Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Mkuu, hawa MODS zijui vipi leo.

Nimejaribu kuwasiliana na moja lakini naona bado hawajaziunganisha.

Kumekuwa na dublicate ya threads nyingi sana . . . .

Naanza kuchoka Mkuu.

lakini tujitahidi tu . . . .

Pole sana mkuu. Hata mimi nakuonea huruma. Kazi hii nzuri uliyoifanya sasa imeharibika kabisa. Hivi kwa nini watu badala ya kuweka matokeo hapa wanakimbilia kuanzisha thread mpya? Hata wale tunaofuatilia tunakosa mwelekeo.

Hope Mods watalishughulikia hili haraka sana. Yaani sijui hali itakuwaje hadi kufikia kesho asubuhi!
 
Jamani, hawa chanel ten mbona siwaelewi, naona kama vile haya matokeo haya yana namna, kwani baadhi ya maeneo yameripotiwa tofauti, ngoja nitafute hao wengine wamesemaje ili niattach hapa
 
Hiyo hapo juu inaonekana imechakachuliwa tayari...................madiwani wapate nyingi lakini urais na ubunge pungufu....somethin ain't right!

Mkuu hata mimi nakubaliana na wewe something is wrong yani kura za udiwani nyingi namna hiyo halafu za urais na ubunge washinde dih ngoja tuone
 
Meya Manispaa ya Arusha:

Mimi niko hapa Kata ya Kimandolu anakotoka Meya wa manispaa ya Arusha ndugu Laurent Hedi. Tayari matokeo yametoka na ameshindwa vibaya na Ndugu Estomih malla wa CHADEMA.
Katika kata hii ya Kimandolu CHADEMA inaongoza kwa matokeo yote kuanzia Rais, Ubunge na Diwani.
Kwa sasa hapa mtaani hakufai na hakuna kulala wananchi wameingia mtaani wanashangilia ushindi.
Figure nitawapatia baadaye kidogo
 
The best thing ni kwamba, tukiwaacha tunawaacha kabsaa, so wakija jumlisha lazima kitaeleweka tu!!! MORE UPDATES PLS
 
Kutoka Arusha.....

Gerald2008 said:
Mimi niko hapa Kata ya Kimandolu anakotoka Meya wa manispaa ya Arusha ndugu Laurent Hedi. Tayari matokeo yametoka na ameshindwa vibaya na Ndugu Estomih malla wa CHADEMA.

Katika kata hii ya Kimandolu CHADEMA inaongoza kwa matokeo yote kuanzia Rais, Ubunge na Diwani.

Kwa sasa hapa mtaani hakufai na hakuna kulala wananchi wameingia mtaani wanashangilia ushindi.

Figure nitawapatia baadaye kidogo
 
Hii ni kutoka Mwanza, but confirmation will be highly desirable.

Kokol said:
Kwa taarifa nyepesi toka mwanza nyamagana- masha wa ccm yuko hoi bin taabani mbele ya mgombea wa chadema kwa mbali sana. Karibu sehemu zote za udiwani chadema washachukuwa ushindi tayari. Pia ilemela dialo yuko kwenye intesive care unit, chadema inaongoza kwa juu sana. Hivyo mwanza wamempeleka slaa ikulu.
 
Mkuu, hawa MODS zijui vipi leo.

Nimejaribu kuwasiliana na moja lakini naona bado hawajaziunganisha.

Kumekuwa na dublicate ya threads nyingi sana . . . .

Naanza kuchoka Mkuu.

lakini tujitahidi tu . . . .

Mkubwa Maxence kasema yupo analifanyia kazi! Pamoja sana
 
Ruvuma:

URAIS
Kituo: Shule ya Msingi Peramiho "B" KATA YA MAPOSENI
CHADEMA 116
CCM 82
CUF 1
APPT 1

UBUNGE: CCM imemwacha CUF mbali sana. Jenista Mhagama anaongoza.

Kituo: Jengo la Maarifa ya Nyumbani: KATA YA MAPOSENI
URAIS:
CCM 147
CHADEMA 42
UBUNGE: KAMA HAPO JUU
 
Bukoba Vijijini:

Bukoba vijijini
Kituo Nkindo

Chadema 188
CCM 144
CUF 1

Udiwani
Chadema 169
CCM 68
 
Mkubwa Maxence kasema yupo analifanyia kazi! Pamoja sana

Mkuu,

Hii hali inakera sana. Yaani matokeo yanatupwa tupwa hovyo. Nakumbuka kwamba niliomba toka mwezi wa 8 kwamba tuwe na sehemu moja watu wamwage matokeo hapo. Sasa hivi hali inakatisha taamaa kutoa updates and kufuatilia. But Sperman has done wonders. Keep it up mkuu. We will lend a supporting hand from now on...
 
SUA Morogoro!

Yafuatayo ni matokeo ya kura YA Urais iliyopigwa katika Campus ya SUA (Main) kwa vyama viwili muhimu

GUEST WING A
CHADEMA= 44
CCM = 44

GUESTWING B
CHADEMA = 64
CCM = 56

MULT-PURPOSE HALL A
CHADEMA = 54
CCM = 31

MULTI-PURPOSE HALL B
CHADEMA = 62
CCM = 50

MULTI-PURPOSE HALL C
CHADEMA = 64
CCM = 47

Nawasilisha wakuu
 
Back
Top Bottom