Lissu: Rais Magufuli haonekani kanisani wala mitaani, Msemaji wa Serikali atujuze

Lissu: Rais Magufuli haonekani kanisani wala mitaani, Msemaji wa Serikali atujuze

Hawezi kwenda kirahisi, alizoea akipewa nafasi ya kuongea kanisani anasema, naona pale Ma sister hamjavaa barakoa, namuona yule mama pale hajavaa barakoa, safi sana. Sasa kaambiwa live kuwa Mapadre 26 na Masista 60 wamekufa kwa changamoto za kupumua
 
Naam wakuu,

Leo ni Jumapili nyingine. Nimezoea kukutana na mnakasha humu JF au kukutana na mabandiko katika makundi sogozi ya WhatsApp yakiambatana na picha yakionyesha Rais alikoshiriki ibada. Mara nyingine hata akipewa nafasi kutoa neno kanisani.

Yupo Dar bado? Leo Machi 7, 2021 amesali wapi? Amepata nafasi ya kutoa neno?
Labda yuko Dodoma aliswali Ijumaa kwenye Msikiti wake alojenga kwa msaada wa Kanisa Katoliki kule Chamwino karibu na Ikulu, hakupewa nafasi ya kuhutubia, Waislam wangeshangaa Kafiri kuingia Msikitimi. Sasa ni mpenzi wa Allah baada ya kuona Changamoto ya kupumua haiishi licha ya yeye, msema kweli, na wanaCCM wote kumwomba Mungu wa Israel siku tatu mfululizo bila mafanikio. Labda hasemagi kweli Mungu kachukia, gonjwa linaongeza kasi!
 
Akienda na akirekodiwa shida ,asipoenda napo shida...
 
Mzee yupo amejaa tele.

Leo alikosa tu muda wa kuhudhuria ibada kutokana na kikao alichofanya na wasaidizi wake.

Kuna lingine la kuuliza Bwashee?
Anafanya kikao siku ya Ibada ? Kuna umuhimu kiasi hicho? Unless kama Nchi imevamiwa
 
Anafanya kikao siku ya Ibada ? Kuna umuhimu kiasi hi hicho? Unless kama Nchi imevamiwa
Aaahh unajua aaahh pale ikulu, eeehh huwa shughuli zinaendelea tu kama kawaida siku zote!! Eehh hatuna siku za ibada na sikukuu pale!! Sawa mkuu.
 
Kupitia kurasa ya ya Twita Tundu Lissu amehoji juu ya kutonekana kwa wiki mbili rais wa JMT akiwa kanisani.Pia hajaonekana uraiani, na inashangaza Greyson Msigwa na msemaji wa serikali kutopost taarifa yoyote ya rais akiwa anasali au mitaani kama ilivyokawaida yao.

Ikumbukwe kila jumapili rais Magufuli akienda kanisani lazima huko Twitani watu washuhudie akiwa anasali.

My take hoja ya Tundu Lissu sio ya kupuuza huenda kuna jambo
Screenshot_20210307-154643.png
 
Mzee yupo amejaa tele.

Leo alikosa tu muda wa kuhudhuria ibada kutokana na kikao alichofanya na wasaidizi wake.

Kuna lingine la kuuliza Bwashee?
Ungesema tu ukweli ili ukuweke huru. Kanisani hivi sasa ni mwendo wa barakoa...

Na barakoa inatisha....
 
Back
Top Bottom