Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Aliekuambia elimu ni kiingereza Nani? Wachina na wakorea wanaongea kiingereza? Unaweza kujilinganisha nao kimaendeleo? Acheni hizi aliki za kushikiwa na wazungu kwamba ili uonekane msomi lazima ujue kiingereza. English language is just a language like other languages nothing more
 
Kwahiyo hayo maendeleo ambayo anasema atawaletea watu kumbe ilikuwa anamaanisha kuongea kingereza vizuri?

Daah Chadema mmetuletea mtu wa aina gani?
Akili yako ni ndogo sana kumuelewa Lissu!
Aliyekuroga kafa kwakweli,ifike mahali ujitambue uko jukwaa gani na ushiriki mjadala kwa viwango vya jukwaa husika!
Hizi porojo unaishia kuonekana kituko mbele ya jamii ya walioelimika!
 
Mkuu hicho kichwa endelea kufugia nywele na kubebea masikio
 
Kwahiyo hayo maendeleo ambayo anasema atawaletea watu kumbe ilikuwa anamaanisha kuongea kingereza vizuri?

Daah Chadema mmetuletea mtu wa aina gani?
Makada wa CCM mmegeuka wa kupinga kila kitu!Subiri JPM aiunge mkono hoja hii ndipo akili yako itakaa sawa!
 
Hujamwelewa Lissu
 
Hata wewe uelewa wako ni mdogo sana hujui kuwa kwa sasa sera yetu ni kukuza lugha yetu ya kiswahili ili iwe lugha ya Afrika na imeshaanza kukubalika sasa inatumika SADC!! Kweli wanasaccos hawajitambui
mnaikuzaje wakati msingi wa lugha kuanzia chini ni mdogo. fuatilia walimu wazuri wa kiswahilli wapo kenya na wazungu wengi wanajifunza kiswahili toka kenya. kama kukuza kiswahili kianzie mashuleni sio magu anahutubia kwa kiswahili afu mnasema anakuza kiswahili.
 
Fikiria tu muda Mtu anaotumia kujifunza Kiingereza ajifunze na aelewe miaka 4 tu ya Sekondari anakuwa hajaelewa Kiingereza sawa sawa na anakwenda tena form 5 na 6 bado anakuwa vilevile, kwa kifupi Watu wetu hawajui Kiingereza.

Nakumbuka nikiwa form 1,definition mfano Physics,biology nk nilikuwa nakariri neno kwa neno!Hata nilikuwa sijui maana yake na ukija mtihani najibu na kufaulu bila hata kujua maana ya kile nilichojibu!I

meenda hivyo mpaka form 4,baadhi ya vitu ilikuwa ni kukariri tu kama kilivyo kwenye kitabu!Form 3,nakumbuka nilikariri maelezo ya mfumo wa kumeng'enya chakula ukurasa mzima wa kitabu!

Yaani process nzima kuanzia chakula kinapoingia kinywani mpaka kinapotoka na kimepitia hatua zipi mpaka kinatoka kama kinyesi!

Na kweli kwenye mtihani nilihamisha kila kitu bila kusahau nukta wala mkato!Mwalimu aliniita maana hakuamini nilivyonyoosha lugha,akaniambia nielezee!

Nikarudia vilevile,nikatema kila kitu kama nilivyoandika!Mwalimu akaishia kucheka na kuniambia nimuelezee kwa kiswahili,hapo nikachemka!

Kwakweli lugha ni changamoto sana,Lissu ana hoja ya msingi sana!
 
Bado hujamuelewa Lissu!Wengine mngesubiri wenye uelewa wachangie kwanza halafu nyie mkawa wa mwisho mwisho!
 
Aiseeee !!
 
Mnajibu upuuzi tupu, mmejazana wapuuzi.
Akili yako ikiona Lissu moja kwa moja inasema "reject"!Hata usiku utauita mchana!Jaribu kuacha akili yako ifanye kazi kwa uhuru,else huwezi kuona jema la usiyempenda!
Subirini hoja ikibebwa na JPM mtakuwa mstari wa mbele kuunga mkono!

Lissu kaachia goli wazi,ni waksti wa kuwa na mjadala utakaoamua tuelekee wapi!
 
Nyie wa Lumumba uelewa wenu mdogo sana .... jitahidini walau kurudia kusoma kama hamjaelewa kitu!! Ndiyo maana Membe ameenda ACT anadai amekuta vijana kule walivyo na akili kuliko pakaaliowaacha Lumumba....!!
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚,kwamba CCM ameacha vijana mabox matupu?
 
Mkuu sisi kayumba tumepata tabu sana huko vidato!Mambo ni kukariri tu!Nikiwa form 3 niliwahi kukariri page nzima kwenye kitabu ya mfumo wa umeng'enyaji chakula,sikuacha hata nukta!!Kwenye mtihani ukiniletea mimi napaste tu!Kasheshe niambie nikuelezee hatua kwa hatua!
Lugha ni changamoto sana,sio kwenye kuongea tu bali hata huko kwa wanafunzi wa sekondari!Wanaotoka medium huwa wana nafuu sana!
 
Hata bidhaa zao wanazitangaza kwa kiingereza kilicho nyooka hivyo wachina wapo vizuri katika kujifunza na kutumia kutumia English language
Mataga wao ni kumpinga tu Lissu ila kila hoja ya Tundu ni mwiba kwa utawala uliopita
MATAGA bwana! China kwa taarifa imewekeza mno kwenye Kiingereza sasa.
 
Mkuu watu wanapokuwa wanajadili mustakabali wa elimu ya watanzania uwe unajikali kando tu usubiri mada zinazohitajia mipasho kama kwenye taarabu!
 
The Greatest
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…