List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Hey! yamekuwa haya.........

Masatu hii ndo JF....ukiwashinda kwa hoja watakushinda kwa personal attacks, ukiwa mtu wakuangalia pande zote za safaru wanasema umetumwa....wakati huo huo wanadai "Where we Dare to Talk Openly"....but DONT Dare to Talk Open-mindly...
 
Masatu hii ndo JF......but DONT Dare to Talk Open-mindly...

ohhh crap....

Kuna mtu yeyote kakuzuia kuongea openly hapa? kulialia huku ndio kunashangaza..... crying all the time! gooosh... grow up

Unless kama umeandikiwa PM na Admin.... so far sijaona Admin au mtu yeyote akikuzuia kuongea hapa kama CCM mulivyomfukuza ZITO kutoka bungeni!
 
ohhh crap....

Kuna mtu yeyote kakuzuia kuongea openly hapa? kulialia huku ndio kunashangaza..... crying all the time! gooosh... grow up

Unless kama umeandikiwa PM na Admin.... so far sijaona Admin au mtu yeyote akikuzuia kuongea hapa kama CCM mulivyomfukuza ZITO kutoka bungeni!

heheheheheheh, I can't laugh louder than that. Ohh gosh,,,your postings are like funny commercials at the midist of a good movie....keep it up....we need such breaks.
 
Mkubwa akijamba humsingizia mdogo.
Taabu ni pale mdogo akitoa kauri yenye ushahidi kwamba mkubwa ndo kajamba.
Kingunge anazidharirisha MVI kwa kutetea Ufisadi, huyu ni lazima ataingia kaburini huku vijana wa njini wakimsindikiza kwa
K%^$^#$O Mzee Kingunge M%^$#^(&E Mkubwa UnaF^%A na vijana wako wa SISIEMU.

Sijui sasa nianze kuamini kwamba Mvi kama za Lowassa ndo kipimo cha ujinga???
 
Masatu hii ndo JF....ukiwashinda kwa hoja watakushinda kwa personal attacks, ukiwa mtu wakuangalia pande zote za safaru wanasema umetumwa....wakati huo huo wanadai "Where we Dare to Talk Openly"....but DONT Dare to Talk Open-mindly...

Hujamzidi yeyote kwa hoja hapa, ila kwa kuanika ugonjwa wako na kutetea mafisadi. Wala hakuna aliekuzuia kuwatetea, isipokuwa umetusaidia kupata utambulisho wako. Kuona pande zote za shilingi sio kutetea yasiyoteteka. Soma hapo juu uone babu yako Kingunge alivyojibiwa na wapinzani.

Taifa zima linalilia mali zinazopotea kwa ufisadi wewe unawabeza wanaotusaidia kufichua ufisadi. mambo mengine muwe mnayafanyia vyumbani kwenu, msiyalete hadharani. Kwani wewe una uchungu na tuhuma hizo kuliko Rostam, Karamagi, Chenge, Balali, Mkapa, Kikwete, Rutabanzibwa, Mkono, Mramba na Lowassa? Uanshindwa kuchunguza kisa cha kimya chao unamshambulia aliyeibua uoza wao? Halfu unasema umeazidi watu kwa hoja? Hoja gani?
 
No wealth like knowledge,No poverty like ignorance.
 
Ndanda Kosovo alisema Uchumi unapaa na ndiyo justification ya kuuza madini yetu kwa bei ya chee . Achana na Kichaa Kingunge anaongea hadi anasahau anachokisema .
 
Wakati mwingine mtu anatetea Ufisadi kwa mazoea tu.

Nililazwa Muhimbili pale mwaisela mwaka fulani kukiwa na Kesi ya wizi wa Mahela wizara ya Afya.

Kila kitu ilikuwa taabu, kupata kitanda taabu, kupata dawa taabu, kwenda kuchukuliwa kipimo taabu hata kutoa Rushwa tu ili upate huduma ilikuwa taabu. Rushwa ilikuwa inapokelewa kwa kufahamiana.

Mgonjwa mmoja akaleta gazeti la daily News na Mfanyakazi.

Yote yalikuwa na vichwa vya habari juu ya wizi huo wa mamilioni.

