List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania


Unasema kuwa huoni leader mwenye vision wakati the most you do here ni kumpigia debe mwizi na mkwepa kodi Edward Lowasa awe rais wa Tanzania?!
 

Sioni tatizo kwenye hili kwani rais akiwa chumbani na mkewe na wewe utataka kujua? Kama anakutana na Sinclair kama rafiki yake sioni ubaya. Ubaya ni kama mazungumzo hayo yatakuwa ya rushwa lakini kukutana na mtu yeyote behind closed doors ni right yake.
 
naona tunapoteza lengo. hivi mwanakijiji hebu tusaidie
slaa na mrema walieleza kwamba hayo majina yanatolewa
na chadema na tlp au uliwahoji kama slaa na mrema?
 
Mchambuzi anataka kuturudisha nyuma kuamini kwamba bila Nyerere Tanzania hakuna. sasa amekuja na falsafa ya bila CCM Tanzania hakuna. tunaposema ccm haiwezi kurekebishika mapema hivyo inatakiwa kuwa nje kwanza kwa muda tunazo sababu.

Zaidi ya miaka kumi iliyopita Kada namba mbili wakati huo Marehemu Kolimba alisema CCm imekosa Dira haina mwelekeo, leo hata baada ya muda huo kupita tunachokiona kinatisha zaidi kuliko wakati ule, na kwa mwendo huu Itatisha zaidi miaka mitano ijayo. Je mchambuzi unataka tuamini kwamba CCM itajirekebisha ikiwa bado viongozi wake wako madarakani?

UUngwana ni pamoja na kujiuzulu kunapokuwa na tuhuma dhidi yako. na kama JK anataka tuamini kwamba si mmoja wao, basi lazima achukue hatua haraka juu ya viongozi walio chini yake. Asipofanya hivyo, binafsi nitamuweka kwenye kundi la mafisadi tu. hata aimbe wimbo au ngonjera tam tamu, kwangu atakuwa fisadi tu.
 
Kuna Taarifa kuwa Wizara ya Utamaduni na Habari kwa kupitia watendaji wake wakuu na Idara ya Habari, walitoa Tamko jana kuwa "Majina yote yaliyotajwa"kwenye Mkutano wa Hadhara huko Mwembeyanga-Temeke yasichapishwe kwenye Magazeti ya Leo (Jumapili).

Sababu zilizotolewa na wahusika hao ni kwamba allegations za Dr Slaa dhidi ya aliowataja sio za kweli, Taratibu za kisheria zinafuatwa ili kumfikisha Mahakamani kwa kuchafua majina ya Viongozi kwa nia ya kuleta Uchochezi na vurugu!!.

Ni kweli kwamba Magazeti ya Leo huko Dar (isipokuwa Habari Leo) hayana majina ya waliotajwa na Dr Slaa.Gazeti la Habari leo ambalo lilikuwa na Habari hiyo na majina pia lilisimamishwa kutoka,baada ya nakala chache kutoka kimakosa.

Waungwana wenye Access ya kuandika Magazetini naomba majina yale yaandikwe kwenye magazeti ambayo hayana mahusiano ya karibu na serikali,Tunataka watanzania wajue na kuchuja maneno ya Dr Slaa.Vita imeanza na ni wazi hawa jamaa (watawala) watapindisha sheria ili kumtia adabu Dr.Slaa.Wanapanga strategies za kummaliza Dr. na kukanusha kwa nguvu zote allegations za vyama vya Upinzani.
 
 
Mchambuzi anataka kuturudisha nyuma kuamini kwamba bila Nyerere Tanzania hakuna. sasa amekuja na falsafa ya bila CCM Tanzania hakuna...

Huku ni kutoelewa nini ninachozungumza. sijui nikusaidieje hapo kwasababu nitaishia kurudia niliyoyasema ambayo kuna walioyapata vizuri.

Otherwise kitaifa, Tanzania ya kabla ya upinzani na tanzania ya leo haina tofauti yoyote kubwa. kwangu mimi ni kama hakuna upinzani. until upinzani wa maana uje na since hakuna independent candidates, nitabakia ccm kwasababu bado nina imani ccm ina baadhi ya viongozi ambao wakipewa nafasi wanaweza kupeleka nchi yetu mbele.
 
