1.
Mbona tunaongea kisichosemwa?
Katika posting yangu nimechambua ushahidi wa Dr Slaa ambao ameutoa dhidi ya watu aliowatuhumu. Na conclusion yangu ni kwamba tuhuma alizotoa ni mzito lakini ushahidi hafifu.
Mkuu heshima mbele, ushahidi unakuwa justified as hafifu pale tu wanaotuhumiwa wakijibu, au kesi nzima ikienda mahakamnani na kuthibitishwa na sheria kuwa ni hafifu, otherwise mimi na wewe ni watazamaji ambao hatuwezi kutoa conclusion bila kujua ukweli wote wa kesi. Kesi ya Clinton na Monica, ilipoanza tuliambiwa na democrats kuwa hakuna kesi ila Republicans ni wajinga na hawana ushaidi in the end rais wa USA kutoka democratic party, akawa impeached, kwangu hoja yako ingekuwa nzito iwapo tu at this moment tungekuwa tunaujadili ushaidi ambao umekuwa presented mahakamani tayari na pande zote mbili, kwa hiyo so far tuhuma zilizotolewa na Dr. Slaa ni nzito sana, na zinaendelea ku-stand mpaka pale waliotuhumiwa watakapokuja na ushaidi wao kujibu tuhuma hizi, then tuone pande mbili zikipigana katika ule mtindo wa advesarial system, ndipo tutaweza angalau kuanza ku-predict kuwa ushaidi upo au haupo, lakini sio katika hii stage ambayo so far ni siasa at work, sheria bado haijaanza kazi yake, maana kumbuka kuwa iwapo Dr. Slaa atashindwa kuthibitisha madai yake, ni halali kabisa kwa serikali kumshitaki on treason charges, hivi kweli Mkuu unataka kuniambia kuwa Dr. Slaa, na washauri wake, Chadema nzima as chama, wanasheria wake, wote hawakujua hili kabla ya kumruhusu kwenda public na tuhuma zake?
Katika uchambuzi wako sioni mahali ulipoziachambua evidence kisheria, nilichooona ni uchambuzi wako wa kimtaaani na in the process ninaona kiu yako ya ku-display your accademic cresidentials, yaani kutuonyehsa kwamba umesoma shule, lakini as far as tuhuma na evidence, no way hujazigusa na huzijui, unless wewe ni wakili wa waliotuhumiwa, au wewe ni mmoja wa watuhumiwa wenyewe!, otherwise wewe wala sisi wananchi hapa hatujachambua kitu as far as the Dr. Slaa's charges, ambazo ni complicated na ni white collar's one, na zinahitaji professionals na muda mwngi sana kuzichambua na kutoa conclusion, the matter of fact zinahitaji hela nyingi sana kuifanya hiyo kazi!
Ndio maana ninasema kuwa so far hizi charges hazijaingia kwenye sheria rasmi, kwa hiyo zina-hang kwenye political realms, sasa kama kweli unaelewa siasa unapaswa kuelewa kuwa reaction ya wananchi lazima iwe woooh! kumbe ndio maana rais wetu alisema kule Mbeya kuwa ana majina ya viongozi wala rushwa na wauza unga, huenda ndio hawa! Hiyo ni a natural political reaction ya a serious political annoucement, iliyotolewa na kiongozi wa upinzani na Mbunge wa taifa letu Dr. Slaaa.
Otherwise mimi na wewe at this moment hatuna qualifications zozote kisheria, kuzi-dismiss hizi charges as hazina ushahidi, I can understand ukisema kuwa ngoja utusubiri kama hii kesi itaenda mahakamani, ninaamini Dr. slaa hatashinda, lakini conclusion at this stage kuwa hakuna ushaidi, ni a cheap short cut tu ya kukwepa responsibility as mwananchi kwa sababu unazozijua mwenyewe, na it is fair kwangu na wanachi wengine humu forum ku-speculate kuwa inawezekana kuwa ni ushiriki katika ulaji huo wa rushwa, au kuwa ni mmoja wa watuhumiwa wenyewe!
2.
Nilitegemea wachangiaji wenzangu waonyeshe wapi ushahidi wa Dr Slaa una strength, badala yake wachangiaji wengi wanajaribu kushawishi kwamba Dr Slaa anayajuwa mengi zaidi ya aliyoyasema. Mimi sio mtaalamu wa ndoto wala sio mpiga ramri, hivyo basi nachambua kile kilichosemwa.
(b). Je Dr Slaa ni mjinga? Sidhani, ila kwa hili anastahili kuitwa mjinga machoni mwangu. Mwenye ushahidi wakutosha, mzalendo mpenda haki na maendeleo ya watu habembelezwi kuutoa, wala hakimbilii waandishi wa habari. Badala yake anakwenda mahakamani, na bungeni ikiwezekana. Dr Slaa hajafanya hivyo, badala yake ana-adaa wananchi wanaolia kwa kipindi kirefu juu ya rushwa.Kama Dr Slaa ana ushahidi mzito zaidi ya huo alioutoa (kama wachangiaji wanavyojaribu kutuongopea)anasubiri nini kuwashitaki? Vyama kama CUF, TLP, NCCR, viko wapi wakati vina kila ushahidi dhidi ya watuhumiwa? Hivi hii sio BINGO kwa wapinzani? Nadhani Dr Slaa ameamua kutupa makengeza tuzani ukungu ni moshi.