Cha kushangaza 90% ya wagonjwa pale Wodini kwangu waliwasifia wezi wa fedha za Wizara ya Afya Kwamba wamechangamka.

Walinishangaza zaidi waliposema hata wangekua wao wangefanya hivyo hivyo.

Mimi nilibaki nimeachama domo kama Chewa kwa kushindwa kuamini.

Wenzangu wale pale Mwaisela hawakuwa wakiona Uhusiano kati ya Wizi wa Miela pale Wizara ya Afya na huduma mbovu pale Mwaisela.

Si kila mwenye macho anaona.
Si kila mwenye masikio anasikia.
Pia,Si kila mwenye ubongo anafikiri.
 
Wasee JF,

Hivi mie nataka kujua kwanini kama mtu una maslahi binafsi usijitoe ktk debate kama hizi??? kuna faida gani kutaka kupotosha facts??hii ndio sababu inafanya mara nyingine watu kwenda personal na kusema yasiyotakiwa.........halafu baadae watu mnaanza kulalamika, Mtu na wenzako aibu na utu vipo wapi? mkiambiwa mmetumwa mnalalamika...........basi labda mna mtindio wa ubongo, iweje sie tunaona nyie msichokiona??
 
Ahsante Mgonjwaukimwi,wengine tukisema humu tunaonekana kama tumetumwa.Lakini sio ndugu zanguni,mimi nafikiri kweli Dr slaa muda huu angekuwa kashabisha hodi mahakamani na sio kusubiri akina Kingunge watege Patrot zao!

kana ni kweli unafanya ufanyavyo kwa hiari yako basi una mushkeli mkubwa sana na ni vigumu kukuamini.............jaribu kuwauliza wenzako ambao mpo upande mmoja ktk debate hii kwanini wanamisimamo inayofanana na wewe, labda utapata jibu na pengine watakutoa kwenye ligi za mchangani na kukupeleka kwa premier.
 
Hakuna haja ya kwenda personal. Mgonjwa wa Ukimwi anafikiri amejenga hoja, na hajaona kuwa amejibiwa kwa hoja yenye nguvu. Mara nyingi tunaweza kuangukia kwenye mtego wa "yaani haoni ufisadi wote huu" ambayo katika falsafa wanaita pseudo-obviousness. Ni wajibu wetu kumsaidia ndugu yetu kuona hoja za wapinzani na kuweza kumshawishi kwa hoja na nina uhakika akishawishiwa kwa hoja zenye nguvu zaidi basi anaweza kubadili mawazo (kama yuko open minded).

Mgonjwa wa Ukimwi, kama msimamo wako unatokana na ushawishi ulionao kuwa mambo yanayosemwa kuhusu serikali hayana ukweli na ya kuwa hoja za wapinzani hazina ukweli hata chembe, ni wajibu wako kutetea hadi dakika ya mwisho. Hata hivyo, kama unatetea kwa sababu hutaki kukubali kuwa kuna ufisadi kwenye serikali kama walivyoanisha wapinzani na licha ya preponderance of evidence, basi ni wazi hakuna lolote litakalosemwa linaloweza kukufanya ubadili msimamo wako.

Hata ni matumaini yangu kuwa uko open minded kuweza kushawishika kwa hoja zenye nguvu zaidi au kuwapa kina Dr. Slaa benefit of the doubt huku ukihamisha burded of proof kutoka kwao (kina slaa)) kwenda kwa waliotajwa. Are you?
 
1.
Mbona tunaongea kisichosemwa?

Katika posting yangu nimechambua ushahidi wa Dr Slaa ambao ameutoa dhidi ya watu aliowatuhumu. Na conclusion yangu ni kwamba tuhuma alizotoa ni mzito lakini ushahidi hafifu.