Mwalimu aliwahi kusema pale mlimani, kwamba Njia pekee ya kumsaidia mlalahoi (Masikini) ni kumsomeshea mtoto wake. Leo hizi za akina Slaa zinaitwa contemporary stategies, Hizi za mabilioni ya kikwete tuziiteje? hivi hakuna watoto wa maskini pale mlimani wamekosa mikopo? kwa nini hizi pesa zisiende huko?

Kama ni suala la contemporaly strategies basi hata tulionao madarakani wanahitaji usaidizi mkubwa maana mengine ndo hayo ya Mvua ya Lowassa n.k wengine mtanisaidia.

Labda pia nimmulize mchambuzi, lile Azimio la Songea la kuanzisha vuguvugu la kutetea rasli mali zetu nalo ni porojo? Je hiyo siyo long term strategy? je hakukuwa na haja ya sisi kuambiwa kwamba hawa ndiyo vinara wa uporaji wa rasli mali zetu ili move ipake kasi stahili? Mimi nadhani hapa tuache uvyama, bali tujadili pointi moja kwamba, je Hawa Slaa na wenzake hawakuwa na haki kama watanzania (si kama Chadema, Tlp au CUF) kulisema hili?. Na hata kama lina sura ya Uvyama kuna ubaya gani ili hali walioanzisha mchezo huo ni CCM wenyewe kule bungeni?

Nazidi kusisitiza, tumsaidie JK, njia anayokwenda si Sahihi. Slaa na wenzake si vichaa, wamechunguza wakajiridhisha, sasa ni jukumu letu kuwasaidia wafanye nini baada ya hapa.
 
Kwa wazee kama mimi, miaka ya mwanzoni ya tisini ilikuwa ni kama wakati huu watu walipokuwa wanasubiria majina ya wala rushwa.

Mtikila alisema ana list ya 'magabacholi' na palikuwa hapakaliki tanzania kwa sababu kila mtu alikuwa anataka kujua hayo magabacholi ni nani. kama zilivyo siasa za udaku, it all died. I am seeing the same process na inanifurahisha kuona kuna ushabiki wa hali ya juu on this matter, same way as it happened in ealry 1990s. Hizo ndizo siasa za upinzani.

Kwa wale ambao wanasubiria kina mrema, slaa wawatajie hiyo list, i wish you all the best in that endevour. tupo hapa na tutasoma tu hayo majina with no further actions zaidi ya ufahamu.
 
Mchambuzi

Kujaribu kukuelimisha ni sawa na kupoteza muda.Nimekueleza tangu mwanzo kwamba jaribu kuzichambua hoja za akina Slaa beyond hizo interests za kisiasa unazong'ang'ania.

Who would give a damn about CCM au CHADEMA,to mention only a few,kama nchi inakwenda vema.Kwa uzembe wako wa kufikiri,unaamini kwamba kwa vile yalosemwa na akina Mtikila hayakuleta vuguvugu lolote basi tukitambua kwamba flani anatafuna uchumi wetu basi tukae kimya.

MAPAMBANO YETU YA KUIKOMBOA TANZANIA HAYATAKWAMISHWA NA WAZEMBE WANAOFURAHIA KUNYANYASIKA.Who gives a hoot about sera za chama as long as nchi inatumia vema raslimali zake kwa ajili ya faida ya wote.

Hebu jaribu kuutumia vizuri ubongo wako na kuangalia hoja za Slaa kama za Mtanzania mwingine,na sio kiongozi wa chama cha upinzani.

As I said earlier,kuna watu wanasikia raha wanapokuwa na maumivu,lakini katika ishu hii nadhani ni kama ile "raha" ya funza ilhali kidole kinazidi kuoza.
 
Last edited by a moderator:
nina imani ccm ina baadhi ya viongozi ambao wakipewa nafasi wanaweza kupeleka nchi yetu mbele.

Tatizo langu bwana mchambuzi unapokuja na Majina ambayo ni yale yale yenye uoza. (Sina hakika kwa Mwandosya) lakini huyo mwingine unayemsema hana tofauti na JK. Ni kama tutakuwa tumehamisha pesa mfuko wa kulia kwenda kushoto. Tulimtegemea sana Jk kwamba na sisi tulikuwa tumempata Mwanawasa wa TZ, au Bingu wa TZ. but haya si yale tuliyoyatarajia hata kidogo, move zake si za kutupeleka kwenye maisha bora kwa kila mtanzania.

