List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Natumaini itaweza kuwafikia watu wengi.. hadi ikinirudia mimi mwenyewe nitajua kuwa ripoti hii imezungushwa.
 
Nimeifanyia editing na kuiformat upya ripoti ya Dr. Slaa iliyowekwa hapa na "Mpaka Kieleweke". Sasa hivi iko kwenye format ya PDF na unaweza kuidownload na kuisambaza kwa urahisi. Admin.. kwa hekima yako ya Kispika unaweza kuiacha hapa kwa muda wowote ule ili watu wanaoitaka waipate kiurahisi.

Maoni yangu tu; vipi mkiiweka na ile ya kiswahili hapo hapo kwenye pdf ya kiinglish zikae karibu ili kuturahisishia siye wenye matatizo yaliyo sambamba na ya akina Maimuna... ahsante.

SteveD.
 
Nadhani wengi wa wanaotandaa hawana tatizo la umaimuna. Nadhani hii ni kazi nzuri, kama na list of shame ingekuwa kwa kiingereza Ingekuwa ni vizuri sana ili iweze kusambazwa kwa wengine kama vile opposition MPs wa UK, na Senators wa US, kama alivyodokeza member mmoja, nadhani hiyo inaweza kusukuma gurudumu kwenyehatua nyingine.
 
MWafrika wa kike, nadhani mhabeshi naye ni mwafrka wa kike kwa hiyo hayuko mbali
 
katika hali inayoendelea kuwa tete na ya kutaharuki ,.katibu mkuu wa mudan mrefu wa wizara ya fedha ,gray mgonja amewaagiza wanasheria wake kumburuza dr.slaa mahakamani...

lakini hata hivyo kwa wanaomju MGONJA pamoja na uadilifu wake huko mahakamani itabidi naye aeleze inakuwaje familia yake na mke wake wanaishi huko FLORIDA ...califonia ..huku mke wake akiwa na "yule" mkenya akistarehe na akisimamia miradi mbali mbali kama apartments na kuishi maisha ya gharama.pesa za hayo majumba mrekani katoa wapi??? kwani huku hakuna ardhi.

naamini anapoelekea mahakamani asubiri kuumbuka zaidi.
 
duh,na hii ya FLORIDA ...califonia ,jamaa anamiliki majumba huko?
Kwa mshahra gani huo?kweli wabongo tunaliwa.
 
Naona wanatishia kujamba huku wakijua wazi kwamba wanaumwa ugonjwa wa kuhara ambapo mtu anaweza kuaibika mbele za watu. Nikisoma habari kwenye magazeti sioni kama kuna dalili za wao kwenda mahakamani, bali ni kujisafisha na ninaona wameamua kutumia same words kwenye statement zao. Nahisi imeandaliwa moja the wengine wanadesa tu huku wakiwa hawajui wanaenda kushitaki kwa misingi gani? Wanasema wanaenda wao kama watu binafsi, lakini press conference inafanyika kwenye ofisi zao za serikali na pia chini ya statement zao wameweka majina yao na title zao. Huo naona ni mkanganyiko wa kufa mtu!

Mgonja anasema yeye kama Katibu Mkuu atatetewa na serikali, hivi kweli ufanye ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha ukiwa na kofia ya serikali then usubiri serikali ikusafishe? Sijawahi kuona kioja kama hiki tangu nizaliwe! Sasa hapa ndiyo ninaanza kuamiani kwamba hawa watu wameambiwa wajisafishe na hawakuelewa wanatakiwa kusema nini na ndiyo maana wamekimbilia kusema vitu ambavyo vina utata.
 
Kigogo mwingine ambana Slaa
Stella Nyemenohi
HabariLeo; Thursday,September 27, 2007

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, jana alikuwa kiongozi wa pili kujitokeza na kutangaza kuwa anatarajia kufungua kesi dhidi ya Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (Chadema) kwa kumpaka matope kwa kumwita fisadi.

