Lissu ninayemfahamu mimi kama wanadhani 'Prima Facie' itamnyenyekeza, wanakosea sana!

Lissu ninayemfahamu mimi kama wanadhani 'Prima Facie' itamnyenyekeza, wanakosea sana!

Well said...
Ila mtawala zile taarabu zake za "who are you?" Zilikua zinaonesha kabisa namna amejipanga na athari za so called "cold war" na ni kama tayari Alisha settle njia yake ya kutokea!!
Nachokiona, ni kama "tawala" Inacheza mchezo wa trial and error then terminate or repair..

Nachokiona hakuna clear roadmap ambayo ipo kwa sababu Tanzania haina hulka ya kufungamana na international block yoyote hivyo, ni kama mwanamke asiye na ndoa kamili lakini ana wanaume wawili anaocheza nao kwa muda na style tofauti ili aweze kulinda maslahi yake kwa pande zote mbili.

Lakini wakati huu ni tofauti. Oct 29 imeipa Tanzania disadvantage kwenye global politics haswa kwenye mahusiano yetu na western block ambayo ni face of democracy, so kinachotokea ni sawa upunguze mazoea na mpenzi unaefaidika nae zaidi na kwenda kuonesha mahaba yako zaidi kwa hasimu wake ili umpunguze makali ilhali wewe ndiye uliyemkosea kwa hiyo, hayo makali huna

Kwa hiyo hapo ni option mbili, urudi kwa wa siku zote kwa kukubali masharti yaks au uende extra miles kumridhisha mmoja kati yao ili akupe salio la kukutosheleza kusavaivu.

Japo options zaweza kuwa nyingi zaidi..

Ila leo nimejiachia sana, mkuu Pascal Mayalla Mayalla
Kama wakipitia thread waambie sina jambo mimi ni kijana mnyonge. Sina impact zaidi ya ukibodi waria🙏🏽😁
 
Nchi imetia aibu sana kwenye nyanja za kisheria, majaji aibu yao.

Sasa tunataka katiba ili hizo nafasi zishindaniwe ili tupate haki na siyo kutoa hukumu inayompendeza aliyekuteuwa.

Aibu naona mimi na Tanganyika yanguuuu, mshahara usio na kodi kwa majaji unasababisha wawe biasnes kwenye maamuzi.
 
MAWAZO YA UWANDISHI WAKO BADO NI MGANDO - Huwezi kuandika hoja nzito kama hii bila kupangilia hoja zako kwa mantiki ya msingi kama msomi mzuri - Unakuwa kama hujataka kuandika andiko kama msomi huru nadhani ujitafakari mwandishi kwa hilo maana upo very poor kabisa katika andiko lako unakuwa kama sio msomi au mtu umeenda shule kabisa .....
 
Kesi inapaswa kufutwa haraka sana maana mashahidi walijikanyaga na hata wanafunzi wetu watakuwa wanafundishwa kwa rejeo ya kesi yenye makosa. Tujajenga kizazi kibaya mno huko tuendako.
 
MAWAZO YA UWANDISHI WAKO BADO NI MGANDO - Huwezi kuandika hoja nzito kama hii bila kupangilia hoja zako kwa mantiki ya msingi kama msomi mzuri - Unakuwa kama hujataka kuandika andiko kama msomi huru nadhani ujitafakari mwandishi kwa hilo maana upo very poor kabisa katika andiko lako unakuwa kama sio msomi au mtu umeenda shule kabisa .....
Nini maana ya Neno kukinukisha kwenye kamusi
 
Baada ya verdict.....Tundu Lissu ndie mwanasiasa maarufu number 1 Tanzania , kumbe ndio tunamuongezea umaarufu, huku nchi yetu ikizidi kubagazwa na kuchafuliwa kimataifa, kwa viongozi wetu kufanya maamuzi bila kutumia kanuni ya The Law of Unintended Consequences, ukajikuta badala ya kujenga ndio unaharibu zaidi!.

.... but to expose how rot our justice system is before the eyes of international community.

Kama lengo la hii prima facie, is to make TL to bow down kwa kuogopa kuhukumiwa kifo kwa kosa la uhaini, hivyo baada ya kukutwa na prima facie, atakutwa na hatia, na atahukumiwa kifo kwa kunyongwa mpaka afe!, lakini baada ya hukumu kutoka, atatokea a saviour fulani, atamsamehe TL kwa msamaha wa rais, hivyo TL atarejea uraiani kichwa chini na hawezi tena kugombea wadhifa wowote!, then they are doing a terrible mistake!, the law of unintended consequences will take charge, hili jambo linakwenda kututesa kama nchi kuliko linavyochukuliwa sasa!.
Tawire!
 
Wanabodi

Utangulizi Kuhusu Mashuhuri na Maarufu
Mtu mashuhuri nambari moja, kwenye nchi yoyote ni mkuu wa nchi, rais, ila kunaweza kuwa na mtu mwingine ambaye sio mashuhuri, na akawa ni maarufu kuliko mkuu wa nchi!. Kwenye Uzinduzi wa TASAF II Uwanja wa Jamhuri Dodoma, mgeni rasmi ni Rais JK,, rais alipokuwa anaingia, tukatangaziwa na MC, wote tusimame kumpokea mgeni rasmi, Jukwaa Kuu wakasimama wote, majukwaa mengine hawana time!.

