Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

ndugu wanajamvi... nimepita maeneo ya mwananyamala karibu na hospitali.. ile njia unayopita kama unataka kutokea kinondoni biafra NIMEKUTA MAGARI YA JESHI ZAIDI YA 10... Nashindwa kuelewa kwa nini yamejazana maeneo hayo..
 
NEC hawana macho na masikio kwa Lowassa na JK kupiga kampeni siku ya uchaguzi?
 
Superman na wengine wote Ahsanteni sana na Mubarikiwe sana kwa kutuhabarisha!
 
Wanajamvi naomba kuuliza matokeo yanatazamiwa kutangazwa saa ngapi?
 
ndugu wanajamvi... nimepita maeneo ya mwananyamala karibu na hospitali.. ile njia unayopita kama unataka kutokea kinondoni biafra NIMEKUTA MAGARI YA JESHI ZAIDI YA 10... Nashindwa kuelewa kwa nini yamejazana maeneo hayo..

Mkuu ni magari ya namna gani ya kawaida au maloro ya kivita yale? walikuwa na silaha?

Huenda wako standby tu in case of vurugu kama walivyotahadharisha huko nyuma.
 
Wanajamvi naomba kuuliza matokeo yanatazamiwa kutangazwa saa ngapi?

Mkuu, upigaji wa Kura unamalizika rasmi saa 12 ambapo baada ya hapo kura zinaanza kuhesabiwa vituoni kabla ya masanduku kuondolewa na kisha kupelekwa kwenye kituo kikuu kinachofuata.
 
TBC: Wanaripoti kua kuna mtu kakamatwa Magomeni mchana huu ana shahada tano, ameshakamatwa na yuko polisi... wenye zaidi???
 
Huko nyuma niliripoti kuwa, KUNA askari wamekusanywa huko Kurasini Kwa ajili ya "kutumika kwenye uchaguzi"
 
TBC: Wanaripoti kua kuna mtu kakamatwa Magomeni mchana huu ana shahada tano, ameshakamatwa na yuko polisi... wenye zaidi???

Du! Ipo kazi.

Mwanza inaripotiwa kuwa vijana wamejitokeza kwa maelfu kupiga kura na wamejitokeza alfajiri na mapema.
 
Huyu wa MAGOMENI jamani mkumbuke ni tofauti na yule MOSHI japo taarifa zote zimepatikana hapa TBC!!!! Hivi mmeenda kula lakini? Morogoro kwema, sumbawanga kwema, monduli nako ni kwema haya wengine mnasemaje?
 
Mkuu ni magari ya namna gani ya kawaida au maloro ya kivita yale? walikuwa na silaha?

Huenda wako standby tu in case of vurugu kama walivyotahadharisha huko nyuma.

superman, ni yale malori makubwa ya kijeshi.. ila kwa kuangalia yalikuwa hayana wanajeshi!!
 
TBC: Wanaripoti kua kuna mtu kakamatwa Magomeni mchana huu ana shahada tano, ameshakamatwa na yuko polisi... wenye zaidi???

Huenda hawa ndiyo walioripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa wananunua shada za kupigia kura.
 
Mwache aenze government. Ni haki yake. Nafikiri mwaka huu wataenda wengi sana
 
Unajua NEC ndo hao hao. We acha tu maana Mungu atawaaibisha leo
 
Huko Kagera, wamesimama kidete na kukaa mbali kidogo ya kituo baada ya kupiga kura kwa mdai kuwa 2005 wageni wengi walipiga kura lakini sasa hawakubali na wanataka wahakikishe hawafanyi hivyo. Pamoja na mgombea udiwani wa CCM kuwaomba wanausalama wawaondoe lakini haikusaidia.
 
Ndo naondoka MLIMANI-UDSM, hali ni shwari na thanks GOD turnup ya wanafunzi imekua kubwa sana, ule ujanja wao wa kuwaondoa chuo haujafanikiwa kivile
 
Na aende salama, tumechoka kudanganywa, wanatumia madaraka tuliyowapa sisi wananchi kujinufaisha wenyewe, katu hawatufai! Waende salama.
 
Back
Top Bottom