List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Mwanakijiji

Jamaa wameshikwa pabaya sasa wanahaha mwaka kabla ya kwisha tutaona mengi walifikiri wataendelea kutesa kwa zamu sasa pilipili waliyokuwa wanaililia inawawasha.
 
Rutabanzibwa aikana IPTL
Asema hahusiki kutia saini mkataba wake
Na Njumai Ngota (Uhuru)
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa ameruka kimanga suala la kampuni ya umeme ya IPTL na kusema hahusiki na utiaji saini wa mkataba huo.
"Madai ya Dk. Willibrod Slaa na wenzake dhidi yangu ni ya uzushi mtupu. Ninakanusha vikali tuhuma zote... wakati mkataba huo unatiwa saini mimi nilikuwa kamshina na sio katibu mkuu kwa hiyo sihusiki," alisema.
Alifafanua kuwa wakati mkataba huo unatiwa saini Mei 26, mwaka 1995, alikuwa Kamshina wa Nishati na Madini hakuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Dk. Slaa na wenzake katika mkutano walioufanya viwanja vya Mwembeyanga, Temeke mjini Dar es Salaam, walimtuhumu Rutabanzibwa kuwa anahusika na ufisadi kutokana na kuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini wakati mikataba waliyoita mibovu ya madini inasainiwa, hasa wa IPTL na kampuni ya Tangold.
Rutabanzibwa alisema wakati mkataba huo ukiwa mbioni kutiwa saini alipinga na kupendekeza ufanyiwe marekebisho jambo lililofanya gharama ya uendeshaji kupungua kwa asilimia 40.
Alisema Mei 11, mwaka 1997 ndipo alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini.
"Matamshi ya Dk. Slaa na wenzake yamenishangaza, yamenisikitisha na yamenihuzunisha sana," alisema na kumtaka kiongozi huyo na wenzake wamuombe radhi kwa kumsafisha jina lake.
Rutabanzibwa alisema anatarajia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Dk. Slaa na wenzake kwani wamemchafulia jina lake.
Alisema ili atendewe haki na kulinda heshima yake inayotokana na kuutumikia umma wa Watanzania kwa uadilifu kwa miaka 28, anafikiria kuchukua hatua hiyo.
Rutabanzibwa alisema anashauriana na wanasheria wake na kuwa tuhuma hizo, sio suala la kukurupuka hovyo.
Alisema katika kumfikisha mahakamani Dk. Slaa, atafanya hivyo mapema iwezekanavyo ingawa hakuweka wazi ni lini.
Akieleza jinsi alivyozipokea tuhuma hizo, Rutabanzibwa alisema bado linamuumiza kichwa kwa kuwa anamfahamu Dk. Slaa tangu akiwa Padri na hadi sasa hawajawahi kukosana naye.
Alisema alikuwa katika wizara hiyo kwa miaka tisa, ambapo mikataba minne ilitiwa saini, ukiwemo wa Songosongo.
Katibu Mkuu huo alifafanua kuwa hakuna kitu kinachopitishwa bila ya kupitia Kamati ya Mawaziri na mambo yote makubwa yanayohusu nchi yanasimamiwa kwa mujibu wa sheria.
Kuhusu kampuni ya Tangold, Rutabanzibwa alisema yeye ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya serikali inayosimamia hisa za serikali katika kampuni za madini.
Hata hivyo, hakufafanua kuhusu kuhusika kwake na tuhuma zinazotolewa na wapinzani dhidi ya kampuni hiyo.
Dk. Slaa aliongoza wenzake mbalimbali wa upinzani kutoa tuhuma dhidi ya baadhi ya viongozi na watu maarufu hapa nchini. Baadhi ya waliotuhumiwa wamejibu tuhuma hizo.
Miongoni mwao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Mbunge wa Musoma Mjini, Nimrod Mkono.
Mgonja na karamagi walisema watamfikisha Dk. Slaa, gazeti lililochapisha habari hizo na kampuni iliyohusika kuchapisha gazeti hilo mahakamani.
Mkono ambaye ni mmoja wa wabunge maarufu hapa nchini alipangu hoja mbalimbali zilizotolewa dhidi yake na kusema zote hazina ukweli.
Mkono hakuunga mkono wala kupinga suala la kuwapeleka mahakamani watu waliomhusisha na tuhuma hizo ambapo alisema hawana fedha za kumlipa, lakini bado anatafakari nini cha kufanya dhidi yao.
 
Ile fashion ya kutaka ushahidi sasa imepitwa na wakati. Fashion iliyo kwenye chati ni kwenda mahakamani. Hata Bwana Hosea simsikii tena akiuliza ushahidi, ukiona hivyo ujue hapo kuna ngoma nzito sana. Ingekuwa ngoma nyepesi Hosea angeishatoa tamko siku nyingi pale Idara ya Habari Maelezo kwamba anaomba ushahidi, ili kuweka msisitizo tungemsikia akisema "kama hakuna ushahidi hata ukienda mahakamani utapata ziro tena yenye masikio". Huyo ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kupambana na rushwa!
 
MKJJ: maneno mzaito hayo; nami naunga mkono hili wazo la maandamano ya kumuunga mkono huyu shujaa. Ngoja niongee na watu wengine tuone uwezekano wa hili. Kudos!
 
