List of Rostam and Akram Aziz companies & Mohamed Enterprises

Nini kipya hapo? Au deal kuandika jina la Rostam... maana hayo makampuni ndio aliyoorodhesha kwenye tovuti ya Bunge miaka kadhaa iliyopita.

Huyu naye unamtetea badala ya kuhitaji kujua meengi yanayomuhusu?

Ukiamua kuwa objective, lazima utaona la maana ktk hayo yote. Hakuna mfanyabiashara serious Duniani kote ambaye ataunda makampuni yote hayo bila kuwa millionea wa Dunia.

Sheria za Makampuni zinaeleweka. Ukiiunda halafu unaiacha hewani bila kutangaza kufirisika kwake, pia inaeleweka ni nini ukipate toka ktk sheria.

Hii bi dalili ya ufisadi, tena mkubwa.

Wabia wengine walioko ndani ya Bakhresa na makampuni yake, ni jamaa wa ikulu yetu. Huyo munayemuita JK.

Kampuni ya Ngozi iliyotajwa kuwa kule Morogoro, ni utapeli. 'Alipewa' kiwanda kwa kisingizio cha ubinafsishaji. Hakuwahi hata kuendeleza kiwanda na badala yake alihamisha mashine kupeleka Komoro! Taarifa zilifika PCB, alichunguzwa matokeo yakazuiliwa kwa amri iliyoitwa ya ngazi za juu. Nenda ukaone kama kuna kitu kiitwacho mashine. Hili tu ni sifa tosa ya kuwa fisadi na marafiki zake, hao akina JK.
 
KASHESHE..unaendekeza upinzani ambao hauna tija..kwa jinsi unavyochangia unaonekana wewe either ni kabaraka wa rostam au umetumwa kuvuruga tu mijadara hapa ndani...wewe pia huna uwezo wa kupinga hoja ya mtu kwa kumtetea mhusika direct...hatutakiwi kuonyesha ushabiki sana na badala yetu tunatakiwa tuonyeshe njia...whether ni mengi au rostam, tunatakiwa kama wachambuzi wa mambo kuwa makini katika kujadili hoja zinazowahusu kuliko kuwatetea au kuwakkandamiza...utanisamehe ila ni bora kumrekebisha mtu kihoja zaidi kuliko kupinga kabisa.....na pia wana JF mnapoleta hoja msitutege...kuweni wawazi na sababu za kuleta hoja zenu ili mwishoni ipatikane michango yenye tija....asanteni
 
Ndugu yangu mchambuzi yeyote ambaye anajua biashara hawezi tumia hizi sentensi zako... kukubali kumwita mtu mwizi au fisadi.

Ninachopinga ni kumwita mtu mwizi au fisadi bila kuwa na ushahidi ulio clear bila kiwa na doubt yoyote.

Kukishakuwa na walakini kwenye ushahidi wowote ule unatakiwa kutosema fulani ni mwizi au fisadi.

Mimi siwezi shabikia jamaa kwa kuwa hanijui na wala sina uhusiano wowote zaidi ya uwe wa yeye ni Mtanzania na mimi ni Mtanzania.
 
Samahani, kama hayo manano yamekukwaza lakini siamini kwamba anayetumia maneno hayo hajui biashara. Nadhani ulitaka kusema jingine. RA amekwisha sema ni mfanyabiashara. Ulisikia maneno aliyotumia wakati akijibu hoja ya Mengi? Yamekwisha.

Lakini hakika, Biashara Duniani siyo za aina hii. Kwa huyu jamaa yetu Kila anapoona anaweza kuchota pesa, anaunda kampuni, inachota kwa mtindo wake na kupotea. Hiyo ndo analysis yangu.

Kuhusu uamuzi wa kumuhukumu au la, hapa ni kwenye forum. Siyo mahakamani. Tunajadiliana kwa misimamo tofauti na kwa maana hiyo kila mtu anajaribu kuthibitisha msimamo wake. Mimi naamini huyu RA ni fisadi najaribu kukupa mifano, kama huo wa kiwanda cha ngozi. Baada ya kueleza mfano kama huo, hitimisho langu ni kusema ni fisadi. Siwezi kueleza yote hayo baadaye hitimisho iwe kinyume cha hilo.