Mkuu heshima mbele, ushahidi unakuwa justified as hafifu pale tu wanaotuhumiwa wakijibu, au kesi nzima ikienda mahakamnani na kuthibitishwa na sheria kuwa ni hafifu, otherwise mimi na wewe ni watazamaji ambao hatuwezi kutoa conclusion bila kujua ukweli wote wa kesi. Kesi ya Clinton na Monica, ilipoanza tuliambiwa na democrats kuwa hakuna kesi ila Republicans ni wajinga na hawana ushaidi in the end rais wa USA kutoka democratic party, akawa impeached, kwangu hoja yako ingekuwa nzito iwapo tu at this moment tungekuwa tunaujadili ushaidi ambao umekuwa presented mahakamani tayari na pande zote mbili, kwa hiyo so far tuhuma zilizotolewa na Dr. Slaa ni nzito sana, na zinaendelea ku-stand mpaka pale waliotuhumiwa watakapokuja na ushaidi wao kujibu tuhuma hizi, then tuone pande mbili zikipigana katika ule mtindo wa advesarial system, ndipo tutaweza angalau kuanza ku-predict kuwa ushaidi upo au haupo, lakini sio katika hii stage ambayo so far ni siasa at work, sheria bado haijaanza kazi yake, maana kumbuka kuwa iwapo Dr. Slaa atashindwa kuthibitisha madai yake, ni halali kabisa kwa serikali kumshitaki on treason charges, hivi kweli Mkuu unataka kuniambia kuwa Dr. Slaa, na washauri wake, Chadema nzima as chama, wanasheria wake, wote hawakujua hili kabla ya kumruhusu kwenda public na tuhuma zake?

Katika uchambuzi wako sioni mahali ulipoziachambua evidence kisheria, nilichooona ni uchambuzi wako wa kimtaaani na in the process ninaona kiu yako ya ku-display your accademic cresidentials, yaani kutuonyehsa kwamba umesoma shule, lakini as far as tuhuma na evidence, no way hujazigusa na huzijui, unless wewe ni wakili wa waliotuhumiwa, au wewe ni mmoja wa watuhumiwa wenyewe!, otherwise wewe wala sisi wananchi hapa hatujachambua kitu as far as the Dr. Slaa's charges, ambazo ni complicated na ni white collar's one, na zinahitaji professionals na muda mwngi sana kuzichambua na kutoa conclusion, the matter of fact zinahitaji hela nyingi sana kuifanya hiyo kazi!

Ndio maana ninasema kuwa so far hizi charges hazijaingia kwenye sheria rasmi, kwa hiyo zina-hang kwenye political realms, sasa kama kweli unaelewa siasa unapaswa kuelewa kuwa reaction ya wananchi lazima iwe woooh! kumbe ndio maana rais wetu alisema kule Mbeya kuwa ana majina ya viongozi wala rushwa na wauza unga, huenda ndio hawa! Hiyo ni a natural political reaction ya a serious political annoucement, iliyotolewa na kiongozi wa upinzani na Mbunge wa taifa letu Dr. Slaaa.

Otherwise mimi na wewe at this moment hatuna qualifications zozote kisheria, kuzi-dismiss hizi charges as hazina ushahidi, I can understand ukisema kuwa ngoja utusubiri kama hii kesi itaenda mahakamani, ninaamini Dr. slaa hatashinda, lakini conclusion at this stage kuwa hakuna ushaidi, ni a cheap short cut tu ya kukwepa responsibility as mwananchi kwa sababu unazozijua mwenyewe, na it is fair kwangu na wanachi wengine humu forum ku-speculate kuwa inawezekana kuwa ni ushiriki katika ulaji huo wa rushwa, au kuwa ni mmoja wa watuhumiwa wenyewe!



2.
Nilitegemea wachangiaji wenzangu waonyeshe wapi ushahidi wa Dr Slaa una strength, badala yake wachangiaji wengi wanajaribu kushawishi kwamba Dr Slaa anayajuwa mengi zaidi ya aliyoyasema. Mimi sio mtaalamu wa ndoto wala sio mpiga ramri, hivyo basi nachambua kile kilichosemwa.

(b). Je Dr Slaa ni mjinga? Sidhani, ila kwa hili anastahili kuitwa mjinga machoni mwangu. Mwenye ushahidi wakutosha, mzalendo mpenda haki na maendeleo ya watu habembelezwi kuutoa, wala hakimbilii waandishi wa habari. Badala yake anakwenda mahakamani, na bungeni ikiwezekana. Dr Slaa hajafanya hivyo, badala yake ana-adaa wananchi wanaolia kwa kipindi kirefu juu ya rushwa.Kama Dr Slaa ana ushahidi mzito zaidi ya huo alioutoa (kama wachangiaji wanavyojaribu kutuongopea)anasubiri nini kuwashitaki? Vyama kama CUF, TLP, NCCR, viko wapi wakati vina kila ushahidi dhidi ya watuhumiwa? Hivi hii sio BINGO kwa wapinzani? Nadhani Dr Slaa ameamua kutupa makengeza tuzani ukungu ni moshi.

