List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Hii ni danganya toto haendi mtu mahakamani kwani wanajua wataumbuka wanajibu presha za nje tuu hapa.
 
Ukisoma kwa makini utaona kuwa wanatumia press ya aina moja kama ya karamagi jana kwani hii itawasaidia wasipishane naona hili wamekubaliana kwa pamoja.

Songa mbele kusambaza ujumbe mpaka kiwe jina langu, kwi kwi ,....
 
[
QUOTE=Jasusi;76951]Na Mugongo Mugongo kajificha wapi? Tora Bora?
[/QUOTE]

Mimi naaimini Mugongo ni gollira, anapigana nyuma ya pazia bega kwa bega na wana JF ndo maana hajatia neno hadi sasa,

Si unakumbuka yeye ndiye aliyeatuletea ile thread; Look at this stuff? Hawezi kutetea ufisadi huu.
 
Wale tuliko TZ, tuanze kampeni mahsusi ya kutumiana kwenye mail mambo haya ili ikiwezekana kila mtu asome na kujua kinachoendelea. Isiwe ni jambo la hapa JF pekee..lakini tuma kwa rafiki yeyote aliyeko kwenye address yako, INFORMATION IS POWER, na kama hamtajali, wale ambao hatuna kadi za vyama kama mimi hapa, tuanze kuwa wanachama hai wa CHADEMA🙂
 
Kama ni kweli wataenda mahakamani, ni hatua kubwa kwa nchi yetu ya Tanzania ambapo mafisadi hawa huwa wanacruise na maVX wakijua ni amani na utulivu hadi kifo kiwatenge na vyeo vyao. Kitendo cha angalau kudai kuwa wataenda mahakamani (JAPO NI MFA MAJI) ni ishara kubwa kuwa ZITTO, SLAA wamewashika panapo uvungu wa mapaja. na am sure hata tendo la ndoa kwa wake zao wiki hizi halipatikani 🙂
 
mie hii nchi yetu inanishangaza sana...,mtu anatuhumiw akwa mikashfa mingi kama hiyo lakini ndio kwanza anashtaki wanaomtuhumu ambao actuakly ni wananchi..,wakati nchi za watu(japan)..,tuhumu sensitive moja tu waziri anaamua kujiua kwa aibu na uzalendo wa kuwaaangusha wenzake na nchi nzima..,

wakati japan premier anaachia ngazi kwa kuwa na serikali isiyoungwa mkono..,wenzangu na sie ndio kwanza mkuu wetu aongeza kasi!!
 
Mimi nilikuwa na maswali kwa hawa mafisadi na bado sijapata majibu, hivi wanapokaa mezani kula chakula na familia zao huwa wanawaambia watoto wao kitu gani? Wanawafikiriaje WTZ wenzao? Wanayaonaje maisha yao? Je utakapofika wakati wa kuwaburuza mahakamani watamlaumu nani?

Huyu ndiye anatumiwa ku-facilitate malipo hewa, Je anafikiri atakwenda kujificha Canada, Australia, UK, SA, Uarabuni, etc wakati WTZ watakapokuwa wanadai kilicho chao.
 
Naamini Tanzania yenye neema bila chichiem inawezekana play your part
 
Wakuu wote hapo juu heshima mbele kazi nzuri. Taifa linatusubiri ili tuliokoe kutoka kwenye mikono ya mafisadi walafi wachache ambao bado wako kwenye usingizi wa pono wakati kulipambazuka zamani, wanafikiria Tanzania ni yao peke yao na familia zao.

Wazo - pale chini kuomba apology kama member atapata ujumbe kama huo zaidi ya mara mbili? Kwa kasi hii kuna uwezekano kabisa wa some MP's kupata more tha 50 e-mails na vile vile balozi zao tayari wana hard copy. Tupo wengi hapa.
 
nimeona alivyokuwa anaongea kupitia Channel Ten' ni utumbo mtupu
 

NO Dua...

US hakuna tatizo kama senator au member of parliament akipata message zaidi ya moja... sijui kuhusu UK.

Ukiangalia movements nyingi za US.... the more is always the better... wakipata messages over and over and over ndio wanajua kuwa issue ni serious.

Hakuna sababu ya ku-apologize kwa kutuma message zaidi ya moja.
 

Huyu kama ni kukimbia atakimbilia California, USA kwa sababu mke na watoto (teenagers) wake wawili wamekuwa kule karibia miaka kumi.

Wamekwenda shule ya msingi na secondary kama international students. Mke hafanyi kazi na pesa yote inatoka Bongo. Kwa mshahara gani wa serikali mtu afanye kazi Bongo halafu aendeshe maisha ya watu watatu California? Huyu mtu kama siyo jambazi ni nani?
 
Nitawawekea updated and edited "Resisting Corruption" ripoti ya Dr. Slaa in few minutes...
 
majina gani tena hayo? inamaana yale tuliyo tajiwa kule TMK ni feki? akina balali,chenge,Mkapa,Mkono,JK and the rest ni tofauti au mboni mwanichanganya? msije mkanitaja na mimi bure maana list inaendelea
 
Lol, kumbe hizi thread zimeunganishwa...nilidhani nimechemsha.
 
Nimeifanyia editing na kuiformat upya ripoti ya Dr. Slaa iliyowekwa hapa na "Mpaka Kieleweke". Sasa hivi iko kwenye format ya PDF na unaweza kuidownload na kuisambaza kwa urahisi. Admin.. kwa hekima yako ya Kispika unaweza kuiacha hapa kwa muda wowote ule ili watu wanaoitaka waipate kiurahisi. Pia nimeongeza nyaraka ya "orodha ya aibu" kama ilivyochambuliwa kwenye Mkutano kule Temeke na kufafanuliwa zaidi na Dr. Slaa kewnye mahojiano yangu naye kwenye KLH News.
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…