Lissu ninayemfahamu mimi kama wanadhani 'Prima Facie' itamnyenyekeza, wanakosea sana!

Tuendelee tu, mwisho wa siku maji na mafuta vitajitenga, hapa kuna wanao tumia nguvu, na kuna anayetumia elimu na kipawa ambacho Mungu amempa, hawa wengine lengo ni kutumia nguvu ili kuficha maovu yaliyotendeka, huyu mwingine anatumia Elimu na kipawa alichopewa na Mungu ili kuhakikisha hayo maovu yanaanikwa.

Sasa utaratibu wa Mungu hapendi na maovu na anayachukia ikitokea kuna binadamu naye anayachukia hayo basi Mungu huwa upande wa huyo mtu
 
Mimi ni Miongoni mwa wanao lifahamu Hilo

Ni issue tu ya mkate
 
Hiki ulichokiandika kina ukweli kwa 99.99%
Hata baadhi ya wanaccm na wenyewe wanakiri hii kesi imemuongezea Lissu umaarufu, ushawishi na wafuasi mara dufu huku serikali na chama umaarufu na ushawishi wao ukizidi kudidimia! Hii kesi pia inaamsha hisia za muungano! Huku sitaingia kwa undani.

Haya mambo ya vuta nikuvute hayana manufaa yoyote yale kwa serikali na pia chama cha mapinduzi. Ni vile tu wamekosekana watu wenye busara wa kumshauri mwenyekiti pamoja na baadhi ya makada wazoefu mfano Prof. Anna Tibaijuka, Jaji Joseph Sinde Warioba, na wengine wengi kushauri hii kesi iondolewe mahakamani!

Huku mtaani chuki dhidi ya ccm, polisi na Rais aliyeko madatakani inaongezeka kila uchao! Na hakuna anayejali! Zinaanzishwa tume za kutaka kuwaaminisha watu serikali haihusiki na yale machafuko, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo!

Serikali inatakiwa itambue mapema Lissu siyo Mbowe! Kama aliweza kukataa begi lililojaa hela! Alipigwa risasi zaidi ya 30 akanusurika! Badala ya kubakia uhamishoni Ubelgiji, akaamua kurudi nchini kuja kuendeleza mapambano! Alimshinda Mwenyekiti wake wa chama aliyekaa madarakani kwenye chama zaidi ya miaka 20, huku akiwa na ushawishi ndani na nje ya chama! Huyu mtu ni wa kawaida kweli? Akiitisha mikutano ya hadhara, maelfu ya wananchi wanajitokeza kumsikiliza!
 
Hakika umefanya analysis nzuri sana ya kisomi isiyokuwa na chembe ya uchawa ahsanteni sana kwa elimu nzuri kwa wasioelewa namna ya kutafuta haki unayosimama na ukweli👍👍👍
 
Kwamba mpaka sasa serekali imeonyesha ina ushahidi, ama ni mambo ya mahakama za simu moja? Jaji anakuambia mahakama haitazami uzito wa ushahidi, ili mradi washitaki wameonyesh mshatakiwa anatakiwa ajibu🤣🤣

Kwenye hii kesi ndio imedhihirika kuwa wawekazaji wako sahihi kutotumia mahakama zetu kupeleka mashauri yao. Yaani haya maamuzi ya mahakama yanaendana na zile kura 31m alizopata Samia bila kuwa na idadi hiyo ya wapiga kura vituoni.
 
Pascal Mayalla ahsante kwa kupandisha bandiko zuri lenye angalizo wakati sahihi.

Kwa mujibu wa katiba yetu, TL akipatikana na hatia, ampapo kisheria na aina ya mashtaka yake hukumu ni kifo. Ikatokea mtu kutangaza msamaha, itamuondolea sifa za kugombea nafasi ya ukuu wa nch?

kwa sasa nnaona kuna jitihada za kukizamisha chama na kumdhorotesha TL

hii ni miongoni mwa sifa za mgombea

"Hali ya Kisheria na Masharti ya Mahakama: Kikatiba, mgombea hapaswi kuwa amehukumiwa kwa makosa ya jinai yanayohusisha ukosefu wa uaminifu au kukimbia kodi katika kipindi cha miaka mitano kabla ya uchaguzi. Hali yake ya kisheria na matokeo ya mashitaka yoyote yanayomkabili mahakamani yana mchango mkubwa katika kuamua uwezo wake wa kugombea kisheria."
 

Ni kama inavyokua kwenye uchaguzi, anaetangazwa ndio mfalme, sio anaepigiwa kura nyingi.

Hali kadhalika kwenye hili, watalazimisha kufikia malengo yao hata kama yapo kinyume na taratibu za kisheria.

Mwanasheria anaposema hawaangalii uzito wa ushahidi, unabaki kinywa wazi, sasa wametumia vigezo vipi kuhitimisha ana kesi ya kujibu?
 
Hiyo Clip yako nimejiona YouTube tangu juzi, aisee unamjua vizuri TL
 
Hapa kuna mambo mawili labda utuelimishe

Mens rea nia ya kutenda uovu

Na hiyo seditious,
Ni wakati Gani kupinga kitu inakuwa Haki na wakati Gani inakuwa sio Haki ??
 
Mkuu acha kuzunguka wewe ni mboga mboga 😃
 
Huyo akifa itakua vizuri zaidi,huyo na makamu wake,waliosema uchaguzi hautofanyika,tutakinukisha na kweli pakatokea vurugu,hao hawatakiwi kuuona mwanga wa jua na chama chao kifutwe


Yeah well talking strong behind keyboard while you aint shit and ww binafsi hamna kitu unaweza fanya
🤣
Type of mind yinazo dhani kutumia nguvu is the only solution
 
Wanaotumia nguvu wanataka wanyenyekewe but bad news lissu aint that type
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…