Heshima yako Mchambuzi...napenda unavyokata issues.
Hebu niangalie mtazamo wako unaoutetea wa hoja ya sera. Katika siasa zetu Bongo SERA zinachukua nafasi gani? watanzania wanaopiga kura kwa kuangalia sera ni asilimia ngapi ya wapiga kura wote. Je unaweza kuniambia wanakijiji pale Buzwagi ukiwaambia mzungu amepewa mgodi kwa njia zenye mashaka ndio maana hapa kijijini kwenu hakuna hospitali, shule, kituo cha polisi, barabara n.k watakuuliza sera ya chama chako ni ipi. Je kuna kweli hata hapo Dar ambako wapiga kura wenye elimu ni wengi zaidi wanajua kweli sera za CCM kulinganisha na za Chadema, TLP, CUF n.k?
Nimependa maswali yako ambayo kwa kweli ndio msingi wa matatizo yote hapa nyumbani. Mtanzania , maskini in particular lazima aelimishwe kwamba maendeleo yoyote ya maana yatatokana na sera, sio kwa kutatuliwa scandals za hapa na pale. Isitoshe, wabunge wengi wakipita kwenye hayo majimbo yenye migodi wataishia tu kusifika kwa hao wapiga kura kwamba wamei challenge serikali, but then what?
Tatizo ambalo tunalisahau ni kwamba Tanzania ni nchi ambayo haijapiganiwa toka kwa mkoloni. Mkoloni alitupa kwa amani na hii haikutokana na approach ya nyerere wala nani kupigania uhuru, handing over kwa amani ilikuja based on circumstances za wakati ule za koloni la Tanganyika. At the end of the day, hakuna kiongozi au generation ya uongozi ambayo inaweza sema ina uchungu na nchi ya tanzania kwa kuipigania na kuipokonya toka kwenye makucha ya wakoloni. Ndio maana viongozi wengi wanatafuna na hawaogopi. Nchi kama zimbabwe, angola, msumbiji, south afrika haziwezi fikia hatua ya rushwa kama tanzania sababu kuna walio pigania hizi nchi na either generations zao zimekaa pembeni zikitazama au zipo madarakani in one way or another na wanafanya kazi kwa uangalifu mkubwa. Kenya ni same ila ukiangalia kwa makini, wakikuyu wanapewa all the opportunities na hii ni kwa sababu ndio waliopigana kwenye mau mau. Ukiwachezea hawa wakikuyu kwa kuweka viongozi wengine na waanze kula na kuharibu nchi, kenya itaenda kubaya. So ukila nchi kenya lazima uhakikishe wakikuyu na wao hawaachi nyuma.
Tanzania hatuna kiongozi mwenye uchungu na tanzania zaidi ya nyerere ambae ni marehemu tayari au wale wafuasi wachache wa nyerere ambao na wao hawakutumia nafasi zao kula nchi. lakini kuna baadhi yao ambao wamejimegea hapa na pale hivi karibuni kwa sababu kustaafu na dignity doesnt help your well being katika maisha ya kustaafu. At most utageuka kuwa kicheko tu as mheshimiwa mwenye suruali yenye vitobo kwenye makalio.
Nchi yetu tuliipata kwa bei ndogo sana. Wenye uchungu ni generations za sasa ambazo either - uchungu wao unatokana na kwamba wao hawajapata nafasi ya kula au uchungu wao unatokana na exposure yao ya kuona wengine wanavyoendesha nchi kwa principles nzuri za good governance, so they wonder why nchi yao inachezewa. Na katika kundi hili la pili, wakipewa nafasi ya kula watatulia. At the end of the day, wazalendo wa kweli wa Tanzania ni wa kuhesabu.
Tanzania haitaweza kombolewa na any of the politicans wa sasa. Katika kipindi hiki cha mpito, kwa mtazamo wangu, ni bora hao kina mwandosya na wengine washikilie sababu ccm ukiondoa uchafu wa hapa na pale ni chama peke yake cha kweli.
Mbeleni, watanzania watakaoweza ikomboa Tanzania ni vijana wengine wenye uchungu na Tanzania kwa mfano baadhi ya wa humu JF, na wengineo wengi walio ndani na nje, wenye elimu zao, exposure zao na akili zao. It will need mapinduzi ya fikra na pia akili nzuri sana on how to educate watanzania maskini kuhusu haki zao za kimsingi katika elimu, afya, ajira n.k.
Hatua ikienda kuwa mbaya sana na ccm isipokuja na solution, nchi yetu inaweza ingia kwenye vita mbaya sana, mungu atuepushe kwa hili. Hivi vita havitakuwa vya kidini bali vya kisiasa - kati ya wana ccm na upinzani wa kweli utakaotokea. Na kawaida vita huwa vinaleta madhara makubwa kwa uchumi na jamii kwa ujumla lakini vikiisha huwa vinapeleka nchi kwenda kwenye maendeleo ya kweli. Kunakuwa na kuheshimiana na kuogopa kula mali ya nchi since ile dhana ya kupigania nchi inakuwa imeshajijenga. Angola, Rwanda, Msumbiji ni nchi zinazokuwa kwa kasi sana. Annual GDP growth zao hawa ni 8-9% a year. Hata marekani, uingereza etc walipitia such a phase na in the end kikaja to set the tone ya good governance. Wote hawa wanatuacha hawa huku sisi tunaangaika kutafuta majina ya wala rushwa.