Wewe au mwingine ana ushahidi tofauti. Hitimisho lazima liwe tofauti.
Sasa ukishasema uzuri wake RA mwishoni ukasema "nasema hivyo kwa sababu huyu ni Mtanzania kama mimi...." then what?

Hata kama ni mahakama, kuna pande mbili za misimamo tofauti.

Tukienda hivyo baadaye nitafanikiwa kukushawishi kwamba RA ni FISADI.
 
Mfumo ni watu. Lenga watu/mtu. na Rushwa haipatikani hewani. Rushwa inafanywa na watu. Rushwa inayozungumziwa hapa ni ya kiwango cha "mafisadi papa". Rostam ni papa.

Sio kila jambo linahitaji elimu ya kurusha maroketi. Masuala mengine ni mepesi tu kuyaelewa, kama a, be, na che.

Ni mtazamo tu.
 
Just kuongezea jamaa alivyojificha na mizizi yake. Pia ni mwenyekiti wa Bodi ya Chai Tanzania.

The Tea Board of Tanzania TBT) is a corporate body established by the Tea Act No. 3 of 1997 after the separation of the regulatory and development functions of the then Tanzania Tea Authority. It is entrusted with the mandatory responsibility of regulating the tea industry in Tanzania. The Board came into force on the 1st October 1997. The main functions as set out in the Tea Act No. 3 of 1997 are as follows:

Board of Directors
Currently the Tea Board of Directors is composed of eight ( members under the Chairmanship of Hon. Rostam Aziz (MP) as follows:-
1. Hon. Rostam Aziz (MP) - Chairman
2. Hon. Prof. Raphael B. Mwalyosi (MP) - Member
3. Hon. Abdi Mshangama (MP) - "
4. Prof. Bruno Ndunguru - "
5. Mr. Andrew Mitei - "
6. Mrs Sophia Kaduma - "
7. Mr. George Kyejo - "
8. Mr. Peter Rowland - "
The Board of Directors assumed its responsibilities on 01/10/2006 and will last for three years to 30/09/2009
 
Inashangaza sana kuona watu wanakataa kabisa kuona kwamba ccm imeloot hazina ya nchi!
juzi nilikuwa naongea na diwani mmoja wa ccm kijana mdogo degree mbili kasoma nje ya nchi miaka mingi. Nikadhani jamaa kweli atakuwa na uelewa mkubwa na kama mwanaccm atakuwa na changamoto na mawazo ya kisasa...lakini mambo aliyokuwa anayaongelea bora nikamsikilize capt.komba au makamba!
Hamna cha rostam wala mo. Hawa wamekuwa matajiri kupindukia kwasababu ya njaa ya viongozi mbalimbali serikalini (hakuna director alifanya kazi bot for more than 20yrs asiyekuwa na access to chini ya sh billion 2 ( i stand to be corrected) ..mohammed enterprises utajiri wake umetokana na kuhusika na kifo cha GAPEX (kosa la nani??) hawa vodacom tunalalamika nao tunasahau kuwa TTCL inakufa kifo kibaya sana..asset zake watu wanagawana kila siku (kosa la nani?)

HUUU SI UVIVU KASHESHE NI TATIZO LA KUWA NA SERIKALI ISIYO ELEWA NENO 'Accountability'
Mataka kaaingiza ATCL pabaya then anapewa u director NIC??
HII NDO SERIKALI YA CCM
SERIKALI ISIPO JUA KUWA KALI (Zaidi ya kupambana mengi kipuuzi..lol) Isitegemee kutokuwa na Ufisadi...
 
Endelea kuona kuwa haya mambo ni rahisi.

Kuoga si sawasawa na kuogelea, huhitaji mbinu katika kuoga, lakini je unaweza kuogelea bila ya mbinu?
 
Hakuna hoja hapa, tafuta jingine.
 
nadhani haipendezi kupeana woga hapa !!!
 
