List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Walisema kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala. Naona huyo mwenye nyumba sasa analala kwa starehe zaidi.
 
Mkono ashindwa kumshitaki Slaa

Hawa jamaa wanatucheze akili hawa,Sh&#% type zao.Mkono muda huu ningetegemea angekuwa mahamani.
Kuna mijamaa inakula pesa yetu kweli.

Nilitaka kutukana lakini ngoja kwanza nishushe hasira zangu.WE Mkono #!@#@$% zako......narudi
 
What an old fart this asshole has become.I feel sooooooooooo sorry for him.

You dont have to feel sorry for him,instead start feeling sorry for the starving walalahoi's who are in the majority in Bongo.I've always said that in Tz we need Gods intervention more than anywhere else in the world. So, lets hope it wont be long before we see God At Work.( the guy is HIV positive)
 
This was probably the worst thing to say among the millions of hungry and impoverished Tanzanians. Unajua, ingawa huyu jamaa amesoma na kubobea katika sheria, inaonekana ame-panic na ameshindwa kujua aseme nini ili kujitetea. You can't just blubber kwa watanzania kwamba benki yenu ya BoT inanilipa mamilioni ya saa moja wakati mtanzania wa kawaida kiasi hicho hakipati mpaka afanye kazi miaka 10. What an old fart this asshole has become.I feel sooooooooooo sorry for him.

Huyu Mkono ndio wale waliohudhulia shule hakuelimika.Jamaa mjinga huyu....next time nitalazimika kuhoji ukamilifu wa akili zake
 
Kesi inaendelea miaka 20? Na jamaa miaka yote hiyo anavuna hizo pesa?

Huyu jamaa ndio anaongoza kundi la mafisadi. Mtu kama huyu hawezi kwenda mahakamani maana mengi yataibuka.
 
Nchi hii inashangaza sana ... inakuwaje BoT isiwe na Company Secretary? Nina jamaa yangu ni wakili na anafanya kazi BoT, hao mawakili walioajiriwa na BoT kama wafanyakazi wa BoT na inasemekana wana Idara kabisa inayojitegemea, which means kuna zaidi ya lawyers 10, wanafanya kazi gani kiasi kwamba Mkono na kampuni yake waingie kwenye mkataba wa kuitetea BoT kwenye kesi zake.

Ina maana hao mawakili walio BoT hawako competent? Na kama hawako competent kwanini BoT iendelee kuwaweka kazini na hivyo kujiongezea wage bill unneccesarily!

Hivi Mkono ni nani mpaka afikie mahali pa kusema bila ya yeye hajui Tanzania ingekuwa wapi. Umaarufu aliopewa na Mkapa ndiyo unamfanya atambe kiasi cha kujiona yeye ni mtu muhimu sana nchini kuliko watu wengine? Kweli watu wakishatafuna hela ya walalahoi wanajisahau na kujiona wao ni miungu watu na kuwadharau watu wote.

Sijaona utetezi wowote kwenye hiyo press conference aliyoiita ofisini kwake. Sasa ndiyo tunazidi kupata ukweli zaidi kwamba yaliyosemwa humo ndani yana ukweli kwa asilimia kubwa na ndiyo maana wanaogopa kwenda mahakamani.

MgonjwaWaUkimwi tunaomba uje uwatetee maana wewe ulijaribu kuchambua dose ya Dr. Slaa lakini sikuona kama ulikuwa una hoja, sasa huu utetezi wa lawyer maarufu unazidi kutia shaka kwamba hilo dongo la Dr. Slaa ni la moto.

Ukiona wakili maarufu anaanza kutumia jina la Rais kama utetezi wa kuomba government intervention kwamba kwanini vyombo vya dola havijamshika Drr. Slaa basi huo ni ushahidi tosha kwamba Slaa kawashika sehemu nyeti.

Kwani kumwita Rais fisadi ni kosa? Na kama ni kweli ni fisadi tutumie jina gani? Kama Rais ameona kasingiziwa kwamba yeye ni fisadi, sheria ziko wazi aanze mbele mahakamani ili taasisi zinazohusika zikamshughulikie.
 
Pato la mtanzania (per capita income) ni dola 320 kwa mwaka Mkono analipwa dola 500 kwa saa. Duh hii ni soo.