Great answer, kuwa wewe sio mtabiri wala mpiga ramli, na pia sio mwanasheria wa watuhumiwa, wala sio DCI, au Bwana Hosea. What Dr. Slaa knows au does not know, ni uamuzi wa sheria sio wewe na mimi kuhsu strength za charges za DR. Slaa, Dr. Slaa ameanzia kwenye jukwaa la siasa, na charges ambazo zinapaswa kupelekwa kwenye sheria, Kwa nini Dr. slaa ameamua kwenda kwenye mahakama ya public kwanza? Si rekodi inajisema yenyewe what happened to Mbunge Zitto! Ametoa ushaidi dhidi ya Karimagi, akafukuzwa bunge, sasa kwa nini Dr. Slaa asiamini kuwa akienda bungeni hatafukuzwa?

Lakini look at the double standards za chama changu CCM, Mzindakaya alipotoa ushahidi wa minofu ya samaki, akimtuhumu na rais wa CCM, kuhusika, Mzindakaya hakufukuzwa bunge, ila kumuokoa rais ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa CCM, ikaundwa tume haraka sana, mwenyekiti wake akiwa mbunge wa CCM Idd Simba, na Mbunge mwingine wa CCM, Masilingi akiwa katibu wa tume! Matokeo yakawa "..katika suala zima kuna harufu ya rushwa....na harufu inamhusu waziri tu na sio rais.....", wiki mbili baada ya kamati hiyo kutoa tamko hilo mwenyekiti wake Idd Simaba kawa waziri wa biashara na viwanda, huku Masilingi akiwa waziri wa utawala bora ofisi ya rais! Sasa with this kind of history Dr. Slaa angeenda mahakamani au bungeni na ushaidi wake? are you kidding me?

Again, strength au weakness ya hizi charges ni mahakama tu kwanza ndio yenye mamlaka kisheria, kuamua au baada ya watuhumiwa kujibu, maana ingekuwa uamuzi ni wetu wananchi kama wewe ulivyoamua, basi tunakuwa tuko Banana Republic, something I know kuwa we are not!

Hatuwezi kuamua tu baada ya kusoma upande mmoja wa Dr. Slaa kuwa hii kama ni kesi haina ushaidi, hicho kitendo kitaashiria one thing only, yaani arrogance!


3.
JF tumekuwa mstari wa mbele kuipiga vita rushwa, ila kwa mshangao naona tuna double standard. Amina Chifupa (R.I.P)alipokatazwa kutoa press conference, JF kulikuwa na movement ya kushinikiza aruhusiwe.


Oooh Yah! tulitaka Amina(RIP), ataje majina kama Dr. Slaa alivyofanya na ushaidi, ili as taifa tuamue kusuka au kunyoa? Katika vitabu vya historia ya siasa ya Tanzania, Dr. Slaa anakuwa ni Mtanzania wa kwanza kusimama kwenye public na kuwatuhumu viongozi wa juu wa serikali kuwa ni wahalifu, akiambatanisha na ushaidi, huku Muuungwana akisimama Mbeya na kusema kuwa anayo majina lakini bila ya kuyataja, na utakumbuka jinsi tulivyopiga kelele hapa kuwa Muungwana ayataje majina kama kweli anayo? Tukaishia kupewa Mahalu, ambayo pia haikuwa haba kuliko kutowataja kabisaa!