ULITAKA USHAHIDI TOKA MBINGUNI ? HUWA HUFUATILII MAMBO , NINA HOFU SANA 😕 KAMA UTAKUWA MTANZANIA HALISI BASI UNALAKO JAMBO..!!
 
Endelea kuona kuwa haya mambo ni rahisi.

Kuoga si sawasawa na kuogelea, huhitaji mbinu katika kuoga, lakini je unaweza kuogelea bila ya mbinu?

I GUESS HATA KATIKA KUOGA KAMA HUNA MBINU ZA KUJISAFISHA VIZURI BASI INAWEZA KUTIA SHAKA MBELE ZA WATU..!!

SHULTI UJUE JINSI YA KUJIPAKA SABUNI , KUJISUGUA NA KUJIMWAGIA MAJI...!

AU KUOGA NI KUJIMWAGIA MAJI KWA KOPO TU 🙄?
TUNAJIFUNZA MENGI !!!!!!!
 
Wewe ungekuwa umepanga mambo yako na umekwisha fanikiwa usingekuwa hapa na mawazo yako duni kumtetea mtu kwa umaarufu wa kuchemsha.
Kwamba uko hapa kumtetea mtu amabaye ni maarufu kwa sababu ya jina lake kujitokeza katika kila Umafia, inaonekana wazi kwamba bado hata hujakanyaga kipandio cha kwanza cha ngazi kuchanganya Bongo.
Lakini inawezekana uko sahihi na utetezi wako, njia za kuachana na uchache wa fedha mfukoni ziko zaidi ya elfu lakini zinajigawa katika mafungu mawili tu, HALALI NA HARAMU. Ya kwanza ni Kuiba( KUCHUKUA KWA NAMNA YEYOTE KISICHO CHAKO) na ya mwisho ni kutembea na Bakuli la Matonya huku umevaa suti(KUOMBA MISAADA, KUJIPENDEKEZA NA KUJIPITISHA). Zilizo baki 988 ni home work yako ukishindwa Waulize Nyati na Nyumbu wakusaidie.

Wewe ni mwenzetu tu, unajivunia kubebwa, lakini kumbuka umebebwa na mbeleko yenye matobo umejisahau.
 
Last edited:
Hivi kuwaibia watanzania na kufanya biashara za kihalifu kama utumwa na pembe za ndovu ukapata utajiri hayo nayo utayaita mafanikio?
 
Kapinga unaongea the same issues ambazo mimi kila siku nagombana na watu ambao awaelewi iweje mtu afikie hapo iwe fisadi papa au nyangumi au for that matter Mtanzania wa rangi yoyote. First mimi si condemn a business man, give people the benefit of the doubt not guilty until proven so. Lazima tukumbuke kuna watu watafanikiwa kwenye biashara anywhere ulimwenguni na iwapo nchi yenyewe Tanzania when there is so much to develop wajanja wataona tu hela iko wapi ilo si kosa la mtu. Saying that people like Rostam should produce all the documents and dealings on how they acquired those assets. Reason being tusiongopeane mimi na amini amna mtanzania aliezaliwa na bahati ya baba yake mfalme, serikali inawalipa kodi kwa hivyo maisha mazuri, ingawa viongozi wetu wameshajenga imani tanzania ni ya kwao wenyewe. Hivyo basi asilimia kubwa ya matajiri wetu leo tanzania ni mikopo ya benki au abusive of power. Sawa kama ni nchi ambayo imeamua capitalism we need to start somewhere na watu wapewe capital. tatizo ndipo lilipoanza waliokuwa madarakani wanatoa mikopo sio kwa nia ya kukomaza capitalism bali kwa nia ya kujisaidia wenyewe hivyo mikopo ailipwi wao wanapata ganji lao life goes on. hii ni sera ya tanzania mpaka tumeua NBC. Sasa benki tena mchezo umeshakua mmbovu dili zimeamia kujibinafsishia makampuni ya serikali, kwanza kabisa capitalism yetu its still in a 'tot' state instead of the government trying to stablize what primitive industries it has got, and try to modernize them so that mlalahoi can make a living it goes and auction them within themselves let me tell you most of this companies dont last 10yrs more, they acquire them and use them as the basis of getting bank loans and not much is being invested back in the companies thats why this companies dont last in the hands of fools. But guess what the government is going to come up watataifisha the company as if to say mali yetu aipotei. ata uziwa mjinga mwingine the same ritual repeats its self. kwa mimi na wewe serikali imewanyan'ganya makampuni mafisadi kwa wao tayari wameshatajirika. wakitoka hapo ndipo uanza miradi yao ya kweli midogo na mara nyingi ushamiri.
During the fisadi Papa and Nyangumi beef much was said by Rostam on Mengi but no action is yet to be taken this is why i do agree with you Kapinga, the issue is not who has what; but its what the government has given them. therefore the finger should be pointed to the people in power and we know what happens to those MP who try to raise these issues car accidents are never far away from them.
 