Kweli ninavyojua kila wizara ina idara ya Sheria na kuna madirecto na hata BOT nadhani kuna idara ya sheria na mkuu wake ni Director of legal service. Kule kuna maadivocate wa serikali kwani kazi yao ni nini? Basi serikali ibinafsishe na idara zake za sheria kamailivyobinafsisha mashirika yake.

Cha kushangaza serikali huwa haishindi kesi hata sasa hivi ukizua isshue ukipeleka mahakamani utaishinda tuu? Tatizo ni nini? Inamaana mawakili wa serikali sio competent?

Hii kesi itaendelea kwa muda gani? ikiendelea miaka kumi naye ataendelea kula dola 500 kwa saa kwa hiyo miaka yote? Hadi sasa aseme amekula kiasi gani na serikali itasave kiasi gani kama ingeshindwa hiyo kesi na akishinda hiyo kesi serikali itapata fidia kiasi gani?
 
“Ndiyo… ninalipwa dola 500 kwa saa kila siku ya kazi na fedha hiyo nalipwa kwa saa nane,” alisema Mkono na kuongeza kuwa kesi hiyo inasimamiwa na wanasheria saba. Alifafanua kuwa watatu wapo hapa nchini, wawili wapo Ireland na wengine wawili wapo Jamhuri ya Watu wa Czech, ambako kesi hiyo inasikilizwa.

Inatia uchungu na inasikitisha, inamaana analipwa kwa kuisimamia hiyo kesi,means hizi ni extra money anazozipata on daily basis.

Mkono alisema wanaoishi nje ya nchi hulipwa dola 200 (karibu sh 260,000) kwa saa kila siku ya kazi kwa saa nane na kusisitiza kuwa hawezi kuiachia kesi hiyo, kama wanavyotaka wapinzani, hadi imalizike

Huyu jamaa ameshakolea na hela ya bure! ameshaonja utamu wa nyama ya mtu!

Alisema kesi hiyo ina mawakili wanane ambao kila mmoja analipwa Dola za Marekani 500 kwa saa na anafanya kazi saa nane ambapo kwa ujumla analipwa Dola 4,000.

Aliongeza kuwa kila wakili katika kesi hiyo analipwa Dola 1,000 kwa saa inapofanyika nje ya nchi ambapo malipo yanafikia Dola 8,000 kwa hizo saa.

Hawa waandishi wote walikuwepo kwenye hiyo interview? naona taarifa zinajichanganya kidogo.

Malipo mungu anayatoa hapa hapa duniani, mwanzo wa mabadiliko umeshawadia.
Ahsante 'father' kwa kuwaanika hadharani.
 
Ukiandika katika dola naona kama inapunguza ladha kwa watu ambao hawakusoma kama mimi. Kwa maneno mengine analipwa Sh.625,000/- kwa saa au Sh.5,000,000/- kwa siku.

Yeye naye kaitwa mwizi.Kama anaona JK ilifaa amkamate ili wamfungulie mashtaka, sasa yeye haoni akiwa kama mwana sheria asianze kumpeleka Slaa Mahakamani.
 
Walisema kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala. Naona huyo mwenye nyumba sasa analala kwa starehe zaidi.

Alale wapi na kila kukicha wanasongwa na skendo juu ya skendo. Mwaka huu ni wao na sijui kama watakuja kusahau katika uongozi wao. Wanajifanya wako "comfortable" lakini cha moto wanakiona japo hawasemi. Matokeo yake kila mtuhumiwa anakuja na version yake ya maelezo ya majibu ya tuhuma zake. Badala ya kudai haki za kuchafuliwa majina, wanaishia kusema hawaendi mahakamani ila wako tayari kwenda huko iwapo Dr. Slaa atatangulia.

Majibu haya yananikumbusha zama zile Sumaye akiwa amesongwa na tuhuma kibao za rushwa na Mchungaji Mtikila akamtuhumu kwamba yeye (Sumaye) ndiyo mla rushwa namba moja. Washirika waliotajwa na Mtikila walitishia kwenda mahakamani lakini hakuna hata mmoja aliyekwenda mahakamani mpaka BWM alipokuja kudai kwamba tuhuma hizo zilikuwa ni wivu wa kisiasa.