Mimi siiongelei JF, lkakini ninaamini kuwa tuna msimamo mzito na wa haki, usioangalia upande wowote, ingawa ni lazima nikubali kuwa sio wote hapa, lakini Mkuu Masatu, Mtanzania, Mswahili, na Mimi, Mugongo mugongo, tulisimama kidete kumdai Mheshimiwa Zitto, aje kujibu maswali hapa kuhusu tuhuma za uozo wake, wapambe wake wakaja juu na mpaka leo hajawahi kujibu, ila tu alikimbia bila kuaga, kwa hiyo si kweli kuwa hapa forum kuna macho mawili, halafu mkuu kama Mugongo mugongo, huwa ni very critical wa Zitto na Freeman, lakini leo hapa forum yeye ni loved na wakuuu wa pande zote mbili, kwa hiyo hoja za double standards hapa forum si zakweli, kuna some isolation ishus, ambazo sio serious kama zinavyokuzwa na wale ambao hoja zao zinashindwa kukubalika na wengi hapa, na ukweli ni kwamba huwa ni hoja hafifu!


4.
Sasa wachangiaji wengine humu wamenichekesha, wakisema kwamba wanataka viongozi walioshutumiwa wamjibu Dr Slaa. Nadhani JF tunataka kuona malumbano badala ya suluhisho. Hatufiki tunakokusudia. Ukimshika mwizi unampeleka kwa pilato, wala hauhitaji kumhoji kama kaiba au lah, mana kama kuna possibility kwamba hajaiba basi kuna possibility kwamba sio mwizi. Na mwizi ana haki ya kukaa kimya unapomuhoji na akasubiri kwenda kujibu kwa pilato. Hasipokujibu na ukaishia kutokwenda kwa pilato haina mana kaiba, hata kama utampiga. Kadhalika inanishangaza kuona kwamba JF tunalazimisha viongozi washutumiwa wamjibu Dr Slaa. Kana kwamba rushwa inapigwa vita kwa malumbano. By the way, nitawaona viongozi wa ccm wajinga endapo watajibu shutuma zenye ushahidi wa kuokotezea.

Viongozi wetu wakuu walipoitwa wasanii na magazeti flani bongo, serikali ilijibu kwa kutishia kuyafungia, kwa nini serikali ilijibu kwa niaba ya viongozi wakuu? WHY? waste their time huku wakijua kuwa viongozi wetu sio wasaniii? Kwa nini wananchi walipolalamika sana kuhusu Richmond, rais aliona umuhimu wa kuwajibu kwa kuaondoa waliokuwa kwenye wizara iliyohusika, kama kwa viongozi wetu kujibu wananchi ni kichekesho? Viongozi wa CCM, wanawajibika kujibu serious political accusations za ulaji rushwa zilizotolewa na kiongozi mwingine wa taifa kama wao tena kwenye public, kama shutuma zina ushahidi wa kuokoteza ni mahakama ndio ina umauzi, au Takuru kama ilivyofanya kwenye Richmond, ndio maana Gavana Balali ilibidi ajibu tuhuma dhidi yake, ina maana yeye ni kichekesho au? Wasipojibu, hawalazimishwi ndio maana ya demokrasia, lakini kama wanawaheshimu wananchi wanatakiwa kujibu mapigo tena hadharani, mimi simfahamu kiongozi yoyote duniani ambaye asingependa kuitumia opportunity hii kujisafisha na kujiweka sawa zaidi kisiasa!

Kwa kumaliza mkuu, ninasema kuwa hoja zako zitakuwa muhimu sana pale tu, kesi hiii ikienmda mahakamani na ushaidi ukaonekana baada ya kupingwa na pande zote mbili, mimi binafsi siwahukumu viongozi waliotuhumiwa, lakini ninawataka wajibu mapigo kama Mwalimu na Kawawa, walivyomjibu Kambona bila ya woga wala aibu, au kusubiri kuambiwa na chama, au kama majuzi Gavana Balali, alivyojibu mapigo bila ya woga, na hawa wajitokeze sasa ili tumalize hii ngwe ya kwanza ya public court, na baadaye tuhamie kwenye mahakama ya kweli, kama hakuna ushaidi basi Dr. Slaa afunguliwe kesi ya treason, anything less chama changu kitakuwa imechafuliwa, na indirectly kitakuwa kimekubali tuhuma hzio za Dr. Slaa,

Na hiyo ikitokea, jawabu litakuwa clear kuwa ni nani hasa anayechekesha!



