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itangaze kwa heri au kwa shari.

Amesisitiza wanataka Uchaguzi wa Amani, lakini hawatakuwa tayari kugeuza shavu la pili ili waumie zaidi. Ameyasema haya alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni Tabora.
Huruhusiwi kujitangaza kwa lolote, iwe ushindi au kushindwa. Fuata sheria.
 
Huyu jamaa hii kauli yake huwa inanichekesha Sana! Eti 'ntaingiza watu barabarani" 🤣🤣🤣 aysee... Ni mtu gani anaeweza kukubali kuingizwa barabarani?
Hata km ni manyumbu ila sizani km watamuelewa.
 
Back
Top Bottom