Imani yangu kwake itakuwa pale tu atakapowaondoa bila kuwaonea haya au kuwabadilishia kazi wale wote wanaokichafua chama, ikiwa ni pamoja na kukirudisha chama kwa wakulima na wafanyakazi si wafanya biashara.
 
Imani yangu kwake itakuwa pale tu atakapowaondoa bila kuwaonea haya au kuwabadilishia kazi wale wote wanaokichafua chama, ikiwa ni pamoja na kukirudisha chama kwa wakulima na wafanyakazi si wafanya biashara.

tatizo ni kwamba mimi bado ni mzito sana wa akili, sijafikia kumuona lowassa kwamba ndio tatizo la rushwa tanzania, nachoona ni mafanikio ya nyerere na sumu yake. sina nia mbaya na marehemu nyerere ila im questioning on why wengine aliona ni sawa tu wale nchi but wengine sio sawa. ni hapo ndipo naona kumekuwa na agenda on lowassa and it has worked very well.

Your point kuhusu kuirudisha nchi kuwa ya wakulima na wafanyakazi ni correct by 200%. hawa hawa wakulima na wafanyakazi ndio wenye uwezo wa kuleta mageuzi tanzania, working bega kwa bega na viongozi safi na wenye vision, whether ni wa ccm au upinzani.
 
Mchambuzi Yawezekana una imani kubwa sana na EL, but fanya home work kwa muda,tafuta habari zake, weka pembeni habari ya kufahamiana au mnatoka kumoja (mimi sijui) lakini fuatilia kwa karibu sana unaweza kupata ukweli.

Nijuavyo ni kwamba EL is a very smart guy, kwa hiyo ukitaka kuujua ukweli wake pia yakupasa nawe uwe smart. My comment inabaki kama mwanzo kwamba this is another JK
 

Una hoja nzuri sana saharavoice. Lakini pia nina swali - je wewe na wale ambao mnampinga lowassa, mmejua lini alikuwa na jk? hamkujua all along kwamba jk nyota yake imetokana na lowassa 1995 na pia hamkujua kwamba lowassa ndio kamfikisha jk kwenye urais wake wa leo as mtu aliyem introduce to the scene ya urais 1995 na pia as mtu aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya kumuandaa jk? jk anaweza kubadilika na kuachana na siasa za mtandao, uwezo na ujasiri huo anao lakini itam cost sana kwa sababu hajafika alipofika alipo leo peke yake. its either mtu unamkubali jk na lowassa as one au unawakataa wote, sio mmoja. thats the reality and its a fact.
 
Mimi natoa hoja based on experience of what has transpired since mrema miaka ile, mtikila all the way to ..

Unatoa hoja kulingana na pesa unazopewa na Rostam Azizi kwa ajili ya propaganda.... hakuna experience wala nini...

Kuna watu ni wana CCM hapa na wana experience na serikali na mambo ya siasa za bongo kuliko wewe na hicho cheo chako cha mshauri wa Lowasa wa. ......

upinzani una sera zipi in the context of rushwa na overall context ya maendeleo ya mkulima na mfanyakazi? mbona hakuna mtu hata mmoja anayejibu hili?

sisiemu ndio ina serikali na ndio ina wala rushwa wakiongoza na mwenyekiti wao Kikwete.... unachojaribu kuuliza au kuitofautisha na upinzani ambao ndio unatoa hizo siri kwa wananchi ni kipi?

Nani atategemea mzee wa propaganda za Rostam Azizi kama wewe utoe ushauri mzuri kwa maendeleo ya mkulima na mfanyakazi?

Kwa mwendo huu ndio maana binafsi naona nibaki ccm mpaka kimeguke au aje mpinzani mwingine wa kweli.

Ni tamaaa yako ya pesa za wizi ndizo zinakufanya ubakie CCM na wala usilaghai watu hapa.... usingekuwa unalipwa na mwizi na mkoloni Rostam Azizi na kufanya kazi for living kama mimi na hakika kwa sasa ungekuwa unaongea lugha tofauti...


Wewe endeleza tu ndoto zako za safari ndefu wakati malipo ni hapahapa duniani.... hata yasipotokea kwako yataifuata familia yako........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…