Last edited by a moderator:
Kapinga unaongea the same issues ambazo mimi kila siku nagombana na watu ambao awaelewi iweje mtu afikie hapo iwe fisadi papa au nyangumi au for that matter Mtanzania wa rangi yoyote. First mimi si condemn a business man, give people the benefit of the doubt not guilty until proven so. Lazima tukumbuke kuna watu watafanikiwa kwenye biashara anywhere ulimwenguni na iwapo nchi yenyewe Tanzania when there is so much to develop wajanja wataona tu hela iko wapi ilo si kosa la mtu. Saying that people like Rostam should produce all the documents and dealings on how they acquired those assets. Reason being tusiongopeane mimi na amini amna mtanzania aliezaliwa na bahati ya baba yake mfalme, serikali inawalipa kodi kwa hivyo maisha mazuri, ingawa viongozi wetu wameshajenga imani tanzania ni ya kwao wenyewe. Hivyo basi asilimia kubwa ya matajiri wetu leo tanzania ni mikopo ya benki au abusive of power. Sawa kama ni nchi ambayo imeamua capitalism we need to start somewhere na watu wapewe capital. tatizo ndipo lilipoanza waliokuwa madarakani wanatoa mikopo sio kwa nia ya kukomaza capitalism bali kwa nia ya kujisaidia wenyewe hivyo mikopo ailipwi wao wanapata ganji lao life goes on. hii ni sera ya tanzania mpaka tumeua NBC. Sasa benki tena mchezo umeshakua mmbovu dili zimeamia kujibinafsishia makampuni ya serikali, kwanza kabisa capitalism yetu its still in a 'tot' state instead of the government trying to stablize what primitive industries it has got, and try to modernize them so that mlalahoi can make a living it goes and auction them within themselves let me tell you most of this companies dont last 10yrs more, they acquire them and use them as the basis of getting bank loans and not much is being invested back in the companies thats why this companies dont last in the hands of fools. But guess what the government is going to come up watataifisha the company as if to say mali yetu aipotei. ata uziwa mjinga mwingine the same ritual repeats its self. kwa mimi na wewe serikali imewanyan'ganya makampuni mafisadi kwa wao tayari wameshatajirika. wakitoka hapo ndipo uanza miradi yao ya kweli midogo na mara nyingi ushamiri.
During the fisadi Papa and Nyangumi beef much was said by Rostam on Mengi but no action is yet to be taken this is why i do agree with you Kapinga, the issue is not who has what; but its what the government has given them. therefore the finger should be pointed to the people in power and we know what happens to those MP who try to raise these issues car accidents are never far away from them.[you can fool people sometimes but you cant fool all the people all the time]
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuwaibia watanzania na kufanya biashara za kihalifu kama utumwa na pembe za ndovu ukapata utajiri hayo nayo utayaita mafanikio?

Tunachofurahi zaidi ni kwamba hawa mafisadi sikuhizi wanatumia mda mwingi kufanya utafiti wa nini jamii injua husu vitendo vya ili wafiche ushahidi rather than kutumia huo mda kupanga mbinu za kutuibia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…