Field Marshall ES,
Nashukuru kwamba bado tunaendelea kukata ishu huku tukielimishana/kueleweshana na kuipa jamii ya JF mitazamo mbali mbali ya jambo husika.
That said, hoja yako ya msingi kwamba mimi na wewe ni watazamaji tu na kwamba hatuwezi kutoa tathmini zetu isipokuwa mahakama ni hoja hafifu mno. Kama unavyosema ndivyo basi nakushauri uondoe neno DEBATE kwenye kamusi.
Kumladhi mzee mwenzangu, nashindwa kuamini kwamba ungeweza hata kutoa hoja kama hii...wakati kama sikosei wewe ni mwanzilishi wa neno KUKATA ISHU. Mimi nimekata ishu, nimechambua ushahidi alioutoa Dr Slaa nika conclude kwamba ushahidi wake ni hafifu, ni juu yako wewe kutoa uchambuzi wako (kama ukichagua kufanya hivyo) na kuja na conclusion yako kwamba ushahidi wa Dr Slaa ni mzito. Bado hujafanya hivyo na badala yake unashauri niwe mtazamaji na kusubiri mahakama. Hivi ulipobandika list ya Dr Slaa ulitegemea kwamba wasomaji wasome tu kama bibilia bila kutoa uchambuzi wao?
Hoja hujibiwa kwa hoja, kama MMKJJ anavyosema....ila naona mzee mwenzangu concept hii ndo kwanza unai-abuse. Badala ya kujibu hoja zangu kwa kueleza strength za ushahidi wa Dr Slaa, naona unarukia character assassination kwa kudai kwamba nimetoa uchambuzi kwa lengo la kuonyesha education credential zangu....I think Field Marshall ES you have more to offer to JF than this. You have my trust in your wisdom when it comes to JF but sometimes your lowest points reduce your JF wisdom to nothing.
Then katika posting yako unamwingiza Mugongo-Mugongo katika kujaribu kunifanya niamini kwamba Mugongo-Mugongo akikubali jambo basi na mimi nikubali. Naamini kwamba una utashi wa kujuwa kwamba Mugongo-mugongo ni mtu mwenye mawazo na msimamo wake unaojitegemea, kadhalika na mimi. JF hatushawishi watu kwa kutoa reference ya watu tuliofanikiwa kuwashawishi katika jambo fulani. Kesho naweza kukubaliana na wewe, keshokutwa nikapingana na wewe na kukubaliana na MMKJJ, wala sitasema kwamba kwakuwa MMKJJ alikubaliana nami basi ni budi wewe nawe pia ukubaliane nami.
All in all mzee mwenzangu, sikubaliani nawe kwamba niwe mtazamaji bila kutoa uchambuzi wa ushahidi wa Dr Slaa. Kama unapingana na uchambuzi wangu, it is very simple; leta wakwako. Na hilo tu ndilo litanishawishi vinginevyo. Kweli uchambuzi wangu ni wamitaani, kama ulivyodai, ila ni bora ukasema hivyo baada ya kutoa uchambuzi wa ofisini....nisaidie kwa kunipa uchambuzi unaouna ni wamaana. Sio kunitaka nizibe kinywa na nisubiri mahakama. Mahakama itatoa uamuzi wa mwisho, na it is possible ikaamua kwamba Dr Slaa ana ushahidi mzito, bado nitakuwa na uchambuzi wangu, na conclusion yangu, na wala haitakuwa mwisho wa debate.