Lissu ninayemfahamu mimi kama wanadhani 'Prima Facie' itamnyenyekeza, wanakosea sana!

Well said...
Ila mtawala zile taarabu zake za "who are you?" Zilikua zinaonesha kabisa namna amejipanga na athari za so called "cold war" na ni kama tayari Alisha settle njia yake ya kutokea!!
Nachokiona, ni kama "tawala" Inacheza mchezo wa trial and error then terminate or repair..

Nachokiona hakuna clear roadmap ambayo ipo kwa sababu Tanzania haina hulka ya kufungamana na international block yoyote hivyo, ni kama mwanamke asiye na ndoa kamili lakini ana wanaume wawili anaocheza nao kwa muda na style tofauti ili aweze kulinda maslahi yake kwa pande zote mbili.

Lakini wakati huu ni tofauti. Oct 29 imeipa Tanzania disadvantage kwenye global politics haswa kwenye mahusiano yetu na western block ambayo ni face of democracy, so kinachotokea ni sawa upunguze mazoea na mpenzi unaefaidika nae zaidi na kwenda kuonesha mahaba yako zaidi kwa hasimu wake ili umpunguze makali ilhali wewe ndiye uliyemkosea kwa hiyo, hayo makali huna

Kwa hiyo hapo ni option mbili, urudi kwa wa siku zote kwa kukubali masharti yaks au uende extra miles kumridhisha mmoja kati yao ili akupe salio la kukutosheleza kusavaivu.

Japo options zaweza kuwa nyingi zaidi..

Ila leo nimejiachia sana, mkuu Pascal Mayalla Mayalla
Kama wakipitia thread waambie sina jambo mimi ni kijana mnyonge. Sina impact zaidi ya ukibodi waria🙏🏽😁
 
Nchi imetia aibu sana kwenye nyanja za kisheria, majaji aibu yao.

Sasa tunataka katiba ili hizo nafasi zishindaniwe ili tupate haki na siyo kutoa hukumu inayompendeza aliyekuteuwa.

Aibu naona mimi na Tanganyika yanguuuu, mshahara usio na kodi kwa majaji unasababisha wawe biasnes kwenye maamuzi.
 
MAWAZO YA UWANDISHI WAKO BADO NI MGANDO - Huwezi kuandika hoja nzito kama hii bila kupangilia hoja zako kwa mantiki ya msingi kama msomi mzuri - Unakuwa kama hujataka kuandika andiko kama msomi huru nadhani ujitafakari mwandishi kwa hilo maana upo very poor kabisa katika andiko lako unakuwa kama sio msomi au mtu umeenda shule kabisa .....
 
Kesi inapaswa kufutwa haraka sana maana mashahidi walijikanyaga na hata wanafunzi wetu watakuwa wanafundishwa kwa rejeo ya kesi yenye makosa. Tujajenga kizazi kibaya mno huko tuendako.
 
Nini maana ya Neno kukinukisha kwenye kamusi
 
Tawire!
 
Je kutoa shillingi kwenye budget , ili kuiangusha serikali sio uhaini au kuitishia serikali.


Na je Kiongozi akiongelea kitu Kwa ukali sio kuwatishia wananchi ambao no serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…