Halafu mkuu angalia hii chini toka serikalini, yaani ndivyo hasa ninavyosema hapo juu:-

"SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amewasilisha vielelezo vya madai ya ufisadi vilivyotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (Chadema), kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili hatua zaidi za sheria zichukuliwe.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema ameamua kuzipeleka nyaraka hizo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa vile ndiye mshauri mkuu wa mambo yote ya sheria ndani ya serikali.

"Tumeamua kuzirejesha serikalini. Wao watajua watazifanyia nini hizo nyaraka," alisema Sitta.
Awali, Spika alisema angevipeleka vielelezo hivyo Polisi kwa hatua zaidi kutokana na utata wake.

Hata hivyo, baada ya kupokea ushauri wa kisheria kutoka kwa maofisa wa Bunge, ameamua kuvipeleka vielelezo hivyo serikalini vikafanyiwe kazi zaidi.

Ofisa mmoja wa Bunge aliliambia gazeti hili kuwa waliamua kumshauri spika wasipeleke vielelezo hivyo Polisi kwa kuhofia kujiingiza kufanya kazi zinazopaswa kufanywa na maofisa wa upelelezi wa polisi.

"Tulikuwa makini tusigeuke kufanya kazi za CID (wapelelezi wa polisi)," alisema ofisa huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa vile si msemaji wa ofisi hiyo.

Naye ofisa mwingine katika ofisi hiyo alisema kwa kuwa hoja ya Dk. Slaa haikuwasilishwa bungeni, ndiyo maana wameshauri nyaraka hizo zipelekwe serikalini.

"Sisi huwa tunafanyia kazi vitu ambavyo vimewasilishwa bungeni, lakini hoja hiyo haikuwasilishwa ndiyo maana tumeshauri viende kwa mwanasheria mkuu wa serikali," alisema ofisa huyo ambaye pia hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Kwa upande wake, Spika alisema nyaraka za Dk. Slaa zina utata na mchanganyiko wa vitu vingi, hivyo kwa kuvipeleka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu anaamini kuwa watajua cha kufanya.
"
 
Hapa naona tunaleteana hadithi za Michezo ya kuigiza ya kule kenya ya mtuhumiwa aliyeshikwa akiiba.

Mimi wakati nakuibia wewe ulikuwa wapi?

Nilikuwa nimelala.

Sasa ulijuaje nimekuibia kama ulikuwa umelala?

Mara baada ya kuiba ulishikwa na majirani ndipo nikaitwa kuja tammbua mali yangu.

Ni hayo tu MH
 
Ilibidi Clinton ashinde kesi ili kutoa mwanya wa Republican kushinda urais yeasr 2000.


Kibarua cha Clinton kingeota nyasi Makamu wa rais angekuwa rais na hivyo kufanya Republican wakione Kimbembe cha Zure 2000. Hawakuta hiyo itokee.
 
Vielelezo vya Dk. Slaa viko kwa Mwanasheria Mkuu

HabariLeo; Friday,September 21, 2007 @00:06

SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amewasilisha vielelezo vya madai ya ufisadi vilivyotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (Chadema), kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili hatua zaidi za sheria zichukuliwe.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema ameamua kuzipeleka nyaraka hizo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa vile ndiye mshauri mkuu wa mambo yote ya sheria ndani ya serikali.

"Tumeamua kuzirejesha serikalini. Wao watajua watazifanyia nini hizo nyaraka," alisema Sitta.

Awali, Spika alisema angevipeleka vielelezo hivyo Polisi kwa hatua zaidi kutokana na utata wake.

Hata hivyo, baada ya kupokea ushauri wa kisheria kutoka kwa maofisa wa Bunge, ameamua kuvipeleka vielelezo hivyo serikalini vikafanyiwe kazi zaidi.

Ofisa mmoja wa Bunge aliliambia gazeti hili kuwa waliamua kumshauri spika wasipeleke vielelezo hivyo Polisi kwa kuhofia kujiingiza kufanya kazi zinazopaswa kufanywa na maofisa wa upelelezi wa polisi.

"Tulikuwa makini tusigeuke kufanya kazi za CID (wapelelezi wa polisi)," alisema ofisa huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa vile si msemaji wa ofisi hiyo.

Naye ofisa mwingine katika ofisi hiyo alisema kwa kuwa hoja ya Dk. Slaa haikuwasilishwa bungeni, ndiyo maana wameshauri nyaraka hizo zipelekwe serikalini.

