Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Magufuli and I like listening to Tundu lissu for there are so many things to learn as far as the history of this country's concerned. he's a history & political class on it is own. lissu doesn't speak like regular politicians do. he speak as an intellectual who's passionate about justice
 
Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua kiingereza?????? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu.We want to make Tanzania great nation,kiswahili ni ajenda kuu
Amri za Mungu zisingekataza kuua, wewe ulistahili kuuliwa. Maana kichwa chako badala ya kuwa msaada kwako kimegeuka kuwa mzigo kwako.
 
Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua kiingereza?????? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu.We want to make Tanzania great nation,kiswahili ni ajenda kuu
Tundu Lissu atakufanyaje mjinga wakati tayari ulishakuwa mjinga?
 
Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua kiingereza?????? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu.We want to make Tanzania great nation,kiswahili ni ajenda kuu
Kwahiyo hayo maendeleo ambayo anasema atawaletea watu kumbe ilikuwa anamaanisha kuongea kingereza vizuri??

Daah Chadema mmetuletea mtu wa aina gani??
Nyie wa Lumumba uelewa wenu mdogo sana .... jitahidini walau kurudia kusoma kama hamjaelewa kitu!! Ndiyo maana Membe ameenda ACT anadai amekuta vijana kule walivyo na akili kuliko pakaaliowaacha Lumumba....!!
 
"Ukiniuliza mimi, honest opinion Nchi yetu haiwezi kuzungumza Kiingereza, hivyo tunahitaji kuwa na mjadala juu ya sera ya lugha, tusipokuwa na mjadala huu, hatufiki popote kwani language of instruction is everything" - Tundu Lissu akizungumza na Wanahabari nyumbani kwake DSM

"Mimi ni Wakili, Majaji wengi hawajui kiingereza, ukienda Nchi za wenzetu huko Mtanzania akiongea unatamani kuingia uvunguni mwa meza, Kiingereza chetu ni kibaya, sio kwasababu hatuna akili ila ni kwasababu tumekosa Sera ya Lugha" - LISSU

"Tangu tumepata Uhuru tumekua na ndimi mbili kuhusiana na lugha na ndimi mbili ni hatari, ulimi mmoja tumesema Kiswahili ni lugha ya Taifa na tumeiendeleza kwelikweli, ulimi wa pili tumesema Kiswahili si lugha ya kufundishia" - LISSU

"Fikiria tu muda Mtu anaotumia kujifunza Kiingereza ajifunze na aelewe miaka 4 tu ya Sekondari anakuwa hajaelewa Kiingereza sawa sawa na anakwenda tena form 5 na 6 bado anakuwa vilevile, kwa kifupi Watu wetu hawajui Kiingereza" - LISSU
Ulikuja na mawazo hasi dhidi ya Lissu ukitegemea mashambulizi dhidi yake, lakini wajuzi wamekuumbua hapo juu.
 
Ni kweli kabisa ndio maana baadhi ya viongozi wetu wakuu wanaogopa kwenda ulaya sababu lugha ya kiingereza haipandi.🤣

They are timid of hard talks.
 
Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua kiingereza? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu.We want to make Tanzania great nation,kiswahili ni ajenda kuu

Kama nimemuelewa vizuri, anataka tuchachague moja, kiingereza au kiswahili. Kama ni kiingereza basi tuanze nacho tangu chini kama wenzetu wakenya, au Kama ni kiswahili tuhakikishe ndicho kinakuwa lugha ya kufundishia.

Ndiyo maana hao wachina uliowataja wamefanikiwa kwa sababu sera yao ni kutumia kichina kama lugha ya kwanza na ya kufundishia.
Unaweza ukarudia kusoma tena Kama hutojali.
 
Well, lugha ya taifa ni kiswahili.. ikitokea kiswahili kinapitishwa kama lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwaje kwa upande wa kuongea hicho kingereza? Mimi sioni kama kuongea kingereza kinahusiana na namna elimu yetu ilivyo, maana mtu anasoma sekondari miaka 6 kwa lugha ya kiingereza sasa akishindwa kuongea kingereza mtu huyo utasema tatizo ni lugha ya kujifunzia na kufundishia au tatizo ni la mtu binafsi? Lugha ni juhudi ya wewe kujifunza na kupenda kuiongea tu bhas.

