Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,992
1) Lissu enzi za utawala wa Mkapa, aliwatoa magerezani kule Tarime, watu zaidi ya 400, waliokuwa wamebambikiziwa kesi na serikali ya ccm kwa kushirikiana na makampuni ya "mabeberu" ya kuchimba dhahabu. Wengine hadi kesi za mauaji. Lissu alitoa huduma hii bure bilashi. Ndio maana, kwa kutambua hili, polisi walijaribu sana kumzuia Tundu Lissu asipite maeneo hayo wakati wa kampeni za 2020, japo hawakufaulu. Walijua angepata mapokezi ya kifalme.Sasa hiyo ya kuwa best student katika kitivo chake inalisaidiaje taifa letu tofauti na kufanya uhuni wa siasa huko ughaibuni akishinikiza tukatiwe misaada,Bure kabisa huyu mtu.Na ni very selfish huyu jamaa!!!
Bora hata Mimi na ualimu wangu huu nasaidia taifa langu kwa kuwapa vijana elimu,Mpaka sasa nina vijana zaidi ya laki tano waliopita mikononi mwangu,huyu bwana kafanya lipi kwa watanzania ambalo kwalo twaweza mkumbuka
2) Wakati wa bunge la Spika Anne Makinda, Tundu Lissu, akitumia uwezo wake mkubwa katika mambo ya sheria, alitia mchango mkubwa sana bungeni, ikabidi kiti cha spika mara kwa mara kutafuta ushauri wa kisheria kwa Tundu Lissu, baada ya mwanasheria mkuu wa Serikali wakati huo kuonekana kupwaya sana. Kila mara, nguli mwingine wa sheria, japo ni fisadi mkubwa, Andrew Chenge, kuthibitisha kwamba "Lissu yuko sahihi"
3) Lissu anatoa mchango mkubwa kwa kutoa Darsa katika nyanja za sheria na siasa, kupitia Cyber Lounge kila ijumaa na mahojiano ya one on one with Tundu Lissu, kupitia Pod Cast za NADJ MEDIA.
4) Katika migodi ya Nzega, Tundu Lissu pia alitoa huduma za kisheria bure kwa wachimbaji wadogo. Hilo alithibitisha mh. Bashe, na altoa shukrani rasmi bungeni kwa Tundu Lissu, kwa kuwasaidia wapiga kura wake Bashe.
Kwa hiyo nakushauri usitiwe upofu na chuki binafsi, wivu, mawazo finyu kutokana na kushiba propaganda za maadui wa Lissu