FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 723
Kmawe Tanzania hakuna vita, tutaendelea kudai mambo yetu kwa amani!
Wananchi tupo sokoni tunauzwa, mtu anakupigia hesabu ya kuchukua Ikulu ili kutawala nchi kwa dola bilioni kadhaa fedha inanunua nchi,
Rais amekwisha jibu pale alipokuwa Arusha kwenye shughuli za kuzima mwenge. Aliwaasa vijana wasikubali kutumiwa na wanasiasa wenye tamaa na ikulu ambao wako tayari kufika huko hata kama itabidi kupanga miili ya watu waliouliwa kama ngazi. Sounds desperate !
Unajua mambo mengine ni utashi na hulka binafsi tuu.Unaweza kuta wapambe wake wa karibu wanampa magazeti yanayomsifu tuu na kumpa habari za kumpamba tuu.
Tena waweza kuta anajua wanozomewa ni wapinzani na si mawazili wake.
Angelikuwa serious ata nje asingeenda na ukiangalia majibu aliyotoa that day via cha ten inaonekana kwake yote hayo ni uzushi tuu na hayana ukweli ndani yake thats why ana confo ata la kuvizit nje.
Wanasema mzaha mzaha hutumbuka usaha.
Labda aliahidi maisha bora kwa kila mtanzania kwa kujua atapata pesa za misaada tele, labda hili ndilo linalomsukuma kila wakati kwenda nje, pengine kufuatilia zile ahadi alizopewa akiwa mambo ya nje maana amekiri kujiandaa kwa miaka kumi ili apate urais. Labda ndiyo maana hawezi kutuma mwakilishi hivyo lazima aende mwenyewe. kama hivyo ndivyo anatudhalilisha sana, sisi si omba omba.
Inasemekana ni mchumi, sina hakika, mimi si mchumi, lakini naweza kutambua kwa haraka kwamba inawezekana anachokitumia kwenda kuombaomba ni kikubwa kuliko tunachokipata. hata kama itakuwepo baki, basi magnitude yake hailisaidii taifa kusonga mbele kiuchumi.