Kituo nilichopigia kura mimi wale makarani waongozaji bure kabisa, wamenilekeza milango zaidi ya minne na huko kote hakukuwa na jina langu. Nikawaambia, acheni ubabaishaji, nitajihudumia mwenyewe.
Nikapitia milango yote 15; pale kituoni nikisoma kila jina kwa kutrack kialphabet, baada ya milango tisa nikaona jina Mama mdogo, moyo ukatulia, nikapiga kura kuchagua rais, mbunge na diwani wangu! Ajabu yule msimamizi hata hakuniuliza kamna najua kusoma na kuandika, wala kunielekeza tick niweke chumba gani.
Niliamua kukaa pale kuwasaidia wazee na wasiofahamu kusoma na kuandika wapatao kumi na watano, I repeat 15, kutambuwa wamepangwa kuingia chumba gani. Nimechukia sana kufanya kazi za hawa makarani waongozaji wakati wao wamekaa tu wanatumbua macho na kunywa soda! Ila nimefurahi nimetimiza wajibu wangu wa kiraia, na niliowasaidia, nilishia kuwaonyesha milango husika, sijaifluence kura zao.
Rai yangu, tume ya uchaguzi naona hawajifunzi kutokana na makosa, kwani errors za 1995, 200 na 2005 zinajirudia leo 2010, hawakuwa wamejitayarisha kikamilifu!!