"Sisi huwa tunafanyia kazi vitu ambavyo vimewasilishwa bungeni, lakini hoja hiyo haikuwasilishwa ndiyo maana tumeshauri viende kwa mwanasheria mkuu wa serikali," alisema ofisa huyo ambaye pia hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Kwa upande wake, Spika alisema nyaraka za Dk. Slaa zina utata na mchanganyiko wa vitu vingi, hivyo kwa kuvipeleka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu anaamini kuwa watajua cha kufanya.

"Mwanasheria anaweza kufanya lolote kwani ndiye mshauri wa mambo yote ya sheria ya serikali, kwa hiyo usiniulize kwa nini sikuvipeleka Polisi kama nilivyoahidi," alisema Sitta.

Alisema kuna sheria za nchi zinazoelekeza namna ya kufanya iwapo kuna nyaraka za namna zinapofikishwa serikalini. "Hivyo sisi hatunazo tena hizo nyaraka," alisema.

Juhudi za kumtafuta Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika hazikufanikiwa na ilielezwa na katibu wake muhtasi kuwa alikuwa anahudhuria mkutano wa Baraza la Mawaziri.

Dk. Slaa alipanga kutoa hoja binafsi juu ya ubadhirifu ndani ya Benki Kuu (BoT) bungeni, lakini baadaye akaondoa hoja hiyo kwa madai kwamba ilikuwa inapigwa danadana.

Baada ya kuondoa hoja hiyo, aliahidi kwenda kwa wananchi kuwashitaki wale aliodai ni mafisadi wanaoitafuna nchi.

Alifanya hivyo kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita na kuwataja vigogo 10 wakiwamo viongozi wa kitaifa wa serikali, mawaziri, wanasheria na makatibu wakuu wa serikali na watendaji ndani ya BoT yenyewe na kiongozi wa CCM.

Jumanne wiki hii, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii), Kingunge Ngombale-Mwiru alisema serikali inasubiri kupata nyaraka za tuhuma zilizotolewa na mbunge huyo ili iweze kuzijibu.

Waziri alisema tuhuma hizo zilikuwa na lengo la kuwachafua viongozi wa serikali na CCM.

Ngombale-Mwiru aliwaambia wanahabari kuwa serikali ilikuwa haijapata nyaraka hizo.

Tangu kutolewa kwa kwa orodha hiyo na wapinzani, Ofisi ya Rais kwa kuwatumia mawaziri wake wawili, Philip Marmo (Utawala Bora) na Ngombale-Mwiru (Siasa) pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Aggrey Mwanri, wameshatoa matamko mbalimbali ikipinga madai hayo ya ufisadi kwa viongozi waliotajwa.

Mwanri amewataka wananchi kuwapuuza wapinzani kwa kauli hizo, kwani zina lengo la kuwachonganisha viongozi na wananchi.

Ngombale-Mwiru alisema kauli hizo za wapinzani zina lengo la kudhoofisha utendaji wa serikali na ni wivu kutokana na serikali kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya CCM.

Marmo kwa upande wake, alimtaka Dk. Slaa kuwasilisha ushahidi wake kwa mamlaka zinazohusika na uchunguzi wa ufisadi yaani Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), ambayo Dk. Slaa anadai hana imani nayo.


Chanzo: HabariLEO
 
Ni wivu tu na woga umewajaa. Hizo pesa na utajiri wote unaoibiwa na unaoendelea kuibiwa kila kukicha kule Tanzania SIYO MALI YENU NYIE WATU! Pesa mnazoweza kuziita zenu ni vile visenti mlivyonavyo benki na mifukoni mwa suruali zenu au pochini.

Watu acheni kujifanya eti "wazalendo" na mliojaa "uchungu na nchi".

Hakika mjichukulie kuwa "priviledged" kwa kupata wasaa wa kujadili na kukosoa "wheelings and dealings" za "political elites" Serikalini, CCM, na kwingineko, kwani hilo ndilo jambo la kwanza na la mwisho ambalo mnaweza kufanya.