Halafu sitegemei mtanzania awe anazungumza kingereza kama mwingereza au mmarekani, hiyo ni uongo na haiwezekani, mmarekani ambae alipelekewa lugha hiyo na muiongereza hata yeye hakuweza kuongea kama mwingereza, alikuja na namna yake ya uongeaji na utamshi wa maneno. Cha muhimu ni kuangalia je ile dhima ya lugha inafikiwa? Ukishaweza kuelewana na mtu na kubadilishana taarifa inatosha ndio lengo la lugha, sio namna ya kutamka maneno.
 
Nimemuuliza mwenzangu kama fomu ya Devotha Minja ilikuwa imeandikwa kwa kiingereza akasema hapana, sasa Lissu na "kiingereza" kwenye kampeni za uchaguzi vinahusiana vipi? Naomba nijibiwe makamanda! Au ndio sababu anapenda aongee na vyombo vya habari vya nje wanaojua kiingereza?
 
Kati ya siku Lissu ameongea ujinga na utumbo ni leo, yaani lugha iwe kigezo cha kutopata maendeleo, hapana watanzania sio wajinga kiasi hicho, swali lakujiuliza kwa nini kumekuwa na taaluma ya Tafsiri na Ukarimani. Lissu jipange upya nchi kama urusi, uchina nchi za falme za kiarabu wanatumia lugha zao na wako vizuri kiuchumi.
 
Kutokujua kiingereza inakuwaje kilema. Watanzania wanahitaji zaidi ya lugha kufikia mafanikio. Wanahitaji ujuzi na maarifa thabiti, na maarifa hayo lazima yatolewe si kwa lugha ya kukopa. Lugha ni mbeleko ya kubebea utamaduni na weledi wa binadamu kokote duniani ndio sababu pia mataifa yenye maendeleo makubwa wameendelea kubaki na lugha zao za asili na kujifunza lugha zingine ili kuzijua. Huwezi kuendelea kwa lugha ya mkopo!
 
Kwa hili Tundu Lissu Yukon sahihi, kama taifa tunatakiwa tuchague lugha moja itumike kiofisi na iwe lugha ya kufundishia kuanzia shule ya msingi Hadi chuo kikuu, hapa kwetu tuna jichanganya mara kiswahili mara kiingereza hapo ndio shida inapokujia, hajasema tufute kiswahili tuongee kiingereza kasema tuchague lugha moja sasa sio kazi ya Lissu kuamua ni lugha ipi itumike ndio maana kasema tunatakiwa tuwe na mjadala tuamue, yuko sahihi kabisa.
 
Wakulaumiwa ni Nyerere na kiherehere chake Kiswahili ni kitamu ila kimetunyima ubarikio wetu tuliopewa na bwana kukamilika kwa 100%!

tulipaswa kuwa namba 1 Afrika kwenye kila kitu.
1. Umalaya tunauweza.
2. Umbea na majungu hakuna anayetuweza.
3. Roho mbaya ndio sisi.
4. Roho nzuri sisi.
5. Mdomo tunao, tunaongea ni hakuna mfano.
6. Ujinga ni namba moja.
7. Ujuaji hakuna kitu hatujui.


Tatizo ni ka lugha tu WAJAMENI, malaya wa sea cliff pale wanapata taaaabu sana
Dah!
 
Hapa kagonga point bwana lissu, ila pia kizazi cha sasa hivi wengi wanasoma shule za English medium tunapoelekea haitakua tatizo tena, watoto sasa hivi wanaongea kiingereza vizuri sana,
 
Ukiniuliza mimi, honest opinion Nchi yetu haiwezi kuzungumza Kiingereza, hivyo tunahitaji kuwa na mjadala juu ya sera ya lugha, tusipokuwa na mjadala huu, hatufiki popote kwani language of instruction is everything" - Tundu Lissu akizungumza na Wanahabari nyumbani kwake DSM
 
Back
Top Bottom