DAVID PALMER
JF-Expert Member
- Jan 19, 2020
- 318
- 1,597
Halafu hua najiuliza kwa nini bidhaa nyingi za viwandanj kutoka Kenya ni bora zaidi kuliko za Tanzania? Kwa mfano sijaona sabuni ya kushindana na jamaa ya kenya, au BIG G original, tatizo kwa viwanda vya Tanzania ni nini? The same kwenye maziwa bidhaa za Brookside ni bora tena kwa sasa Lato milk ya Uganda inachapa mwendo ikiwa Asas , Tanga fresh zinajivuta tatizo ni commitment ya wenye viwanda, technolojia au ni nini ilihali malighafi Tanzania ni nyingi
Sababu ni gharama za uzalishaji wa hizo bidhaa ziko juu hapa bongo.So ili ulete ushindani wa bei sokon inabidi kupunguza ubora ili upate faida. Otherwise huweze shindana na bidhaa hata za malawi.
Bei ya mafuta, umeme na kodi za selikali ni sababu kadhaa zinazoongeza hizi gharama.
Mfano unakumbuka suala la ile sukari ya malawi.. ikabidi tutumie ubabe tusilete sukari kutoka nje. Kulinda viwanda vya ndani. Sababu price ya sukari yao ni ndogo afu quality.