Wakati JK ameusha kaa, watu wa protocal, hawaruhusu tena mtu mwingine yoyote kuingia ndani kupitia geti kuu, msanii Diamond na msafara wake wa yale ma ndiga yake makali akafika geti kuu kutaka kuingia, msafara ukazuiliwa, akaelezwa lazima ushuke, azunguke kwa miguu kuingilia geti dogo!, kumbe kosa!, ile Diamond kushuka tuu na kuanza kutembea kuelekea geti dogo na wale ma bodyguards wake, kukaibuka kelele huko nje, watu wakamzonga, polisi wakashindwa nguvu, watu wa usalama sukumiza kule, umati ukavamia geti kubwa, sukumiza geti chini, Diamond kuingia tuu ndani, kila mtu alisimama hadi JK kuangalia hii ni vurugu ya nini, kumbe ni Diamond!, hivyo Dai alikuwa maarufu kuliko JK!.

Baada ya verdict ya prima facie, kwa Tundu Lissu, sasa Tundu Lissu ndie mwanasiasa maarufu number 1 Tanzania kuliko hata nanilii, hivyo kwa sisi tunaomjua, naomba tuwasaidie wengine wasiomjua, ili kuwasaoidie wamjue, kwasababu tunaweza kuwa tufanya vi mambo vya ajabu ajabu tukijua ndio tuna mkomoa, kumbe ndio tunamuongezea umaarufu, huku nchi yetu ikizidi kubagazwa na kuchafuliwa kimataifa, kwa viongozi wetu kufanya maamuzi bila kutumia kanuni ya The Law of Unintended Consequences, ukajikuta badala ya kujenga ndio unaharibu zaidi!.

Bandiko hili ni bandiko elimishi kumhusu Tundu Lissu ninayemfahamu mimi toka shuleni kule Ilboru. Kama kuna watu wanadhani kumpiga kwa Prima Facie will bow him down kunyenyekea!, they are dead wrong!, Lissu ni wale watu watu wa type ya no retreat, no surrender, unapigana kufa na kupona, mpaka risasi ya mwisho, chozi la mwisho na tone la mwisho la damu, ndipo its over!, hivyo kwa Lissu, it is not over untill it is over!, linapokuja suala la kutete haki, heri afe huku amesimama kuisimamia kweli na haki, kuliko kuishi huku amepiga magoti!.

Naomba kwanza ni declare interest, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa mahakama kuu, neno "tutakinukisha" sio uhaini ni sedition tuu!, hivyo kama mahakama yetu imeona kuna prima facie ya uhaini, kwa maoni yangu, nauona uamuzi huu kama unakwenda sio tuu kutubagaza nchi yetu, but to expose how rot our justice system is before the eyes of international community. Msimamo wangu kuhusu kesi hii ni ule ule Pascal Mayalla: Kusema Tutakinukisha au kuandamana ...

Kwa vile TL namfahamu, ni mwana Ilboru mwenzangu, so does Mwigulu Nchemba na Lazaro Nyalandu, sisi wana Ilboru, tumefundishwa kusimama kwenye kweli, no matter what!.

Kama lengo la hii prima facie, is to make TL to bow down kwa kuogopa kuhukumiwa kifo kwa kosa la uhaini, hivyo baada ya kukutwa na prima facie, atakutwa na hatia, na atahukumiwa kifo kwa kunyongwa mpaka afe!, lakini baada ya hukumu kutoka, atatokea a saviour fulani, atamsamehe TL kwa msamaha wa rais, hivyo TL atarejea uraiani kichwa chini na hawezi tena kugombea wadhifa wowote!, then they are doing a terrible mistake!, the law of unintended consequences will take charge, hili jambo linakwenda kututesa kama nchi kuliko linavyochukuliwa sasa!.

Sisi wana Ilboru, tumefunzwa kusimama na haki, kuliko kunyenyekea kwa wadhalimu, huwa tuko tayari kufa, huku tumsimama kwenye haki, kuliko kuishi huku tumepiga magoti kuwanyenyekea wadhalimu!, sasa kwa vile sii wengi wanamfahamu TL kijuu juu tuu, mimi ni mmoja wa tunao mfahamu TL kwa undani.
Ili kuwasaidia na wengine, wasiomjua TL kwa undani, huyu ndiye TL ninayemfahamu mimi

View: https://youtu.be/nl3DZK-bXOM?si=wb7HlEOxwPdnNNcd

Hivyo kama amepigwa PF ili apige magoti kunyenyekea na kuomba msamaha,, huyu ni mtu wa no retreat, no surrender!, kama "tutakinukisha" sio uhaini, lakini watu wenye nia ovu, wameamua kuhainisha neno
"tutakinukisha na kuwa uhaini", then TL ata opt bora anyongwe, ila damu yake iwakomboe Watanzania, kuliko kuwa huru huku amepiga magoti kuwanyenyekea madhalimu.

Mzee Pasco
Rejea za Mwandishi kumhusu Tundu Lissu

  • ​


Je kutoa shillingi kwenye budget , ili kuiangusha serikali sio uhaini au kuitishia serikali.


Na je Kiongozi akiongelea kitu Kwa ukali sio kuwatishia wananchi ambao no serikali
 
Back
Top Bottom