This time kwa kuwa Mkuu wa Kaya yuko ndani ya orodha ndiyo tunaanza kuwaona akina Kingunge wakisema ni wivu tu. Akina Mkono wanasema wapinzani wamemtukana Rais kwa kumuweka kwenye orodha ya aibu! Ukiona hivyo ujue wazi kwamba serikali sasa hailali usingizi angalau labda watapunguza ufisadi kwa kuwa sasa wananchi wameamka na wanaona nini kinaendelea. Wafadhili nao wameanza kupiga kelele kwamba serikali inabidi ijibu tuhuma za ufisadi! Sasa hapo usingizi wataupata wapi????
 
Hivi kuna mtu anaweza kupata english translation ya hizi tuhuma za Dr. Slaa? Kama itapatikana, watu waliopo Marekani tunaweza kuji mobilise ili kuomba marafiki na ndugu zetu wapiga kura wa kimarekani ili wawashawishi masenator na representatives wao ili wazuie misaada kwa Tanzania. Muungwana amekua akipewa sifa nyingi za bure tu na Wamarekani ambao hawajui ukweli kuhusu tuhuma dhidi ya serikali yake ya Mafisadi.

KAMA ENGLISH VERSION INAWEZA KUPATIKANA, TUNAOMBA IBANDIKWE HAPA ILI WATU TUANZE KAMPENI.


Ndugu wana JF
Nadhani anachosema Bw mwenzetu hapa sio kitu kidogo. Nadhani inawezekana kabisa kufanya hayo. Senetors wa US wakiandikiwa barua yenye akili wanaweza kufanya kitu. Nadhani hata kwa UK nadhani inawezekana kuwa hivyohivyo. Lazima kwenye bunge la Uingereza (Lords na Commons) na US (senate na House)wanaweza kufanya kitu. Nadhani hiyo inaweza kuwa step forward, badala ya JF kuwa baraza la porojo tu, inaweza kuwa na impact lazima wana JF wa UK na US hata brussels mnaweza kuwaaccess hawa watu. Let us make it.
 
Sijasema hoja za upizani hazina chembe ya ukweli. Nilichosema ni kwamba shutuma alizotoa Dr Slaa zina ushahidi hafifu. Put it differently, ushahidi alionao Dr Slaa ni dhaifu kwa shutuma alizotoa. Na nitaendelea kusema hivi hadi nitakapoona ushahidi mwingine.

Nina uhakika kwamba kama ushahidi alio nao Dr. Slaa ni dhaifu, hiki kilikuwa kipindi muafaka sana kummaliza (Dr Slaa) kisiasa. CCM na serikali yake wala wasingepoteza muda kumshughulikia kwa kuwa wangekuwa na uhakika wa ushindi wa chee.

Vielelezo vya kasheshe ya BoT alikuwa navyo Spika na serikali yake tangu mwezi August mwanzoni. Leo ni tarehe 22/9 na Dr. Slaa aliwaambia kwamba wasipojibu tuhuma zake mpaka kufikia 15/9 basi angeanika orodha ya majina ya mafisadi. Kilichofuata baada ya hiyo orodha ya mafisadi kutolewa kila mtuhumiwa amekuwa akijikanyaga kivyake na majibu ya tuhuma zao yameonekana kupwaya mbele ya wasomaji.

Sijawahi kusikia mwanasheria maarufu anasema kwamba eti hawezi kudai fidia kwa kuchafuliwa jina kwa kuwa mchafuaji wa jina hana fedha! Mkono ni mwanasheria maarufu ndani na nje ya Tanzania, hawezi kutoa kauli kama hiyo huku jina lake likiwa limechafuliwa. Njia pekee ya kujisafisha ingekuwa ni yeye kwenda mahakamani ili asije akaharibu biashara zake za ndani na nje ya nchi. Ukishaona statement kama hizo hiyo ni dalili tosha kwamba mambo si shwari na hizo tuhuma zina ukweli, na wala siyo kwamba tuhuma hizo zina ushahidi hafifu.

Kumwita mtu fisadi ina impact kubwa sana na hasa kama ni mwanasiasa, maana asipojisafisha ni kwamba anakubali kwamba yeye ni fisadi na inaweza kum-cost pindi ikifika kipindi cha uchaguzi. Sumaye alinyamazia tuhuma za rushwa na ilipofika wakati wa mchakato alipoulizwa alishindwa kujitetea and it was too late for him kuweza kujisafisha. Kwa hiyo Mkuu wangu MgonjwaUkimwi sina hakika na hiyo observation yako kuhusu ushahidi wa tuhuma za mafisadi!

