LIVE: Hapa Madrid na Atretico kule Monaco na Juve

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,649
Reaction score
4,786
Atretico Madrid wametembea kwa miguu kuelekea katika Dimba la Estadio Santiago Bernabeu ambapo ndipo nyumbani kwa mabingwa watetezi wa UCL na pia ndio wenye rekodi ya kubeba ndoo hii mara kumi wakifuatiwa na AC MILAN hapa nawazungumzia Los Blancos Real Madrid Musica International...

Madrid wakiwa na kocha boora mwenye mafanikio akiwa mchezaji na pia kama Kocha Mr European Nightmare big Caro Ancelotti watakuwa na kazi ya kukabili kikosi cha Atretico kinachonolewa na mcharuko Diego Simeone.

game ya kwanza iliisha kwa pacha tasa...
hivyo kwa namna yeyote ile leo lazima mtu atage na aage mashindano.
fainali ya mwisho ya mashindano haya tulishuhudia Atretico akipiga mbizi kwenye kokoto baada ya kukubali kipigo cha mbwa koko ndani ya uzio cha goli 4-1 hivyo kwa kibano kile ndicho kinafanya mechi hii iwe na mvuto kwani Madrid anataka kuendeleza Hishma ile hali Atretico anataka kufuta uteja.

watu pekee naotaka kuwadekea leo ni Christiano Ronaldo na mkuu wa Ndevu Arda ustaadh Turan...
.......................................................................

wajukuu wa Lavechia Signora kutoka katika viunga vya Torino nchini Italia wametua nchini Ufaransa na hivi navyoandika wapo katika mji wa Monaco wakijiandaa kumaliza kazi walioianza ktk Dimba la Juventus nchini Italia...

Juve kama Juve wakiongozwa na golikipa boora kabisa Gianluigi Gigi Buffon nawapa turufu yangu leo kwa kuwa wapo kamili kila Idara.

mpaka kufikia hapa Juve waliwaandamisha klabu ya Dortmund ya nchini Ujerumani.
ikumbukwe Juve wana kiungo boora kabisa anayezeheka na ubora wake Uncle Pirlo huku akizungukwa na watu kama Claudio Marchisio, Giorgio Chielini, Vidar Pardo, Patrice Evra, Alvaro Moratta lakini pale mbele yupo Carito nguli ngoma ngumu Oscar Carlos Tevez ambae anaweza kufunga goli aina yoyote, kwa mguu wowote na hata kwa kichwa.
FORZA JUVE...

the countdown has began....
 
Atretico akimtoa Real Madrid basi ntajilamba sikio kwa Ulimi...
 
Monaco akimtoa Juventus basi Sumaku itanasa kwenye Mbao..

mie ndo Gang Chomba msomali nilielowea Tanzania
 
Mungu Ibariki Athletico Madrid.

Amen!

CC everlenk na Watu8. Njooni tuwaombee dua baya watani zetu.
 
Last edited by a moderator:
Mleta uzi umekuja kishabiki hapa. Nenda Real Madrid special thread ukashabikie huko.
Kwanza hujui hata unacho andika hapa. ATRETICO ndio nini sasa.
Kwa taarifa yako tu hii gemu ni sare ya magoli na Real ndipo anatoka hapo.
 
CC: Viper Mourinho Ntuzu Pdidy MosDef salamander BAK janjaweed juve2012 TUPACified rrondo malafyale ndetichia juan moses belo Ziroseventytwo
juve2012 pachanya
 
Mleta uzi umekuja kishabiki hapa. Nenda Real Madrid special thread ukashabikie huko.
Kwanza hujui hata unacho andika hapa. ATRETICO ndio nini sasa.
Kwa taarifa yako tu hii gemu ni sare ya magoli na Real ndipo anatoka hapo.

jina lako linaeleza uhalisia wa ubongo wako...
 
Diego Simeone leo vijana wake watafanya mambo yao
 
Atretico akimtoa Real Madrid basi ntajilamba sikio kwa Ulimi...

Mechi Saba walizokutana msimu huu Carlo Ancelotti ameshinda kumfunga huyu Diego Simeone unasemaje leo kirahisi hivyo kuwa Atletico anatoka...?
 
Mechi Saba walizokutana msimu huu Carlo Ancelotti ameshinda kumfunga huyu Diego Simeone unasemaje leo kirahisi hivyo kuwa Atletico anatoka...?

nasema kirahisi kabisa tena kidali wazi kwa kuwa Carlo Ancelotti ni mchezaji wa zamani wa AC Milan aliebeba hili kombe akiwa kama mchezaji na pia akalibeba akiwa kama kocha wa AC Milan hiohio...
 
Atretico akimtoa Real Madrid basi ntajilamba sikio kwa Ulimi...

-Leo utajilamba hata nywele za kichwani.
-Real anaaga kwa namna ya ajabu sana huku wakilia machozi ya damu.
-Najua upo Real sababu ya Ancelot ila nikwambie kwamba leo Atletico anachapa mtu.
 
Mleta uzi umekuja kishabiki hapa. Nenda Real Madrid special thread ukashabikie huko.
Kwanza hujui hata unacho andika hapa. ATRETICO ndio nini sasa.
Kwa taarifa yako tu hii gemu ni sare ya magoli na Real ndipo anatoka hapo.

Sare yoyote ndo itakuwa juhudi kubwa sana kwa Real zaidi ya hapo ni Real kufungwa leo.
 
naomba kuuliza sheria mpya ya uefa champions kuanzia msimu mpya inasemaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…