Great answer, kuwa wewe sio mtabiri wala mpiga ramli, na pia sio mwanasheria wa watuhumiwa, wala sio DCI, au Bwana Hosea. What Dr. Slaa knows au does not know, ni uamuzi wa sheria sio wewe na mimi kuhsu strength za charges za DR. Slaa, Dr. Slaa ameanzia kwenye jukwaa la siasa, na charges ambazo zinapaswa kupelekwa kwenye sheria, Kwa nini Dr. slaa ameamua kwenda kwenye mahakama ya public kwanza? Si rekodi inajisema yenyewe what happened to Mbunge Zitto! Ametoa ushaidi dhidi ya Karimagi, akafukuzwa bunge, sasa kwa nini Dr. Slaa asiamini kuwa akienda bungeni hatafukuzwa?
Lakini look at the double standards za chama changu CCM, Mzindakaya alipotoa ushahidi wa minofu ya samaki, akimtuhumu na rais wa CCM, kuhusika, Mzindakaya hakufukuzwa bunge, ila kumuokoa rais ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa CCM, ikaundwa tume haraka sana, mwenyekiti wake akiwa mbunge wa CCM Idd Simba, na Mbunge mwingine wa CCM, Masilingi akiwa katibu wa tume! Matokeo yakawa "..katika suala zima kuna harufu ya rushwa....na harufu inamhusu waziri tu na sio rais.....", wiki mbili baada ya kamati hiyo kutoa tamko hilo mwenyekiti wake Idd Simaba kawa waziri wa biashara na viwanda, huku Masilingi akiwa waziri wa utawala bora ofisi ya rais! Sasa with this kind of history Dr. Slaa angeenda mahakamani au bungeni na ushaidi wake? are you kidding me?
Again, strength au weakness ya hizi charges ni mahakama tu kwanza ndio yenye mamlaka kisheria, kuamua au baada ya watuhumiwa kujibu, maana ingekuwa uamuzi ni wetu wananchi kama wewe ulivyoamua, basi tunakuwa tuko Banana Republic, something I know kuwa we are not!
Hatuwezi kuamua tu baada ya kusoma upande mmoja wa Dr. Slaa kuwa hii kama ni kesi haina ushaidi, hicho kitendo kitaashiria one thing only, yaani arrogance!
3.
JF tumekuwa mstari wa mbele kuipiga vita rushwa, ila kwa mshangao naona tuna double standard. Amina Chifupa (R.I.P)alipokatazwa kutoa press conference, JF kulikuwa na movement ya kushinikiza aruhusiwe.
Oooh Yah! tulitaka Amina(RIP), ataje majina kama Dr. Slaa alivyofanya na ushaidi, ili as taifa tuamue kusuka au kunyoa? Katika vitabu vya historia ya siasa ya Tanzania, Dr. Slaa anakuwa ni Mtanzania wa kwanza kusimama kwenye public na kuwatuhumu viongozi wa juu wa serikali kuwa ni wahalifu, akiambatanisha na ushaidi, huku Muuungwana akisimama Mbeya na kusema kuwa anayo majina lakini bila ya kuyataja, na utakumbuka jinsi tulivyopiga kelele hapa kuwa Muungwana ayataje majina kama kweli anayo? Tukaishia kupewa Mahalu, ambayo pia haikuwa haba kuliko kutowataja kabisaa!
Mimi siiongelei JF, lkakini ninaamini kuwa tuna msimamo mzito na wa haki, usioangalia upande wowote, ingawa ni lazima nikubali kuwa sio wote hapa, lakini Mkuu Masatu, Mtanzania, Mswahili, na Mimi, Mugongo mugongo, tulisimama kidete kumdai Mheshimiwa Zitto, aje kujibu maswali hapa kuhusu tuhuma za uozo wake, wapambe wake wakaja juu na mpaka leo hajawahi kujibu, ila tu alikimbia bila kuaga, kwa hiyo si kweli kuwa hapa forum kuna macho mawili, halafu mkuu kama Mugongo mugongo, huwa ni very critical wa Zitto na Freeman, lakini leo hapa forum yeye ni loved na wakuuu wa pande zote mbili, kwa hiyo hoja za double standards hapa forum si zakweli, kuna some isolation ishus, ambazo sio serious kama zinavyokuzwa na wale ambao hoja zao zinashindwa kukubalika na wengi hapa, na ukweli ni kwamba huwa ni hoja hafifu!
4.