La muhimu ni kwamba tusubiri mwisho wa mchezo, but it is premature ku-judge kwamba ushahidi wa Dr. Slaa ni hafifu.
 
Walisema kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala. Naona huyo mwenye nyumba sasa analala kwa starehe zaidi.

Mkuu Dua,

Heshima mbele, this time hiii ni ugly maana wakuu wa nje wameishaingilia kati, je serikali itaenda mahakamani?

Haiwezi, never! kwa sababu wanajua tayari kuwa alichokitoa Dr. Slaa ni chambo tu kuna aliyoficha, yanayosubiri mahakamani,

je wakienda mahakamani itakuwaje? itakuwa aibu ya wazi mbele ya dunia jinsi viongozi wetu wa juu watakavyochafuliwa, huku dunia nzima ikiangalia na kusikia! Big Politics, wanatakiwa kunyamaza na ndivyo watakavyofanya, kupiga kelele kidogo kwenye magazeti kama alivyofanya Mkono, na majukwaa ya siasa ya compromise kwenye CCM, basi!
 
Sijawahi kusikia mwanasheria maarufu anasema kwamba eti hawezi kudai fidia kwa kuchafuliwa jina kwa kuwa mchafuaji wa jina hana fedha! Mkono ni mwanasheria maarufu ndani na nje ya Tanzania, hawezi kutoa kauli kama hiyo huku jina lake likiwa limechafuliwa. Njia pekee ya kujisafisha ingekuwa ni yeye kwenda mahakamani ili asije akaharibu biashara zake za ndani na nje ya nchi. Ukishaona statement kama hizo hiyo ni dalili tosha kwamba mambo si shwari na hizo tuhuma zina ukweli, na wala siyo kwamba tuhuma hizo zina ushahidi hafifu.

I am with you on this!
 
Mkono ni mwanasheria maarufu ndani na nje ya Tanzania................


Kwa anayefahamu hivi Mkono aliwahi kufanya kesi gani nje ya Tanzania? Maana inavyoelekea atakuwa amefanya kesi ngumu nje ya Bongoland, dataz from JF.

Pengine ni maarufu kwa kuwasaidia mafisadi wa ndani na nje ya Tanzania katika kulifilisi taifa, kwa wakati mmoja ambapo yeye ni mbunge anayetunga sheria. TUENDELEE KUMWAMINI?
 
Mr Mkono. Mh Slaa kakuambia mkono wako umeshikilia kinyesi sasa kama wewe unaona vinginevyo tuthitishie sisi Watanzania, na si kutuambia kuwa unalipwa dola 500 kwa saa. Kutaka tu akamtwe Dr. Slaa hakutathibitisha kuwa nyie sio watuhumiwa wa ujangili.Bali mahakama ndo sehemu pekee itakayo thibitisha kuwa ayasemayo Dr. Slaa ni uongo.
 
Mkono anasema malipo aliyopewa siyo ya kesi peke yake, bali kuna kazi nyingine za BoT ambazo huwa anazifanya kulingana na makubaliano kati ya Kampuni yake na BoT. Je, anaweza kutuambia hizo kazi nyingine ni kazi gani???? Au na yeye mkataba wake ni wa siri kama ilivyo mikataba ya sirikali ya Tanzania na wawekezaji uchwara wetu?

On top of that, kama Mkono anafanya kazi za kisheria za BoT, na kama mchangiaji mmoja alivyosema kwamba kuna Kurugenzi ya Legal Services pale BoT, hiyo Kurugenzi au Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria anafanya kazi gani? Vijana walio chini yake wanafanya kazi gani?

Jibu la Mkono kwenye swala la malipo inaongeza maswali mengi zaidi ambayo majibu yake hatuna. Nadhani kila mtuhumiwa akija na version yake ya majibu ya tuhuma zake, badala ya kupunguza utata ndiyo wanazidi kulikoroga. Kaazi kubwa iko mwaka huu na masikio yetu yatasikia mengi na hata yale ambayo hatukutarajia kuyasikia nayo tutayasikia, ndo maana akina Mabere Marando na Maira nao wameingizwa na hatujui wameingiaje!!!! Lakini lengo ni kujisafisha na tuhuma ingawa ndiyo wanazidi kujisiliba matope badala ya kujiosha!!! Shame on them!
 
Hivi sheria zetu zinaruhusu Serikali kutumia mawakili binafsi?
 
Back
Top Bottom