Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Ninachosema kuwa Lissu asitulazimishe kuonge English kama mother tongue yetu. Tutaongea English accordingly,iwe kwa ulimi wa kihaya au kijaluo. Sorry Jaduong!
Bila Shaka uliona mazungumzo na balozi wa US . Ahahahaaaa [emoji3][emoji23] [emoji1787]
 
Soma vizuri uelewe
 
Hawa mataga ni wapumbavu Sana kazi yao ni kupinga kila Jambo
Bila jet lee ,jack chan, don yen kucheza muvi na kuongea kingereza kizuri ungewajulia wapi, asilimia 10 ya wachina wote wanaongea kingereza

Wapuuzi kweli,hawajiulizi kwa nini wazazi wengi wangepewa option ya kuchagua.. WOTE wangepeleka watoto wao Kwenye shule za international ..na moja ya sababu ni Lugha ya Kingereza...sasa badala tupigane Kingereza kiwekwe kwenye mitaala yetu kiwe affordable kwa kila mtoto wa kitanzania..wenyewe wanakuja sijui na upuuzi gani...mkubali mkatae lugha ya Kingereza bado inakua na kuhitajika ulimwenguni,wameng'ang'ania wachina this wachina that...huyo mchina akija Tanzania,lugha gani ataitumia ku communicate na wewe mtanzania kama sio English??? ndio ujue umuhimu wake sasa...
 
Kiingireza ni ugonjwa wa taifa kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anaongea na mtu wa kigeni kwenye simu kwa lugha hiyo ya kigeni nilitamani hata nimpokonye simu ni aibu
 
Wewe utakuwa una wendawazimu. Hujaelewa hata hoja inayoongelewa.

Lisu anazungumzia juu ya tatizo la kutumia lugha mbili kama lugha za kufundishia masomo. Wewe umekwisharukia kwa Waxhina. Huko China umesikia kuwa mtaala wao wa Elimu unatumia lugha mbili kama sisi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeelewa lisu anachojaribu kueleza au umekimbilia kureply ili uwahi nafasi?
 
Hivi jiulize uyo mtaalamu maarifa anayapata kutoka vyanzo gani na vimeandikwa kwa lugha gani? Siongelei wataalamu wa jadi.

Mimi binafsi siwezi kuandika kiswahili kwa ufasaha na kingereza ivyo ivyo . Ndyo haya lissu anayoengelea . Tuna ndimi mbili na hatuwezi master zote
 
Unakurupuka kujibu wakati hujaelewa hoja!Hapa tunasema lugha ya kufundishia iwe moja,ni ama tuchague kiswahili au kiingereza!
China wao wamechagua kichina,na kiingereza ni kama somo tu!
Muwe mnaelewa kwanza kabla ya kukurupuka kujibu mataga nyie!
Huu usajili wa bashiru zero kabisa?
 
Afrika Kusini wanafundisha kwa lugha ngapi vile??? 👂🏿👂🏿👂🏿👂🏿👂🏿👂🏿👂🏿👂🏿👂🏿
 
Wewe na umasikini wenu huwezi kujilinganisha na wachina, nyinyi hamuwezi hata kutengeneza hata tooth pick.

Kwenye ukweli lazima mkubali kuwa kuna mambo mmeyakosea tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja ya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ktk ngazi zote za elimu i.e Kindergarten to University college level...

Kwa sasa 90% ya walimu wetu wanaofundisha ktk shule zetu za sekondari hadi chuo kikuu hawajui Kiingereza kwa ufasaha na ndiyo hao wanawafundisha watoto na vijana wetu wasiojua kiingereza pia...

Ktk hali hii fikiria matokeo yake. Maana yake ni mjinga kuhamishia ujinga wake kwa watoto na vijana wetu....!!
 
Naona kama vile umekurupuka kutoa jibu.
 
Fikiria tu muda Mtu anaotumia kujifunza Kiingereza ajifunze na aelewe miaka 4 tu ya Sekondari anakuwa hajaelewa Kiingereza sawa sawa na anakwenda tena form 5 na 6 bado anakuwa vilevile, kwa kifupi Watu wetu hawajui Kiingereza.
Na hiyo ya kutojua kiingereza vizuri unakuwa ni shida sana kwa mwananfunzi anapoenda kujiunga form one.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…