Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naunga mkono hoja...Lissu ndio karata ya mwisho CDM waliyonayo kwenye kuleta mageuzi na imani tena kwa upinzani nchini.... Lissu ni kuwa mwenyekiti CDM ni zaidi ya Gia angani iliopigwa 2015.LISU ATARUDISHA ITIKADI/IMANI YA WATU KWA CHADEMA. CHADEMA MPENI UENYEKITI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Watanzania ni watu ambao huwaamini kama wanaweza kuishi bila kuonewa. Bila kutetemekea watawala. Bila kuwa machawa wa wenye navyo.
Watanzania wengi huamini kuonewa, kudhulumiwa na Wakubwa ni HAKI yao.
Watanzania wengi wamejenga kasumba kuwa ukiwa na cheo unahaki ya kufanya chochote kwa wasionavyo.
Watanzania wengi ni conservative au tuseme wamedumaa na hawahitaji mabadiliko mazuri zaidi.
Watanzania wengi hawamaani katika utu, HAKI, ndio maana hawawezi kupigania HAKI Zao hata kwa kusema tuu.
Watanzania ndio watu pekee ambao hata wewe hapo unaweza jifanya Usalama wa taifa ukaenda kijiwe chochote ukamchukua mtu yeyote au ukampiga makofi mtu kwa kisingizio cha Usalama wa taifa na Watanzania wakakuangalia tuu
Watanzania wengi ndio watu pekee ambao unaweza kuwaweka benchi wakasugua wakisubiri huduma ya hospital au huduma yoyote na wasiwe kuhoji.
Tundu Antipas Lisu tunamhitaji kwa wakati huu ili kubusti akili za Watanzania. Kuamsha Ari.
Kung'arisha fikra,
Kuchochea Moyo wa kupenda haki na kuipigania.
Kuufanya ukweli uwe mwamvuli wa wananchi.
Kuondoa uchawa na Tabia mbaya za kujipendekeza.
Moja ya dalili ya ukosefu wa HAKI katika jamii ni uchawa na kujipendekeza.
Uchawa na HAKI havikai pamoja.
Uchawa na ukweli havikai pamoja.
Mtu yeyote anayejitambulisha na kujionyesha. kama Chawa hawezi kuwa mtenda HAKI.
LISU atarejesha imani ya watu kwenye vyama vya upinzani. Kama ilivyokuwa 2010-2015.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Dar es salaam
Umenena vema mkuu, yaani umemaliza yote. Maccm yamehamaki sana kuona Lissu ametangaza nia .Haa😄😄haa...
Wewe MamaSamia2025 uko serious kweli...?
Mmemnanga sana Freeman Mbowe kuwa mng'ang'ania madaraka...
Wengine wakasema CHADEMA hakuna succession plan ktk mfumo wa uongozi wao...
Leo Freeman Mbowe anataka kumwachia Tundu Lissu, wewe ukiwa unawakilisha Chawa na wana CCM wenzako unaonesha kumpenda na kumhurumia tena? Really...?
Hakuna shaka kuwa kelele za Chawa wa CCM na allies wao waliomo ndani ya CHADEMA kwenyewe, the whole plan ilikuwa ni ku - frustrate Freeman Mbowe, ajione hafai, wanachama wamwone hafai, mla ruzuku za chama tu, aondoke kisha CCM na serikali yake waweke pandikizi na iwe mwanzo wa kudhoofika kisha kufa au kulala kwa CHADEMA....
The plan has failed spectacularly. Tundu Lissu ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA....
Kuibuka kwa Tundu Lissu (ambaye obvious atashinda uenyekiti akigombea na yeyote hata kama Samia atahamia CHADEMA na kugombea naye), hili limewashitua CCM kwa sababu huyu mtu ni moto zaidi kuliko Freeman Mbowe...
Kila la kheri CHADEMA na kila la kheri Tundu Lissu. Tunakujua wewe ni mtu makini, mwenye msimamo usiyeyumbishwa, mpenda haki, mchukia rushwa na ufisadi, mwadilifu na mtu mwenye ufahamu na maarifa mengi sana ambayo ni silaha muhimu sana ktk ulimwengu wa uovu na uonevu huu tuishio...
..demokrasia ina sura nyingi kulingana na mazingira ya mahali husika na malengo kadiri mambo yanavyobadilika..usikariri demokrasia km dogma kijana!Nawe kama ni muumini wa demokrasia tungekuomba umwambie Mzee apishe wengine .Miaka ishirini ya kukunja ngumi haijaleta matokeo tarajia hata kidogo.
Mwaka 2020 alipohojiwa ana maoni gani kama Lisu akishinda nafasi ya Urais, alisema, "Lisu, sina shaka kuwa ana uwezo wa kuwa Rais, anaweza. Ila Lisu akiwa Rais, tutalazimika kujifunza kufuata sheria"LISU ATARUDISHA ITIKADI/IMANI YA WATU KWA CHADEMA. CHADEMA MPENI UENYEKITI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Watanzania ni watu ambao huwaamini kama wanaweza kuishi bila kuonewa. Bila kutetemekea watawala. Bila kuwa machawa wa wenye navyo.