Uamuzi wa Mgonja umekuja siku moja baada ya Waziri wa Nishati ya Madini, Nazir Karamagi kuwaambia waandishi wa habari kuwa atamfungulia kesi Dk. Slaa sanjari na gazeti la MwanaHalisi na Kiwanda cha Printech kwa kuchapisha habari zenye kumchafua jina lake.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mgonja alisema tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Dk. Slaa ni suala la ushindani wa siasa ambalo ni pigo kubwa katika maisha yake na kwamba zimemwathiri kwa kumvunjia hadhi katika utumishi wake. "Tuhuma zimeniathiri. Hadhi yangu ni ya juu, hili ni pigo kubwa. Nimekaa katika sekta ya umma kwa miaka 33 sijawahi kupata kashfa. Bahati mbaya mimi siyo mwanasiasa, siwezi majukwaa," alisema Mgonja.

Akisisitiza kuwa uamuzi wa kumshtaki mwanasiasa huyo hautokani na shinikizo lolote. Mgonja alisema hakuweza kuchukua uamuzi huo mapema kwa kuwa alikuwa hajapata vielelezo muhimu vya kumwezesha kufanya hivyo.

Ingawa hakutaja siku ya kufungua kesi hiyo, Mgonja ambaye alisema anaifungua binafsi na siyo kwa wadhifa wake, alisema, "hatufuati maneno ya mabalozi. Kila mtu ana uhuru wake. Kama ningepata vielelezo mapema, ningeshazungumza mapema. Hivi sasa ninavyo na wanasheria wangu wako tayari."

Mgonja alisema itakapofika wakati wa kuzungumzia tuhuma hizo kama Katibu Mkuu, serikali ndiyo itakuwa katika nafasi ya kutoa tamko. Hata hivyo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa kwa upande wa uhusiano wa wafadhili, hususan katika utoaji wa misaada, tuhuma hizo za Dk. Slaa hazijaonyesha kuleta athari kwa kuwa hazina ukweli ndani yake.

Katika kujibu maswali ya waandishi, ingawa hakuelezea undani wa kile anachokwenda kudai mahakamani, alielezea kushangazwa kwake na tuhuma hizo kuelekezwa kwake ingawa wamepita makatibu wakuu mbalimbali katika wizara hiyo bila kurushiwa kashfa kama hizo. Alipohojiwa kuhusu mali anazomiliki, alisema, "namiliki mali kidogo sana".

Aliwaambia waandishi kuwa alishajaza fomu zinazoelezea mali zake na kuwashauri anayehitaji aende katika ofisi husika afuate utaratibu apewe taarifa hizo. Uamuzi wa Mgonja wa kumfungulia kesi, unatokana na kile alichosema kuwa ni matamshi ya Dk. Slaa aliyoyatoa Septemba 15, katika viwanja vya Mwembeyanga, wilayani Temeke kwa kumtuhumu hadharani kuwa ameshiriki katika vitendo vya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, vile vile Dk. Slaa alirudia kutoa shutuma hizo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Arusha Septemba 17.

Alisema gazeti la MwanaHalisi limekuwa likisambaza habari hizo za shutuma wakati huo huo Kiwanda cha Printech kinahusika kutokana na kuzichapisha. Katika hatua nyingine, ushirikiano wa vyama vya upinzani umetoa tamko lao kuhusiana na majibu ya serikali na watendaji wake kuhusu orodha ya wanaodai ni mafisadi kwa kugawa mkataba unaodaiwa ni wa uchimbaji madini Buzwagi.

Naibu Katibu Mkuu Chadema, Victor Kimesera alisema wameamua kuanika wazi kwa umma kupitia vyombo vya habari mkataba huo wanaodai ni wa uchimbaji wa madini ya Buzwagi kutoa nafasi kwa umma kujadili yaliyomo pamoja na mchakato uliosababisha mkataba huo.

"Tuko huru kuusambaza mkataba huu pande zote za Tanzania, ingawa ni maalumu kwa serikali kwa kuwa haukuwa na muhuri wa siri, kwa hiyo uko wazi kwa kila mtu kuuona," alisema na kuwakabidhi waandishi wa habari nakala ya mkataba huo jana.
 
mwanakijiji, fanya mambo mpaka kieleweke. nyani hao sisi tutakula nao sahani moja hata kama ni garama ya kuwakejeli na kuwazomea. solidality for ever....
 
Kuna watu wanajisajili hapo hapo wanataka ku-download hii attachment. Please subiri kidogo muwe approved ili mpakue hiyo attachment.

Thanks
 
Back
Top Bottom