Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Huu ni mwanzo mzuri kabisa. Matumaini ya ushindi yanazidi kuongezeka.
 
Nataka kulia kwa furaha, shemejio kaniletea kahawa hapa ya jioni, imepoa hata sijainywa!!! raaaaahaa kweli kweli, ina maana pale alipopita mchana kwenye foleni ubungo ndo ilikua mara yake ya mwisho???
 
Masanduku ya Kura yakamatwa!


Masanduku ya Kura yakamatwa Sunday, 31 October 2010 14:04
Mwananchi

Israel Mgussi na Geroda Mabumo ,Dodoma

HALI ya uchaguzi mkuu jimbo la Dodoma mjini imetia dosari baada ya kukamatwa kwa masanduku ya kupigia kura yakiwa na karatasi za kura kwenye nyumba ya mtu binafsi nje kabisa na kituo cha kupigia kura.

Masanduku hayo mawili yaliyokuwa yamesheheni karatasi za kura ndani yalikamatwa juzi mtaa wa Majengo mjini Dodoma majira ya saa mbili usiku kwenye nyumba ya Mwalimu Walburga Tarimo ambaye pia ilifahamika kuwa ndiye atakayekuwa msimamizi wa kituo cha uchaguzi cha Makole kata ya makole.

Mwananchi ambayo ilifika eneo la tukio ilishuhudia upekuzi ulioongozwa na Afisa upelelezi makosa ya jinai wa wilaya ya Dodoma mjini(OC-CID) Jonathan Shanu ambapo masanduku hayo mawili yalibainika na kuchukuliwa moja kwa moja hadi kituo cha polisi cha kati pamoja na mtuhumiwa kwa ajili kutolea maelezo.

Baada ya kufika kituo cha polisi cha kati masanduku yalifunguliwa ili polisi na mashuhuda waweze kujiridhisha kama karatasi zilizokuwamo ndani zilikuwa zimeshawekwa alama zinazoonyesha kuwa kura zimeshapigwa au hapana.

Hata hivyo baada ya masanduku hayo kufunguliwa karatasi zilizokuwamo ndani zilikutwa bado hazijatiwa alama ya vema wala alama yoyote inayoonyesha dhamira ya kumpigia mtu fulani kura na zaidi ya hapo mtuhumiwa alisema kuwa yeye alilazimika kurudi na masanduku na vifaa vyote vya kupigia kura kutokana na kukosekana kwa ulinzi katika kituo cha kupigia kura.

"Mimi sikufahamu kuwa hili ni kosa na nililazimika kurudi na vifaa vyote hivyo vya kupigia kura kwa sababu giza lilishaingia katika kituo cha kupigia kura na hapakuwepo na ulinzi wowote wa askari hivyo kwa usalama wangu na wa vifaa niliamua kurudi navyo nyumbani.",alisema mwl.Tarimo ambaye ndiye msimamizi wa kituo cha uchaguzi Makole .

Haikuweza kufahamika sababu ambazo zilifanya mtuhumiwa ashindwe kuwasiliana na msimamizi wa uchaguzi au kwa vyombo vingine vya usalama ingawa ilibainika kuwa katika kituo husika kulikuwepo na askari ambaye alikuwa amepangwa kutoa ushirikiano wa kiulinzi na usalama katika kituo tajwa.

Kwa upande wake msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Dodoma mjini Suzane Bidya alisema yeye hana taarifa juu ya kukamatwa kwa masanduku hayo na kusisitiza kuwa hakuna sheria inayomruhusu mtu yoyote kwenda kulala na vifaa vya uchaguzi nyumbani kwake.

"Mimi sina taarifa hizo,hata hivyo muulize huyo mama nani kamruhusu kwenda na masanduku na hivyo vifaa vya kupigia kura nyumbani kwake,akueleze maana mimi sijatoa ruhusa hiyo na wala sina ruhusa ya kumruhusu mtu kwenda na vifaa vya kupigia kura nyumbani kwake sasa yeye kwanini aende navyo nyumbani.",alisema Bidya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Steven Zelothe alipotakiwa azungumzie tukio hili alisema kuwa hakuna taarifa inayohusu tukio hilo ambayo imeshamfikia.

Aidha baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na kufanyika kwa uhakiki wa karatasi zilizokuwemo ndani ya masanduku hayo,yalichukuliwa na kupelekwa kwenye kituo husika cha kupigia kura chini ya ulinzi wa polisi,huku OC-CID Dodoma mjini Jonathan Shanu akisema kuwa maelezo yameshachukuliwa lakini yeye hawezi kutoa maelezo yoyote kwa sababu yeye sio msemaji wa Polisi.

Mbali na dosari hiyo upigaji kura katika vituo mbalimbali vya majimbo ya Dodoma mjini,Bahi na Chamwino imeendelea vizuri huku kukiwa na hali ya utulivu na upigaji kura wa amani.
 
Superman, haya matokeo ninayoyaona?? nataka nichukue kalamu na daftari nianze kunakili

hayo ni matokeo ambayo mdau anadai ni ya awali toka Mwanza.

Hebu yafanyie analysis kuyajumlisha na kuona totals ziko vipi, kisha weka % tuone Synovet, Redet au TCIB nani anakaribia.
 
Habari zinasema kwamba katika Kata ya Saranga hakuna form namba 21B ya matokeo ya Ubunge. Hii ni katika jimbo la Ubungo.
 
Kumbe tunatakiwe tuseme nini tena? si ndio hivyo CCM anavutwa na CHADEMA??? AU hujaelewa mpwa?
 
Mbona matokeo hamsemi tena? Semeni kama yanavyoonekana hapo!


Mkuu usiwe na wasiwasi tuko kwa ajili yako.

Matokeo rasmi hayajaanza, hayo ni kwa mjibu wa SMS na internal networks.

TV hazijaanza kutangaza bado.

Sijui Channel 10 maana kwangu inafreeze.
 
Mkuu usiwe na wasiwasi tuko kwa ajili yako.

Matokeo rasmi hayajaanza, hayo ni kwa mjibu wa SMS na internal networks.

TV hazijaanza kutangaza bado.

Sijui Channel 10 maana kwangu inafreeze.

Yanarushwa kwa pause. Nitajumlisha soon kuwapa hapa hapa. Sasa hivi
 
Matokeo ya Uraisi Zanzibar:


1) Kituo Cha Bwawani

Maalaim seif Shariff CUF 593

Dr Shein CCM 141
 
Maswa kuna mdau amebambwa na karatasi halali la kupigia kura akizitumbukiza nyingi baada ya kupewa na msimamizi. Na alipobanwa alisema kuwa walifundishwa.

Mambo hayo

Source: ITV
 
Hata hivyo wananchi wanalalamika kwa nini police hawajaawakamata wahusika wengine?
 
Back
Top Bottom