Sasa wachangiaji wengine humu wamenichekesha, wakisema kwamba wanataka viongozi walioshutumiwa wamjibu Dr Slaa. Nadhani JF tunataka kuona malumbano badala ya suluhisho. Hatufiki tunakokusudia. Ukimshika mwizi unampeleka kwa pilato, wala hauhitaji kumhoji kama kaiba au lah, mana kama kuna possibility kwamba hajaiba basi kuna possibility kwamba sio mwizi. Na mwizi ana haki ya kukaa kimya unapomuhoji na akasubiri kwenda kujibu kwa pilato. Hasipokujibu na ukaishia kutokwenda kwa pilato haina mana kaiba, hata kama utampiga. Kadhalika inanishangaza kuona kwamba JF tunalazimisha viongozi washutumiwa wamjibu Dr Slaa. Kana kwamba rushwa inapigwa vita kwa malumbano. By the way, nitawaona viongozi wa ccm wajinga endapo watajibu shutuma zenye ushahidi wa kuokotezea.
Viongozi wetu wakuu walipoitwa wasanii na magazeti flani bongo, serikali ilijibu kwa kutishia kuyafungia, kwa nini serikali ilijibu kwa niaba ya viongozi wakuu? WHY? waste their time huku wakijua kuwa viongozi wetu sio wasaniii? Kwa nini wananchi walipolalamika sana kuhusu Richmond, rais aliona umuhimu wa kuwajibu kwa kuaondoa waliokuwa kwenye wizara iliyohusika, kama kwa viongozi wetu kujibu wananchi ni kichekesho? Viongozi wa CCM, wanawajibika kujibu serious political accusations za ulaji rushwa zilizotolewa na kiongozi mwingine wa taifa kama wao tena kwenye public, kama shutuma zina ushahidi wa kuokoteza ni mahakama ndio ina umauzi, au Takuru kama ilivyofanya kwenye Richmond, ndio maana Gavana Balali ilibidi ajibu tuhuma dhidi yake, ina maana yeye ni kichekesho au? Wasipojibu, hawalazimishwi ndio maana ya demokrasia, lakini kama wanawaheshimu wananchi wanatakiwa kujibu mapigo tena hadharani, mimi simfahamu kiongozi yoyote duniani ambaye asingependa kuitumia opportunity hii kujisafisha na kujiweka sawa zaidi kisiasa!
Kwa kumaliza mkuu, ninasema kuwa hoja zako zitakuwa muhimu sana pale tu, kesi hiii ikienmda mahakamani na ushaidi ukaonekana baada ya kupingwa na pande zote mbili, mimi binafsi siwahukumu viongozi waliotuhumiwa, lakini ninawataka wajibu mapigo kama Mwalimu na Kawawa, walivyomjibu Kambona bila ya woga wala aibu, au kusubiri kuambiwa na chama, au kama majuzi Gavana Balali, alivyojibu mapigo bila ya woga, na hawa wajitokeze sasa ili tumalize hii ngwe ya kwanza ya public court, na baadaye tuhamie kwenye mahakama ya kweli, kama hakuna ushaidi basi Dr. Slaa afunguliwe kesi ya treason, anything less chama changu kitakuwa imechafuliwa, na indirectly kitakuwa kimekubali tuhuma hzio za Dr. Slaa,
Na hiyo ikitokea, jawabu litakuwa clear kuwa ni nani hasa anayechekesha!
Halafu mkuu angalia hii chini toka serikalini, yaani ndivyo hasa ninavyosema hapo juu:-
"
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amewasilisha vielelezo vya madai ya ufisadi vilivyotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (Chadema), kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili hatua zaidi za sheria zichukuliwe.
Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema ameamua kuzipeleka nyaraka hizo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa vile ndiye mshauri mkuu wa mambo yote ya sheria ndani ya serikali.
"Tumeamua kuzirejesha serikalini. Wao watajua watazifanyia nini hizo nyaraka," alisema Sitta.
Awali, Spika alisema angevipeleka vielelezo hivyo Polisi kwa hatua zaidi kutokana na utata wake.
Hata hivyo, baada ya kupokea ushauri wa kisheria kutoka kwa maofisa wa Bunge, ameamua kuvipeleka vielelezo hivyo serikalini vikafanyiwe kazi zaidi.
Ofisa mmoja wa Bunge aliliambia gazeti hili kuwa waliamua kumshauri spika wasipeleke vielelezo hivyo Polisi kwa kuhofia kujiingiza kufanya kazi zinazopaswa kufanywa na maofisa wa upelelezi wa polisi.
"Tulikuwa makini tusigeuke kufanya kazi za CID (wapelelezi wa polisi)," alisema ofisa huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa vile si msemaji wa ofisi hiyo.
Naye ofisa mwingine katika ofisi hiyo alisema kwa kuwa hoja ya Dk. Slaa haikuwasilishwa bungeni, ndiyo maana wameshauri nyaraka hizo zipelekwe serikalini.
"Sisi huwa tunafanyia kazi vitu ambavyo vimewasilishwa bungeni, lakini hoja hiyo haikuwasilishwa ndiyo maana tumeshauri viende kwa mwanasheria mkuu wa serikali," alisema ofisa huyo ambaye pia hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Kwa upande wake, Spika alisema nyaraka za Dk. Slaa zina utata na mchanganyiko wa vitu vingi, hivyo kwa kuvipeleka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu anaamini kuwa watajua cha kufanya. "