Watanzania wengi huamini kuonewa, kudhulumiwa na Wakubwa ni HAKI yao.
Watanzania wengi wamejenga kasumba kuwa ukiwa na cheo unahaki ya kufanya chochote kwa wasionavyo.
Watanzania wengi ni conservative au tuseme wamedumaa na hawahitaji mabadiliko mazuri zaidi.
Watanzania wengi hawamaani katika utu, HAKI, ndio maana hawawezi kupigania HAKI Zao hata kwa kusema tuu.
Watanzania ndio watu pekee ambao hata wewe hapo unaweza jifanya Usalama wa taifa ukaenda kijiwe chochote ukamchukua mtu yeyote au ukampiga makofi mtu kwa kisingizio cha Usalama wa taifa na Watanzania wakakuangalia tuu
Watanzania wengi ndio watu pekee ambao unaweza kuwaweka benchi wakasugua wakisubiri huduma ya hospital au huduma yoyote na wasiwe kuhoji.
Tundu Antipas Lisu tunamhitaji kwa wakati huu ili kubusti akili za Watanzania. Kuamsha Ari.
Kung'arisha fikra,
Kuchochea Moyo wa kupenda haki na kuipigania.
Kuufanya ukweli uwe mwamvuli wa wananchi.
Kuondoa uchawa na Tabia mbaya za kujipendekeza.
Moja ya dalili ya ukosefu wa HAKI katika jamii ni uchawa na kujipendekeza.
Uchawa na HAKI havikai pamoja.
Uchawa na ukweli havikai pamoja.
Mtu yeyote anayejitambulisha na kujionyesha. kama Chawa hawezi kuwa mtenda HAKI.
LISU atarejesha imani ya watu kwenye vyama vya upinzani. Kama ilivyokuwa 2010-2015.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Dar es salaam
Mngekuwa chama rafiki mngekuwa mnawateka na kuwaua?Lissu ni adui wa demokrasia na kirusi ndani ya chama rafiki CHADEMA. Sisi wanaCCM tunasikitishwa na vurugu zinazofanywa na Lissu. Mbowe awe tu mtulivu atashinda hii vita.
Mwaka 2020 alipohojiwa ana maoni gani kama Lisu akishinda nafasi ya Urais, alisema, "Lisu, sina shaka kuwa ana uwezo wa kuwa Rais, anaweza. Ila Lisu akiwa Rais, tutalazimika kujifunza kufuata sheria"
Hoja za "Tribalism" kwenye CHADEMA ni hoja dhaifu.
Ifike hatua mbowe nae aachie ngazi.
Ccm wanampigia upatu mbowe maana wanajua ni kibaraka .
Ccm wanamuogopa lissu wanajua ni mwamba kwelikweli .
Chawa wakale polisi?
Subiri matusi toka kwa wachagga
Kuna tatizo la watu kuchanganya chama na watu, CCM kama CCM hainaKilaaniwe Chama Cha Mashetani, CCM.
Km kweli unaamini unayosema na unamtakia mema Lissu ungemwambia watanzania hawaamini ktk siasa za confrotational na hivyo nafasi nzuri kwake ndani ya chama ni kuwa mwalimu wa itikadi, chama kianzishe madarasa ya itikadi hasa kwa viongozi na Lissu atumike kufundisha itikadi ya chama..atakisaidia sana chama chake kuliko akiwa Mwenyekiti wa chama na atakuwa na muda wa kuwa na utulivu ili arudi kwenye hali ya mwanzo kisaikolojia na hata apate muda kuamua familia yake irejee kuishi Tanzania tena.
Duru zinasema Lisu akishinda uenyekiti Pascal Mayalla analamba nafasi ya juu ya uongozi wa chadema.
Hii habari niliipata kwa Kaka yake Lisu.
Lissu ni adui wa demokrasia na kirusi ndani ya chama rafiki CHADEMA. Sisi wanaCCM tunasikitishwa na vurugu zinazofanywa na Lissu. Mbowe awe tu mtulivu atashinda hii vita.
..na si pahala pote confrotational approach ilishinda.Ukiwa Msema kweli na mpigania HAKI lazima siasa zako ziwe za migogoro.
Huwezi kupigania ukweli na HAKI alafu hutaki confrontation
Lissu mnamuogopa sana.Lissu ni adui wa demokrasia na kirusi ndani ya chama rafiki CHADEMA. Sisi wanaCCM tunasikitishwa na vurugu zinazofanywa na Lissu. Mbowe awe tu mtulivu atashinda hii vita.
CCM ndio inayong'ang'aniza utawala huu wa Kiimla.Kuna tatizo la watu kuchanganya chama na watu, CCM kama CCM haina
Tatizo, ila ni kweli kuna wana CCM wachache ambao kweli ni mashetani lakini wana CCM wengi ni malaika na kwenye upinzani mashetani pia wapo!.
Nimeandika sana humu mambo ya malaika na shetani
P