Wazo zuri tuangalie wenzetu nyumbani maana wao wako jikoni. Huu ni moto mkali sana.
 
Magazeti haya mengine nayo ... eti Mkono alipangua hoja mbalimbali zilizotolewa dhidi yake na kusema zote hazina ukweli. Kama hazina ukweli kwanini asitake jina lake lisafishwe hata kama hao waliomkashifu hawana fedha za kumlipa?
 
Hivi hawa watu wanadhani maneno ya Slaa kayatoa mbinguni?Hivi zile report za CAG atasema ziliandikwa na Slaa? Hivi hawa watu hawajui ni nini asili ama kiini cha hili saga? Hivi waliona ugumu gani kuunda Tume na huko landa wangaliweza ku spin nk ?
 
Ile orodha ya ndugu Slaa imesema kwenye nambari 5 kuwa ndugu Rutanziba amehusika na mkataba waIPTL sasa yeye Ruta anasema hakuwa wizarani wakati mkataba unasainiwa, tusaideni hapa ni nani anasema ukweli kama ndugu Slaa amekosea hii small detaili basi we'r in trouble ukweli ni upi ndugu zangu
 
Wasipofanya hivyo mapema as soon as JK amesharudi nyumbani.. watafungwa bao la ghafla..
 

Yeye mwenyewe kajikaanga kwa kuwa amekiri kwamba alikuwa Kamishna wa Nishati na Madini (hao ndiyo wataalam wenyewe) wakati mkataba wa IPTL unasainiwa na alishiriki kwenye review ambayo bado haikutoa unafuu wowote. Lakini akiruka kiunzi cha IPTL bado kuna kasheshe ya TANGOLD ambapo amekiri wazi kwamba alikuwa/ni mkurugenzi kwa ajili ya kulinda maslahi ya Taifa. Taifa gani ambalo lina shemeji/wifi/baba/mama/mjukuu/babu nk?
 
Keil,
Kuna ripoti ya Transparent International juu ya sakata la IPTL inaonyesha kuwa Rutabanzibwa alikuwa mstari wa mbele kupinga mkataba huo. Hapa nitampa benefit of doubt.
 
lowasa alitajwa ktk sakata la richimonduli kuwa alishinikiza kupewa tenda hao jamaa
 
Keli wewe unaongea tena habari ya kuruka kiunzi cha IPTL hapaswi kuruka kiunzi chochote moto kwa moto tu sasa ndio maana nasema ndugu Slaa anaweza kuwa legal troubble kwasasabu kwenye ile orodha amemtaja kama katibu mkuu wa nishati wakati wa mkataba wa IPTL hawa viongozi wetu hawana watu wa kuwafanyia reserch ya vitu vidogo kama hivi
 
Maandamano hayo yanatakiwa yafanyike weekend hii ... mwitikio wa watu wengi kama wakati ule wa Zitto utapeleka msg nzuri kwa serikali na wana CCM. Hata kama serikali ilikuwa na nia ya kumnyamazisha Dr. Slaa kwa njia za porini (mabavu au kutumia dola) itaona aibu kwa sababu watagundua kwamba hayuko peke yake. Wakati muafaka ni sasa ambapo bado serikali imechanganyikiwa na hawajui wafanye nini ili kuzima hizo tuhuma za ubadhirifu, na ndiyo maana watuhumiwa wenyewe bado wanajikanyaga kanyaga hata hawajui waseme nini. Chuma kikunje kingali cha moto ... tusisubiri kipoe itakuwa kazi ngumu kukikunja tena!
 
mzee kijiji hapo nimekufagilia kweli kweli hebu hao viongozi wa upinzani waombe kibali kwa tibaigana nasi tuko tiyari kuacha shughuli zetu zote. tumechoshwa na ushenzi wa aina hii tena ikibidi hata karamagi ashitakiwe na wananchi kwa kulidanganya bunge la ccm kuwa nchi ina maslahi na huo mkataba feki!
 
Aisee Mkijiji hili ni wazo zuri sana. Ubarikiwe

Kwani kufana kwa maandamano kutaweka picha halisi ya watu walivo amka na kuguswa na wizi wa mali zetu. Lakini pia kutaongeza pressure kwa serikali kujibu tuhuma si kukurupuka kama wanavo fanya sasa hivi kutishia kushitaki n.k! Nakama ulivo sema Kumtia moyo wa kusonga mbele Mpiganaji wetu.
 
Lakini muda sio tatizo? kwani kama maandamano ni vyema yafanyike wiki hii,ambayo ndio tupo ukingoni,kwa sababu Wiki ijayo Mkulu anarudi nyumbani na anaweza kurudi na strategies nyingine ambazo zitapunguza nguvu ya kashfa.Kashfa ina nguvu sasa kwa sababu Mkuu anakumbana nayo kila kona anayoyopita huku!Hawa wafadhili wapo makini sana na masuala ya Uongozi Bora!!!.Na hata hiyo kukimbilia mahakamani inatokana na pressure ya Mkuu kuwataka wajitetee.Ni mawazo yangu tu! lakini Maandamano ni Muhimu kuonyesha Mshikamano na kuchoshwa na viongozi Wabadhirifu.
 
This is exactly what needs to be DONE and it should be DON E VERY SOON. MwanaKijiji, you've always impressed me brother, this is yet another evidence of your never-ending resourcefulness.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…