Kama kweli mna usongo na nchi yenu basi wote msingebakia kupiga domo kutwa humu na mngechukua bunduki, mapanga, sime na mabomu na kuanza vita vya ukombozi kama walivyofanya Cono-Zaire na nchi kibao za Afrika ya magharibi.

Kalaga baho!
 
TANGOLD deal: The inside story
-Company said to be state-owned, but registered offshore in Mauritius Constitution includes some very interesting provisions

THISDAY REPORTER
Dodoma

MORE details are emerging about TANGOLD Limited, a supposedly government-owned enterprise which is understood to have been the beneficiary of a highly-questionable $13.34m (approx. 17bn/-) payment from the Bank of Tanzania (BoT) within the past year.

Investigations by THISDAY have now verified that TANGOLD Limited was registered as an offshore company in Port Louis, Mauritius in April 2005, with at least five top government functionaries listed as directors.

They included the BoT governor, Dr Daudi Ballali, and the Permanent Secretary in the Ministry of Finance, Gray Mgonja, who both still retain the same positions todate despite a government changeover in the interim.

Others were the then attorney-general Andrew Chenge; the then permanent secretary in the Ministry of Energy and Minerals, Patrick Rutabanzibwa; and the then permanent secretary in the Ministry of Livestock Development, Vincent Mrisho. All three company directors have since been transferred to other posts in the present fourth phase government.

In the case of Rutabanzibwa and Mrisho, they are now permanent secretaries in the Ministry of Water and the Prime Minister’s Office, respectively. As for Chenge, he is now Minister for Infrastructure Development.

According to the findings of earlier THISDAY investigations, the BoT paid $13.34m (approx. 17bn/-) into a bank account under the name of TANGOLD Limited, at the National Bank of Commerce Limited Corporate Branch in Dar es Salaam. This came on the heels of another BoT payment to a foreign bank account, amounting to over $118m (approx. 150bn/-), to liquidate a loan issued to the now-defunct Meremeta Gold Mine company.

The current Minister for Energy and Minerals, Nazir Karamagi, stated in parliament recently that all assets and liabilities of Meremeta Gold - including the Buhemba Gold Mine in Mara Region - had been transferred to TANGOLD Limited, which he described as ’’a new company wholly-owned by the Tanzanian Government.’’

The BoT is now understood to have dished out the 150bn/- as part of the process of ’liquidating’ the Meremeta Gold company, which nevertheless was in fact a joint venture project owned on a 50-50 basis by the Tanzanian government and a private South African firm going by the name of Trinnex (Pty) Limited.

Our latest investigations show that after its registration in Mauritius, TANGOLD Limited opened a branch in Dar es Salaam the following year and received a certificate of compliance from the Business Registration and Licensing Authority (BRELA) in February 2006.

But official records state the registered office address of the supposedly government-owned company continues to be Suite 520, Barkly Wharf, Le Caudan, Waterfront in Port Louis, Mauritius, while its stated capital is $100,000 (approx. 130m/-).

Furthermore, despite minister Karamagi’s claims that TANGOLD Limited is wholly government -owned, the company’s constitution has provisions that give its directors - Ballali, Chenge, Mgonja, Rutabanzibwa and Mrisho - the right to transfer their shares to family members.

According to a section in the TANGOLD Limited constitution directly pertaining to family transactions: ’’Any share may be transferred by a shareholder to, or to trustees for, the spouse, father, mother, child, grandchild, son-in-law or daughter-in-law of that shareholder; and any share of a deceased shareholder may be transferred by his executors or administrators to the spouse, father, mother, child, grandchild, son-in-law or daughter-in-law of the deceased shareholder.’’

It remains unclear why the ’government’ decided to register the company in Mauritius, and give the five officials complete liberty to transfer their individual ownerships of the firm to their wives, children, in-laws or other family members.

In another development, records also show that the London and Nasdaq stock exchange-listed RANDGOLD Resources - incorporated in the Channel Islands - announced in August 2005 that it had signed a joint venture agreement with the Tanzanian Government to develop new mineral deposits in the country.

According to the company’s media statement at the time, the deal was known as the ’’Tangold agreement’’ and related to a specific area of interest, this being ’’the Kiabakari Maji, which covers 2,692 square kilometres around the Buhemba mine but not the mine itself.’’
 
Back
Top Bottom