Lissu ninayemfahamu mimi kama wanadhani 'Prima Facie' itamnyenyekeza, wanakosea sana!

Lete maana ya Neno kukinukisha toka kwenye kamusi kwanza tuone kama unasitahili Uteuzi?
 
Lissu kwa sasa ndio sura ya upinzani nchini kwa hiyo hata yeye najua kuna kete anazicheza vizuri kwa sababu akikosea step, political career yake inakufa.
Bila shaka, na ndio maana wanaotaka akapige goti labda hawaelewi itakuwa na implications gani kwenye career ya Lissu. Au wanafahamu ila wanacheza kekundu kekundu.
Uzuri ni mmoja. Yeye ndiye ameshikilia makali kwa sababu international community ipo nyuma yake kwa hiyo kesi yake. Si kama zingine za internal affairs kwa hiyo hii inampa upperhand kwenye negotiation zozote
Unawaamini hawa?
Hivyo kuna namna hii issue nzima ni ya

Ego mbili zilizokutana na zote zina power ya kutosha
Thinking of power kaka… Nadhani Lissu ana followers merely, wataka mabadiliko wote wanamuangalia yeye. Sasa kwa necha ya nchi yetu hii si kitu, real power wanayo watawala, na so far watawala mpaka sasa wameshatumia mbinu zote za ukandamizaji, ile 29 october wamecement tu, Kwa watu wa umri wetu hatujawahi kuona kitu kama kike popote nchini.

Swali je? Wanachi wametishika? Naona hapana ila wananchi wamebanwa, siioni chance ya watawala kuweka uzani wananchi waoneshe hasira zao kwa box la kura, au hata kutoa mwanya wa maandamano, ikitokea hivyo tutashuhudia maandamano makubwa ya ajabu nchini, until then sioni watawala wakizimbea hata kidogo. Haya yote hayampi favor Lissu wala mpinzani yeyote, so tell us more about power hasa ya upande wa pili.
 

Lissu power yake ni intervention ya nje,

Je, nawaamini HAPANA

Kwa sababu wanachokifanya ni kutumia kesi ya Lissu kwa ajili ya COLD WAR ambayo imevishwa sura ya Demokrasia

Angalia Eastern vs Western block zote zinachezwa Tanzania. Fuatilia ongezeko la influence ya China na Russia ndio utaelewa kwa nini Western countries zimeikaliza kooni Tz kuliko Rwanda.. SIMPLE

Msingidani analijua hili, na anajua international pressure inampa back up kwa sababu wote wana same interest against a common enemy. So yeye pia ana kete kubwa tu

Na hili si jambo jipya kihistoria

Kwa hiyo ukiona msingidani kakaa ndani naamini kuna TERMS hazijafikiwa ndio maana rulers wanaona kheri athari za nje kuliko athari za ndani zitazotokea kama msingidani hatokuwa nao kwenye same page

Kwa hiyo hata msingidani sio mnyonge kwenye hili na atapoteza advantage yake kama Western countries zitapotezea maslahi yake bongo. Kitu ambacho hakiwezekani
 
Duh, nahitaji muda ku-contemplate hili.

Aiseee!

Nimeona nisiandike kingine.

Good time brother.
 
Ni sawa na kumpiga teke chura unadhani unamkomoa kumbe ndio unamuongezea hatua.
 
Serikali ikishaongozwa na kilazaa utaona kila aina ya ujinga!
Lissu angekuwa ametoka siku nyingi.

Ila kwa yaliyotokea 29/10/2025, Viongozi wanahofu na baruti ya hasira iliyolundikana mioyoni mwa waathirika na wahanga.

Hiyo baruti inasubiri mtu kama Lissu kuichokonoa kidogo tu, inalipuka. Na mlipuko wake sio wa kitoto.

Nionavyo mimi ni vigumu mno kumwachia Lissu katika mazingira ya sasa kutokana na kumbukumbu bado hazijawatoka wafiwa, wajane kwa yatima na wazee waliopoteza maelfu ya vijana.
 

Uzi ufungwe hapa.
 
mchango wa mpumbavu utaujua tu
 
Bandiko bora sana kutoka kwako mzee mkubwa.

Natamani hao wanaopambaniwa na TAL wazinduke usingizini wakomboe uhuru na haki zao.

Wao pekee ndiyo wenye uwezo wa kumkomboa TAL na kujikomboa kutoka mikononi mwa madhalimu wanyonyaji wa haki.


#Hallelujah!!!
 
Well said...
Ila mtawala zile taarabu zake za "who are you?" Zilikua zinaonesha kabisa namna amejipanga na athari za so called "cold war" na ni kama tayari Alisha settle njia yake ya kutokea!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…